Koba,
Mfano wewe ni Mmiliki wa kundi la Ng'ombe. Nikaja kwako nikakulaghai uniuzie majike na baadhi ya madume. Na kwa uelewa wako wa wakati huo ukakubali kukodisha kundi lote kwa sharti la kuwarejesha baada ya miaka kadhaa. Masharti haya hayakuangalia kurejesha pia vizazi vipya vitakavyozaliwa, maziwa na bidhaa za nyama au ngozi kwa wale watakaoshinjwa. Wewe utarejesha tu kundi kama ulivyolichukua!
Uhusiano wetu ukadumishwa na ikafikia mahali hata nguvu kazi yako hutegea kizazi changu. Bahati nzuri kila mwaka wake zangu hujifungua. Ila kwa bahati mbaya watoto wetu huathiriwa sana na kwashiokor na utapiamlo na hata kupoteza maisha. Kwako watambua umuhimu wa wanangu kama nguvu kazi yako. Na pia wajua fika haya si magonjwa bali ukosefu wa msosi. Kwa kuwa unao ng'ombe wangu wanaokupa maziwa mengi na watambua maziwa kama chanzo cha protein yatamaliza matatizo ya wanangu (nguvu kazi yako)ukaanzisha utaratibu wa kuchangi lita 4000 kila mwaka wake zangu wanapojifungua.
Sasa swali Bw. Koba; nani hapa anamtegemea mwenziwe na nani anamchangia mwingine?
Tuje kwenye hali halisi ya kinachotokea hapa Danganyika. Tuanze na mifano hai midogo midogo kuhusu wafadhili wa humu humu Republic of Danganyika. Rostam Aziz (King Creator)wakati akiwa mtu wa kawaida kabisa na karibu sawa na kabwela alichukua mikopo mingi toka Bank ya NBC. Enzi hizo ikiwa Chini ya Chama na Serikali na RA akiwa kama mpambe wa CCM. Huhitaji mpaka huoji kujua kwamba Mikopo ya Mabilioni ilitolewa kwa Vi-MEMO. Baadhi ya Fedha za mikopo hiyo ilikujatumika baadaye kununua Makampuni yaliyobinafsishwa kama Bora na Viwanda vingine. Viwanda vyote chini ya RA vimegeuzwa Godowns na Madeni ya NBC (Mtaji wa RA) haujawahi fuatiliwa. Alipomega sehemu za madeni haya akasaidia Chama akaitwa MFADHILI MKUU NA TENA AKAPEWA M/HAZINA CHAMA...!
Spain Master, Dalali Bingwa toka shule ya Kariakoo, namzungumzia Manji wa Quality Group alichukua bilion 6 akanunua jengo la PPF na ndani ya Miezi 12 akawauzia haox2 jengo lilex2, eneo lilex2 kwa bilion 43.2
Manji kwa kujua umbumbumbu wa TRA officers. Wakati wa kuleta machine za kuchezesha KITITA alipitisha Terminal fulani hizo machines free of tax. Waliloambiwa hawa vijana wa Danganyika ni kuwa hizo zilikuwa Screen za Computer ambazo kwa sheria ya miezi hiyo screen zilikuwa hazilipiwi ushuru. Thamani ya Mzigo uliopita ilikuwa yapata TShs. 300 milioni! Hadi leo naandika KITITA imechezeshwa mara nyingi, watu wamelambwa sana tu TShs. zao lakini la kustaajabisha hata mara moja mshindi hjawahi patikana. Na sasa hii kamri nasikia imepigwa marufuku. Wakina Koba walipopewa ofa CCM Kirumba wakamwita MFADHILI MKUU WA MICHEZO TANZANIA
Twende kwa wafadhili wa nje ya Danganyika. Nimepeni feelings zenu kama somo la juu linaleta mantiki kabla sijatoka nje ya Danganyika. Kisha nitaleta hii mada but in HAKUNA MLO WA MCHANA WA BURE Wafadhili daima wanarejesha sehemu ndogo sana ya jasho letu kwa jina la msaada, kuchangia n.k