Tanzania Economic Freedom Advocacy (TEFA)

Tanzania Economic Freedom Advocacy (TEFA)

made in tanzania_

Senior Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
114
Reaction score
147
TUNACHOPIGANIA SASA;-
Serikali kwa kushirikiana na waekezaji wazalishe umeme wa megawatts 100,000 na zaidi ili kukuza maradufu Saughall za uchumi

Unit moja ya umeme iuzwe sh 50 kwa matumizi ya nyumbani, sh 25 kwa matumizi ya biashara kwa wale wenye leseni, tin number na mashine za efd, sh 15 kwa matumizi ya hospitali, shule na ofisi za serikali na sh 10 kwa matumizi ya viwanda

Serikali itafute waekezaji wajenge smelting zifuatazo kama njia ya kukuza viwanda na kuondoa umaskini Tanzania
  • Mwekezaji asijenge tu kiwanda cha kuchimba gesi asilia (drilling) na refinery bali ajenge na kiwanda cha petrochemical
  • Serikali itafute mwekezaji wa kujenga oil refinery kwa matumizi ya ndani na nje.
  • Serikali itafute waekezaji wa kujenga smelting za chuma kwa matumizi ya ndani na nje
  • Serikali itafute waekezaji wa kujenga smelting za copper kwa matumizi ya viwanda vya ndani na nje ya nchi
  • Serikali itafute waekezaji wa kujenga smelting za aluminium kwa matumizi ya viwanda vya ndani na nje
  • Serikali itafute waekezaji wa kujenga smelting glass kwa matumizi ya viwanda vya ndani na nje.
  • Serikali itafute waekezaji wa kujenga viwanda vya karatasi vya awali (Paper and pulp).
  • Serikali itafute waekezaji wa kujenga smelter za semiconductor na PCB fabricated kwa matumizi ya viwanda vya ndani na nje.
Unit moja ya maji kuuzwa sh 400 mpaka 500
kupiga marufuku wale wanaouza maji na magari mitaani

Huduma za dialysis ziwe bure asilimia 100 kwa kila wilaya nchi nzima kwenye hospital za serikali

Tender zote za serikali za ujenzi wa miundombinu wapewe kipaumbele wazawa tofauti na sasa wazawa hawapewei kipaumbele mfano ujenzi wa miundombinu yote ya barabara na wapewe makampuni ya wazawa kama njia ya kuwajengea uwezo, na miradi mikubwa kama reli ya umeme serikali ifanye mkakati wa kuwajengea uzoefu.

Viwanda vya Tanzania viajiri wazawa kama kipaumbele kwenye core business tofauti na sasa vimejaza wageni huku watanzania waki-tretiwa kama watu wasio na thamani.

Shule za msingi za serikali kuongeza wigo wa masomo ya kingereza (english) na kuwa matatu nayo ni kingereza, hesabu kwa kingereza na science kwa kingereza huku kiswahili kikifundishwa masomo mawili kiswahili na uraia-hii haitawaacha nyuma watoto wa kimaskin kama ilivyo sasa kwamba kuna watoto wanamaliza msingi wakiwa na msingi mzuri wa lugha ya kingereza huku wengine wakiwa na msingi mbovu wa lugha ya kingereza na mitihani iwe sawa kwa shule za msingi za serikali na binafsi ambazo sio za kimataifa.

Serikali kutonunua magari ya kifahari kwa wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi na budget hio kuielekeza sehemu zenye uhitaji.

