Mkuu, kuhusu Gas Refinery, mara nyingi tunaziita Natural Gas Processing Plants. Hizi tulishazijenga; zipo huko Mtwara na Lindi, na tayari zimeshaanza kuchakata au kusafisha gesi asilia. Hii ndiyo gesi tunayoitumia kwenye magari, bajaji, na viwandani.
Pia tunaitumia kuzalishia umeme, na kuna baadhi ya nyumba ambazo tayari zimeshaanza kusambaziwa gesi kwa njia ya bomba kwa ajili ya kupikia. Gesi yetu huwezi kuitumia kupikia ikiwa kwenye mtungi; ni lazima iwe kwenye bomba kwanza.
View attachment 3261861
Tuna:
1. Songo Songo Natural Gas Processing Plant
View attachment 3261844
2. Madimba Natural Gas Processing Plant
View attachment 3261845
Mkuu, Tanzania hatuwezi kuzalisha LPG kwa sasa kwa sababu gesi yetu ina kiwango kikubwa cha Methane. Hivyo, hatuwezi kuitumia kuzalisha LPG.
Ili uzalishe LPG, unahitaji mafuta (crude oil) au gesi yenye kiwango kikubwa cha Butane na Propane. LPG ndiyo gesi pekee inayoweza kutumika majumbani kwa kupikia ikiwa kwenye mtungi, hata katika maeneo ya vijijini yaliyo mbali na visima vya gesi.
View attachment 3261862
Unachokizungumzia hapa ni Liquefied Natural Gas Plant (LNG Plant). LNG Plant siyo refinery, bali ni kiwanda kinachobadili gesi asilia kuwa kimiminika ili isafirishwe nje ya Tanzania na kuuzwa kwenye masoko ya kimataifa.
Gesi asilia inapoozwa kwenye nyuzi joto -162 °C, inageuka kuwa kimiminika cha baridi, kisha inajazwa kwenye mitungi na kupakiwa kwenye meli tayari kwa kusafirishwa kwenda masoko ya nchi za Magharibi, ambako inaweza kununuliwa kwa wingi ili mwekezaji arudishe fedha zake za uwekezaji haraka.
View attachment 3261846