Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 17,048
- 22,790
Mwaka juzi (2007) nilikuwa nyumbani nikiwa namwuguza ndugu yangu wa karibu sana. Ikafika wakati wa sikukuu ya Krismas, na nikaamua nimnunulie mgonjwa huyo zawadi ya viatu, lakini nilitaka kum-surprise; hata hivyo sikuwa najua saizi ya miguu yake sawasawa. Nikabshiri kuwa huenda atakuwa anavaa namba 8, hivyo nikanunua pea nzuri sana ya bei nzuri pia. Kwa bahati mbaya, mgonjwa yule alikuwa anavaa namba 7 kwa hiyo namba nane ikampwaya. Nikasema hakuna tatizo ngoje niende nikabadilishe kule dukani nilikonunua nipewe namba 7. Dah!!, pamoja na kurudi nikiwa na sales receipt yangu, tena siku hiyo hiyo niliyokuwa nimenunua viatu hivyo, mwenye duka alinikatalia kata kata. Nikaamua kutoa viatu vile kwa mtu mwingine tu, na badala yake ninunue pea nyingine ya namba 7 kwa ajili ya mgonjwa wangu.
Huo ni mwaka mzima umepita tangu hayo yanipate. leo hii nikiwa pale kwa shigongo nikatutana na hii sales receipt inayoonyesha kiuwa ukishanunua kitu, basi huwezi kukirudisha, ndipo nikakumbuka ule mkasa wangu. je Tanzania tuna utaratibu wowote wa kumlinda mlaji iwapo atanunua kitu ambacho hakikidhi mahitaji yake ama kwa ubora au kwa sababu yeyote ile?