Kuanzisha mamlaka itakayohusika na upimaji wa makazi kama ilivyo TRA, tunapendekeza iitwe Tanzania agency of rural and urban planning (TARUP) itahakikisha watu wanajenga kwa kufuata mpangilio ili iwe rahisi kuwasambazia gesi majumbani, na huduma nyingine za kijamii na itakuwa na kazi zifuatazo;-
  • Kupima nchi nzima.
  • Kuhakikisha yeyote anayejenga anafuata mipango miji.
  • Kuhakikisha kwenye miji, na vijiji kunakuwa na zoning na sio sasa unakuta gesti imejengwa katikati ya makazi ya watu.
  • Kuhakikisha kwenye makazi yote kunapita miundombinu muhimu kama fiber, maji, n.k inapitak kwa kila mwenye nyumba.
  • Kutoa elimu ya mipango miji na faida zake kwa wananchi.
  • Polisi wa mipango miji watahakikisha wanaojenga wanafuata masharti na kuwatia nguvuni wote wanaojenga kiholela a.k.a wakaidi.
  • Mapato yote ya majengo watakuwa wanakusanya wao.
TEFA (Tanzania Economic Freedom Advocacy) ni wakina nani????
Tuna malengo ya kupigania Tanzania ili kuondoa umaskini unaosumbua kaya nyingi.

MAONO (Vision)
Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

NJIA YA KUFIKIA (Mission)
Kuzalisha umeme mwingi kama njia ya kukuza umeme
 
Hiyo ya pili safi sana ila hapo kwenye ya kwanza huwez panga terms kwa investors...

Labda mngeomba serikali itoe nafasi kwa wazawa wenye uwezo wapewe funds access waweze kusambaza kama hao wengine.. may be ,15%


Hiyo ya pili, hakuna haja ya Mamlaka, ni agency tu wa kupima na sio kuongeza budget kubwa kias utasmbiwa kuna changamoto ua fedha- mfano BRELA etc.

Pambaneni mkuu
 
  • Thanks
Reactions: Ame
TEFA (Tanzania Economic Freedom Advocacy) ni wakina nani
Ni jamii yenye malengo ya kupigania Tanzania itumie rasilimali zake kiukamilifu ili kuondoa umaskini unaosumbua kaya nyingi.

MAONO (Vision)
Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda

TUNACHOPIGANIA SASA
Kwenye mradi wa gesi asilia ambao mazungumzo bado yanaendelea tunapendekeza mwekezaji asijenge tu kiwanda cha kuchakata gesi asilia (natural gas refinery), bali ajenge na kiwanda cha petrochemical kwa pamoja.

Mwekezaji azalishe megawatts laki moja (1,000,000) za umeme kutoka kwenye gesi asili, na bidhaa zitokanazo na gesi asilia kama hydrogen.

Kuanzisha mamlaka itakayohusika na upimaji wa makazi, ili kuhakikisha watu wanajenga kwa kufuata mpangilio ili iwe rahisi kuwasambazia gesi majumbani na huduma nyingine za kijamii
  • Kupima nchi nzima
  • Kuhakikisha yeyote anayejenge anafuata mipango miji
  • Kuhakikisha kwenye miji, na vijiji kunakuwa na zoning na sio sasa unakuta gesti imejengwa katikati ya makazi ya watu
  • Kuhakikisha kwenye makazi yote kunapita miundombinu muhimu kama fiber, maji, n.k inapitak kwa kila mwenye nyumba
  • Jeshi la polisi la mipango miji litahakikisha wanaojenga wanafuata masharti na kuwatia nguvuni wote wanaojenga kiholela a.k.a wakaidi
  • Mapato yote ya majengo watakuwa wanakusanya wao
Yaani uwasambazie gas wakati 2030 inatakiwa iswepo kwenye matumizi? Halafu hayo mambomba na gharama zake utalipa na kitu gani?

Ebu acheni mambo ya aibu!
 
Yaani uwasambazie gas wakati 2030 inatakiwa iswepo kwenye matumizi? Halafu hayo mambomba na gharama zake utalipa na kitu gani?

Ebu acheni mambo ya aibu!
Nani aliyesema gesi isiwe kwenye matumizi mwisho 2030
 
Hiyo ya pili safi sana ila hapo kwenye ya kwanza huwez panga terms kwa investors...

Labda mngeomba serikali itoe nafasi kwa wazawa wenye uwezo wapewe funds access waweze kusambaza kama hao wengine.. may be ,15%


Hiyo ya pili, hakuna haja ya Mamlaka, ni agency tu wa kupima na sio kuongeza budget kubwa kias utasmbiwa kuna changamoto ua fedha- mfano BRELA etc.

