Tanzania bila Upinzani, tuko sahihi au tumepotea? Tujadili

KooZito

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2020
Posts
397
Reaction score
1,378
Happy New Year Brothers and Sisters.

NDUGU zangu, Katiba yetu inaweka bayana kuwa nchi yetu itaongozwa na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Kama Taifa tulikubaliana kwa pamoja juu ya hili na mwaka 1992 tulianzisha mfumo huo ambapo mwaka 1995 tulifanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi.

Toka wakati huo hadi sasa tumeishi ndani ya mfumo huo licha ya Chama Cha Mapinduzi, CCM kutawala kwa kupewa ridhaa na umma kuunda Serikali iwe ni kwa haki au haramu (bao la mkono).

Kwa kipindi chote hicho tumeona faida na hasara ya mfumo huu. Lakini zaidi tumeona faida ya uwepo wa vyama vingi hapa nchini.
Faida moja kubwa ninayoweza kuitaja hapa ni kwamba wapinzani wamekuwa kama watch dog kwa watawala. Kwamba wamekuwa wakisaidia kukosoa watawala na Serikali, wameibua maovu yaliyokuwa yamefichika hasa rushwa na ufisadi.

Mzee Mkapa na Jakaya wameishi vizuri sana na Upinzani maana kwa kuheshimu na kutii Katiba hawakuwafanya kuwa maadui. Hii ni kwa sababu waliwaona kama askari wa Siri waliowaonesha madhaifu yao hata kama walishindwa kuchukua hatua.

Bila hawa wapinzani umma usingejua ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma zilizokwapuliwa maeneo mbalimbali ambayo yamekuja kushughulikiwa na Rais Magufuli kwa umakini.

Kwa mantiki hiyo kama kuna kiongozi angetakiwa kuwa swahiba wa upinzani basi ni Rais Magufuli maana wanamsaidia kupambana na ufisadi na mafisadi.

Ninaweza kusema kwamba ni ufisadi mdogo sana alioibua Magufuli na kushughulikiwa na sana sana itakuwa ni ufisadi wa kimfumo. Lakini ukitazama kwa jicho la akili utagundua kwamba Magufuli anajibu hoja za Upinzani kwa vitendo.

Ujenzi wa SGR ni hoja ya Dk. Slaa 2010 ambapo wakati huo alipingwa na kubezwa mno na buku7 za Lumumba. Leo inajengwa na Slaa ni Balozi. Buku7 kimyaaa kwa aibu. Mifano ni mingi.

Swali kubwa linabaki kuwa ni kwa nini JPM sasa hataki kuwaona wapinzani na Upinzani? Anadai wanamkwamisha, kwa vipi? Kwa nini asisikilize hoja zao na kuzipima kama zina masilahi kwa wananchi wake azichukue au kuzipuuza? Kwa nini awafanye maadui kiasi Cha kufikia maungo yao? Je, sasa Magufuli ataibua mwenyewe kasoro katika utawala wake na kuzirekebisha? Hii imewezekana wapi duniani mtu kuona chunusi usoni bila kutumia kioo?

Kwa mtazamo wangu ni kwamba woga huu wa Magufuli na uadui wake kwa wakosoaji ina Siri nzito. Inawezekana kuna jambo baya na la hatari anayofanya JPM kwa nchi hii na kificho pekee ni ukali, kuchukia wapinzani na wakosoaji lakini pia kwa kujificha chini ya mbawa za dini ya Mungu. Wapo wanaodai sasa JPM ni miongoni mwa mabilionea wachache barani Afrika.

Rai yangu kwa Watanzania ni kwamba bado kuna haja kubwa ya uwepo wa upinzani na wakosoaji. Tuendako tutajua kinachofichwa na JPM kwa chuki yake kwa Upinzani na wapinzani. Mimi naona tumepotea njia kwa kuwatenga wapinzani na kuwaona maadui.

Nawasilisha!!!
 
"Tatizo matusi" andika insha isiyopungua maneno 20 kwa kutumia nukuu hii.
 
Uko vizuri pale sheria zinapopuuzwa na watawala kwa kisingizio cha mamlaka ni tatizo majibu yapo ni muda tu tutajua ni nini kimesababisha chuki kwenye siasa ya mfumo wa vyama vingi hasa vyama vikubwa.
 
Uko vizuri. An opposition political party, in action, acts as a mirror to the rulinga party (government). If we have no opposition part (ies), the government is not corrected through a mirror, so it acts anyhow.
 
