TUNACHOPIGANIA SASA
Kwenye mradi wa gesi asilia ambao mazungumzo bado yanaendelea tunapendekeza mambo yafuatayo;-
- Mwekezaji asijenge tu kiwanda cha kuchakata gesi asilia (natural gas refinery), bali ajenge na kiwanda cha petrochemical kwa pamoja.
- Mwekezaji azalishe megawatts laki moja (100,000) za umeme kutoka kwenye gesi asili, na bidhaa zitokanazo na gesi asilia kama hydrogen. Zitasaidia kwenye ukuaji wa viwanda.
- Tanzania itafute mwekezaji wa crude oil refinery ambayo itakua Tanga pale ambapo bomba la mafuta la uganda litaishia kutoka uganda.
- Shule za msingi za serikali kuongeza wigo wa masomo ya kingereza (english) na kuwa matatu nayo ni kingereza, hesabu kwa kingereza na science kwa kingereza huku kiswahili kikifundishwa masomo mawili kiswahili na uraia-hii haitawaacha nyuma watoto wa kimaskin kama ilivyo sasa kwamba kuna watoto wanamaliza msingi wakiwa na msingi mzuri wa lugha ya kingereza huku wengine wakiwa na msingi mbovu wa lugha ya kingereza na mitihani iwe sawa kwa shule za msingi za serikali na binafsi ambazo sio za kimataifa.
- Kuanzisha mamlaka itakayohusika na upimaji wa makazi kama ilivyo TRA, tunapendekeza iitwe Tanzania agency of rural and urban planning (TARUP) itahakikisha watu wanajenga kwa kufuata mpangilio ili iwe rahisi kuwasambazia gesi majumbani, na huduma nyingine za kijamii na itakuwa na kazi zifuatazo;-
- Kupima nchi nzima.
- Kuhakikisha yeyote anayejenga anafuata mipango miji.
- Kuhakikisha kwenye miji, na vijiji kunakuwa na zoning na sio sasa unakuta gesti imejengwa katikati ya makazi ya watu.
- Kuhakikisha kwenye makazi yote kunapita miundombinu muhimu kama fiber, maji, n.k inapitak kwa kila mwenye nyumba.
- Kutoa elimu ya mipango miji na faida zake kwa wananchi.
- Polisi wa mipango miji watahakikisha wanaojenga wanafuata masharti na kuwatia nguvuni wote wanaojenga kiholela a.k.a wakaidi.
- Mapato yote ya majengo watakuwa wanakusanya wao.
TEFA (Tanzania Economic Freedom Advocacy) ni wakina nani????
Ni jamii yenye malengo ya kupigania Tanzania itumie rasilimali zake kiukamilifu ili kuondoa umaskini unaosumbua kaya nyingi.
MAONO (Vision)
Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.