Pambaneni mkuu
Unapanga vizuri tu kumbuka natural gas refinery inatoa malighafi kama ethane ambayo inatumika na petrochemical plant kama malighafi
 
Kuanzisha mamlaka itakayohusika na upimaji wa makazi, ili kuhakikisha watu wanajenga kwa kufuata mpangilio ili iwe rahisi kuwasambazia gesi majumbani, na huduma nyingine za kijamii na itakuwa na kazi zifuatazo;-
  • Kupima nchi nzima.
  • Kuhakikisha yeyote anayejenga anafuata mipango miji.
  • Kuhakikisha kwenye miji, na vijiji kunakuwa na zoning na sio sasa unakuta gesti imejengwa katikati ya makazi ya watu.
  • Kuhakikisha kwenye makazi yote kunapita miundombinu muhimu kama fiber, maji, n.k inapitak kwa kila mwenye nyumba.
  • Kutoa elimu ya mipango miji na faida zake kwa wananchi.
  • Polisi wa mipango miji watahakikisha wanaojenga wanafuata masharti na kuwatia nguvuni wote wanaojenga kiholela a.k.a wakaidi.
  • Mapato yote ya majengo watakuwa wanakusanya wao.
 
TUNACHOPIGANIA SASA
Kwenye mradi wa gesi asilia ambao mazungumzo bado yanaendelea tunapendekeza mambo yafuatayo;-
  1. Mwekezaji asijenge tu kiwanda cha kuchakata gesi asilia (natural gas refinery), bali ajenge na kiwanda cha petrochemical kwa pamoja.
  2. Mwekezaji azalishe megawatts laki moja (100,000) za umeme kutoka kwenye gesi asili, na bidhaa zitokanazo na gesi asilia kama hydrogen. Zitasaidia kwenye ukuaji wa viwanda
You are not serious..., kwa ushauri tu ukitaka kupigania mambo fuata / ongelea issues ambazo ni realistic..., mfano waambie / waulize hao watu kwanini wanaagiza LPG kutoka nje ili waje wawape wanakijiji kupikia wakati ni gharama zaidi kuliko ambavyo leo hii hii bila mabadiliko wangetumia umeme ambao ni nafuu ?!!!

 
You are not serious..., kwa ushauri tu ukitaka kupigania mambo fuata / ongelea issues ambazo ni realistic..., mfano waambie / waulize hao watu kwanini wanaagiza LPG kutoka nje ili waje wawape wanakijiji kupikia wakati ni gharama zaidi kuliko ambavyo leo hii hii bila mabadiliko wangetumia umeme ambao ni nafuu ?!!!

Tanzania kuna gesi asilia kwanini tusitumie
 
Tanzania kuna gesi asilia kwanini tusitumie
Unatumiaje gesi asilia wakati haiwezekaniki (sio efficient) kuiweka kwenye mitungi the only viable option ni kusambaza pipes (kama wanavyosambaza maji) ila pesa hizo za kuweka infrastructure zinatoka wapi ? Busara itakuwa ni kupeleka hio gesi kufua umeme ili watu wapikie umeme

Narudia tena kwa Bongo hakuna nishati safi ambayo ni feasible kwa mazingira yetu kama umeme....
 
Unatumiaje gesi asilia wakati haiwezekaniki (sio efficient) kuiweka kwenye mitungi the only viable option ni kusambaza pipes (kama wanavyosambaza maji) ila pesa hizo za kuweka infrastructure zinatoka wapi ? Busara itakuwa ni kupeleka hio gesi kufua umeme ili watu wapikie umeme

Narudia tena kwa Bongo hakuna nishati safi ambayo ni feasible kwa mazingira yetu kama umeme....
Kuna mambo mengi huyajui
Ndo maana kuna mpango wa kutengeneza refinery ili kuweze kuzalishwa gesi ya kutumika majumbani na kwenye viwanda