Simply ni kuwa Magu hakustahili na hastahili kwenye nafasi ya urais, na isitoshe sio mtu muadilifu. Ukiona mtu hataki uwazi, na anawachukia waziwazi wanaoweka wazi uovu, ujue mtu huyo sio muadilifu na ni muovu. Hilo la yeye kuwa ni bilionea ni kweli, na ndio hasa sababu ya yeye kuhujumu wapinzani ili uovu wake usiwe hadharani.
 
Happy New Year Brothers and Sisters.

NDUGU zangu, Katiba yetu inaweka bayana kuwa nchi yetu itaongozwa na mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Kama Taifa tulikubaliana kwa pamoja juu ya hili na mwaka 1992 tulianzisha mfumo huo ambapo mwaka 1995 tulifanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi.

Toka wakati huo hadi sasa tumeishi ndani ya mfumo huo licha ya Chama Cha Mapinduzi, CCM kutawala kwa kupewa ridhaa na umma kuunda Serikali iwe ni kwa haki au haramu (bao la mkono).

Kwa kipindi chote hicho tumeona faida na hasara ya mfumo huu. Lakini zaidi tumeona faida ya uwepo wa vyama vingi hapa nchini.
Faida moja kubwa ninayoweza kuitaja hapa ni kwamba wapinzani wamekuwa kama watch dog kwa watawala. Kwamba wamekuwa wakisaidia kukosoa watawala na Serikali, wameibua maovu yaliyokuwa yamefichika hasa rushwa na ufisadi.

Mzee Mkapa na Jakaya wameishi vizuri sana na Upinzani maana kwa kuheshimu na kutii Katiba hawakuwafanya kuwa maadui. Hii ni kwa sababu waliwaona kama askari wa Siri waliowaonesha madhaifu yao hata kama walishindwa kuchukua hatua.

Bila hawa wapinzani umma usingejua ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma zilizokwapuliwa maeneo mbalimbali ambayo yamekuja kushughulikiwa na Rais Magufuli kwa umakini.

Kwa mantiki hiyo kama kuna kiongozi angetakiwa kuwa swahiba wa upinzani basi ni Rais Magufuli maana wanamsaidia kupambana na ufisadi na mafisadi.

Ninaweza kusema kwamba ni ufisadi mdogo sana alioibua Magufuli na kushughulikiwa na sana sana itakuwa ni ufisadi wa kimfumo. Lakini ukitazama kwa jicho la akili utagundua kwamba Magufuli anajibu hoja za Upinzani kwa vitendo.

Ujenzi wa SGR ni hoja ya Dk. Slaa 2010 ambapo wakati huo alipingwa na kubezwa mno na buku7 za Lumumba. Leo inajengwa na Slaa ni Balozi. Buku7 kimyaaa kwa aibu. Mifano ni mingi.

Swali kubwa linabaki kuwa ni kwa nini JPM sasa hataki kuwaona wapinzani na Upinzani? Anadai wanamkwamisha, kwa vipi? Kwa nini asisikilize hoja zao na kuzipima kama zina masilahi kwa wananchi wake azichukue au kuzipuuza? Kwa nini awafanye maadui kiasi Cha kufikia maungo yao? Je, sasa Magufuli ataibua mwenyewe kasoro katika utawala wake na kuzirekebisha? Hii imewezekana wapi duniani mtu kuona chunusi usoni bila kutumia kioo?

Kwa mtazamo wangu ni kwamba woga huu wa Magufuli na uadui wake kwa wakosoaji ina Siri nzito. Inawezekana kuna jambo baya na la hatari anayofanya JPM kwa nchi hii na kificho pekee ni ukali, kuchukia wapinzani na wakosoaji lakini pia kwa kujificha chini ya mbawa za dini ya Mungu. Wapo wanaodai sasa JPM ni miongoni mwa mabilionea wachache barani Afrika.

Rai yangu kwa Watanzania ni kwamba bado kuna haja kubwa ya uwepo wa upinzani na wakosoaji. Tuendako tutajua kinachofichwa na JPM kwa chuki yake kwa Upinzani na wapinzani. Mimi naona tumepotea njia kwa kuwatenga wapinzani na kuwaona maadui.

Nawasilisha!!!
Mko sahihi sana;
Miezi 2 tu baada ya uchaguzi maendeleo yenu yanaikaribia Poland.
 
Back
Top Bottom