Sasa hivi gesi inanunuliwa uarabuni na india kwa sababu tu hatuna refinery hapa Tanzania tukiwa nayo hatuta nunua tena gesi uarabuni na india na tutawauzia majirani zetu

Pesa ni mwekezaji anajenga kama nchi ni ngumu kuhimili mradi wa refinery ya gesi ataendesha fesha yake ikirudi anaikabidhi serikali
 
Kuna mambo mengi huyajui
Ndo maana kuna mpango wa kutengeneza refinery ili kuweze kuzalishwa gesi ya kutumika majumbani na kwenye viwanda
Mkuu LPG hii tunayotumia majumbani n.k. inapatikana katika refinery / uchimbaji wa mafuta.., sisi tuna natural gas ambayo ni more efficient in two ways; Moja kuifanya piped na kwenda moja kwa moja kwa mtumiaji kama anavyofanya Russia na kuwauzia mpaka Europe...., Au kuisafirisha kwenye Merikebu mpaka mataifa ya mbali yenye uhaba kwa kuibadilisha kuwa kimimika under cold condition yaani LNG.., ingawa pia inaweza ikawa compressed na kutumika kwenye magari CNG (sababu hapa compression inayotumika ni ndogo)....
Sasa hivi gesi inanunuliwa uarabuni na india kwa sababu tu hatuna refinery hapa Tanzania tukiwa nayo hatuta nunua tena gesi uarabuni na india na tutawauzia majirani zetu
Gesi nyingi tunayonunua ni LPG ambayo nyingi inatoka kwenye petrol refineries kwahio nchi za huko Uarabuni au nchi kama Algeria inayo ya kumwaga ndio maana wao wanaitumia hadi kwenye magari (LPG sio CNG)

Kubadilisha Natural Gas kuwa LPG is not efficient unatumia Nishati zaidi kubadilisha kitu ambacho ungeweza kukitumia as is in the first place au kuwa piped na kutumika moja kwa moja without any conversion..., hence the efficient way ni kuifanya piped (which is expensive) au kuipeleka kwenye pipe moja kufua umeme, na kuitumia kwenye magari as CNG zaidi ya hapo tuuze kama LNG mataifa yenye uhitaji
Pesa ni mwekezaji anajenga kama nchi ni ngumu kuhimili mradi wa refinery ya gesi ataendesha fesha yake ikirudi anaikabidhi serikali
refinery ya kitu gani at what cost and profit ili tumuuzie nani ? kama unataka ili mtu aweze kupikia the overall cost per unit ni kiasi gani na kwanini ufanye hivyo wakati kuna cheaper option ambayo ni umeme ? Na wakati hio gesi unaweza kuitumia as it kama CNG kwenye magari ?!!!
 
Kuna mambo mengi huyajui
Ndo maana kuna mpango wa kutengeneza refinery ili kuweze kuzalishwa gesi ya kutumika majumbani na kwenye viwanda

Sasa hivi gesi inanunuliwa uarabuni na india kwa sababu tu hatuna refinery hapa Tanzania tukiwa nayo hatuta nunua tena gesi uarabuni na india na tutawauzia majirani zetu

Pesa ni mwekezaji anajenga kama nchi ni ngumu kuhimili mradi wa refinery ya gesi ataendesha fesha yake ikirudi anaikabidhi serikali
Mkuu, kuhusu Gas Refinery, mara nyingi tunaziita Natural Gas Processing Plants. Hizi tulishazijenga; zipo huko Mtwara na Lindi, na tayari zimeshaanza kuchakata au kusafisha gesi asilia. Hii ndiyo gesi tunayoitumia kwenye magari, bajaji, na viwandani.

image_870x_67c59fd51b5b1.jpg


Pia tunaitumia kuzalishia umeme, na kuna baadhi ya nyumba ambazo tayari zimeshaanza kusambaziwa gesi kwa njia ya bomba kwa ajili ya kupikia. Gesi yetu huwezi kuitumia kupikia ikiwa kwenye mtungi; ni lazima iwe kwenye bomba kwanza.

images (45).jpeg


Tuna:

1. Songo Songo Natural Gas Processing Plant
images (41).jpeg


2. Madimba Natural Gas Processing Plant

images (42).jpeg


Mkuu, Tanzania hatuwezi kuzalisha LPG kwa sasa kwa sababu gesi yetu ina kiwango kikubwa cha Methane. Hivyo, hatuwezi kuitumia kuzalisha LPG.

Ili uzalishe LPG, unahitaji mafuta (crude oil) au gesi yenye kiwango kikubwa cha Butane na Propane. LPG ndiyo gesi pekee inayoweza kutumika majumbani kwa kupikia ikiwa kwenye mtungi, hata katika maeneo ya vijijini yaliyo mbali na visima vya gesi.

totalenergies_clean-cooking_2024_1.jpg


Unachokizungumzia hapa ni Liquefied Natural Gas Plant (LNG Plant). LNG Plant siyo refinery, bali ni kiwanda kinachobadili gesi asilia kuwa kimiminika ili isafirishwe nje ya Tanzania na kuuzwa kwenye masoko ya kimataifa.

Gesi asilia inapoozwa kwenye nyuzi joto -162 °C, inageuka kuwa kimiminika cha baridi, kisha inajazwa kwenye mitungi na kupakiwa kwenye meli tayari kwa kusafirishwa kwenda masoko ya nchi za Magharibi, ambako inaweza kununuliwa kwa wingi ili mwekezaji arudishe fedha zake za uwekezaji haraka.

images (43).jpeg


Mtanzania mwenzetu ameeleza vizuri sana kuhusu gesi:
 
Natural gas refinery products
  • Methane
  • Butane
  • Probane
  • Ethane
  • Hydrogen
Gesi asilia inayopatikana Tanzania, ina kiwango kikubwa cha methane (CH₄) asilimia 90% hadi 99%.

Ethane (C₂H₆) chini ya 5%,
Propane (C₃H₈) chini ya 1%,
Butane (C₄H₁₀), na Hydrocarbons nyingine chini ya 1%,
Kaboni dioksidi (CO₂) kwa kiwango cha 0.5% - 3%,
Nitrojeni (N₂) chini ya 1%, na
Kiasi kidogo cha hidrojeni salfidi (H₂S).

Hii inafanya gesi inayo patikana Tanzania iwe gesi inayofaa kwa matumizi ya kuzalisha umeme, kupikia kupitia mabomba, na matumizi ya viwandani.

Kwa kuwa haina kiasi cha kutosha cha propane na butane haiwezi kutumika kuzalisha LPG (Liquefied Petroleum Gas).

LPG kwa kawaida huhitaji gesi yenye propane na butane kwa kiwango kikubwa, ambacho Tanzania haina.

Vilevile, gesi yetu haiwezi kuzalisha hidrojeni (H₂) kwa urahisi kama ulivyo andika. Uzalishaji wa hidrojeni kwa kawaida unahitaji gesi zenye mchanganyiko wa hydrocarbons tofauti au maji kupitia electrolysis.

Kwa kuwa gesi yetu ina methane kwa kiwango kikubwa, njia pekee inayowezekana ni Steam Methane Reforming (SMR), ambayo inahitaji mitambo mikubwa na uwekezaji mkubwa.

Hadi sasa, Tanzania haijaweka kipaumbele kwenye uzalishaji wa hidrojeni kutoka gesi asilia.

References nilizo wahi kusoma na kuelewa kwa kina kuhusu mambo ya gesi:
 
Petrochemical products-bidhaa zinazotokana kwenye kiwanda cha kutengeneza bidhaa za plastic
  • Polyethylene
  • Polypropylene
  • Thermoplastic polyurethane
  • Ethylene
  • Propylene
  • Benzene
  • Toluene
  • Xylenes
  • Ammonia
  • Methanol
Gesi asilia ya Tanzania haiwezi kuzalisha petrochemical products zote ulizo andika hapo kwa urahisi, lakini inaweza kutumika kama malighafi kwa baadhi ya bidhaa fulani zinazotokana na gesi, hasa ammonia na methanol.

Gesi yetu ya Tanzania haiwezi kuzalisha kiurahisi polyethylene, polypropylene, thermoplastic polyurethane, ethylene, propylene, benzene, toluene, na xylenes, kwa sababu muundo wake una methane (CH₄) kwa kiwango cha juu sana (90-99%) na haina kiasi kikubwa cha ethane, propane, au butane, ambazo ni malighafi kuu katika uzalishaji wa petrochemicals.

Petrochemicals ambazo Tanzania inaweza kuzalisha kwa kutumia gesi asilia

Ammonia (NH₃)
Inaweza kuzalishwa kutoka gesi asilia kwa kutumia Haber Process, ambapo methane hutumiwa kuzalisha hidrojeni inayochanganywa na nitrojeni kutoka hewani kutengeneza ammonia. Ammonia ni malighafi muhimu katika utengenezaji wa mbolea kama urea. Lakini kabla ya kupata Amonia lazima kwanza uifanyie gesi asilia (Methane) steam reforming kwa kuipiga na mvuke wa maji kwa kutumia catalyst ili upate hydrogen na carbon monoxide. Baada ya hapo utiapiga hydrogen na nitrogen ili upate ammonia. Unaweza kuitumia Ammonia kwaajili ya kutengeneza kemikali zingine. Au unaweza kuipiga Ammonia na carbon monoxide ili upate Urea.

Methanol (CH₃OH)
Inaweza kuzalishwa kutoka methane kupitia Methanol Synthesis Process, ambapo methane inachanganywa na mvuke wa maji na oksijeni kuzalisha gesi ya mchanganyiko (syngas), ambayo hubadilishwa kuwa methanol. Methanol hutumika kama malighafi ya kutengeneza kemikali nyingine na kama nishati.

Petrochemicals ambazo gesi yetu haiwezi kuzalisha kwa urahisi

Gesi asilia ya Tanzania haiwezi kuzalisha kwa urahisi kemikali zifuatazo kwa sababu zinahitaji gesi yenye ethane, propane, au mafuta ghafi (crude oil) kama malighafi kuu:

Polyethylene (PE)
Hutokana na ethylene, ambayo mara nyingi huzalishwa kutoka kwa ethane au mafuta ghafi. Kwa kuwa gesi yetu haina ethane ya kutosha, hatuwezi kuzalisha polyethylene kwa kiwango kikubwa.

Polypropylene (PP)
Hutengenezwa kutoka kwa propylene, ambayo huzalishwa zaidi kutoka kwa mafuta ghafi au ethane/proane iliyopo kwenye gesi yenye mchanganyiko wa hydrocarbons nyingi (wet gas). Gesi yetu ni “dry gas”, hivyo haina propylene ya kutosha kwa uzalishaji wa polypropylene.

Thermoplastic polyurethane (TPU)
Inahitaji isocyanates na polyols zinazopatikana kutoka kwa petrochemical compounds zinazotokana na mafuta ghafi.

Ethylene (C₂H₄) na Propylene (C₃H₆) Zinazalishwa kwa wingi kutoka kwa ethane na propane, ambazo gesi yetu haina kwa kiwango kikubwa.

Benzene, Toluene, na Xylenes (BTX compounds)
Hizi zinapatikana zaidi kutoka mafuta ghafi (crude oil) au gesi yenye mchanganyiko wa hydrocarbons nyingi, ambayo Tanzania haina. BTX compounds hutumika kutengeneza plastiki, rangi, dawa, na vimumunyisho vya viwandani.
 
Tanzania kuna gesi asilia kwanini tusitumie
Ukiwa na tabia ya kusikiliza na kuchangajya na yako itafaa zaidi kuliko kufunga ubongo wako Kwa Yale tu unayopenda kuyasikia...Ukimsoma utagundua kuna ujumbe anakupatia ila kwakua hutaki kusikia unasikia kelele tu na siyo ujumbe muhimu anaokusaidia kuung'amua
 
Back
Top Bottom