Tanzania Economic Freedom Advocacy (TEFA)

Tanzania Economic Freedom Advocacy (TEFA)

TUNACHOPIGANIA SASA
Kwenye mradi wa gesi asilia ambao mazungumzo bado yanaendelea tunapendekeza mambo yafuatayo;-
  1. Mwekezaji asijenge tu kiwanda cha kuchakata gesi asilia (natural gas refinery), bali ajenge na kiwanda cha petrochemical kwa pamoja.
  2. Mwekezaji azalishe megawatts laki moja (100,000) za umeme kutoka kwenye gesi asili, na bidhaa zitokanazo na gesi asilia kama hydrogen. Zitasaidia kwenye ukuaji wa viwanda.
  3. Tanzania itafute mwekezaji wa crude oil refinery ambayo itakua Tanga pale ambapo bomba la mafuta la uganda litaishia kutoka uganda.
  4. Shule za msingi za serikali kuongeza wigo wa masomo ya kingereza (english) na kuwa matatu nayo ni kingereza, hesabu kwa kingereza na science kwa kingereza huku kiswahili kikifundishwa masomo mawili kiswahili na uraia-hii haitawaacha nyuma watoto wa kimaskin kama ilivyo sasa kwamba kuna watoto wanamaliza msingi wakiwa na msingi mzuri wa lugha ya kingereza huku wengine wakiwa na msingi mbovu wa lugha ya kingereza na mitihani iwe sawa kwa shule za msingi za serikali na binafsi ambazo sio za kimataifa.
  5. Kuanzisha mamlaka itakayohusika na upimaji wa makazi kama ilivyo TRA, tunapendekeza iitwe Tanzania agency of rural and urban planning (TARUP) itahakikisha watu wanajenga kwa kufuata mpangilio ili iwe rahisi kuwasambazia gesi majumbani, na huduma nyingine za kijamii na itakuwa na kazi zifuatazo;-
  • Kupima nchi nzima.
  • Kuhakikisha yeyote anayejenga anafuata mipango miji.
  • Kuhakikisha kwenye miji, na vijiji kunakuwa na zoning na sio sasa unakuta gesti imejengwa katikati ya makazi ya watu.
  • Kuhakikisha kwenye makazi yote kunapita miundombinu muhimu kama fiber, maji, n.k inapitak kwa kila mwenye nyumba.
  • Kutoa elimu ya mipango miji na faida zake kwa wananchi.
  • Polisi wa mipango miji watahakikisha wanaojenga wanafuata masharti na kuwatia nguvuni wote wanaojenga kiholela a.k.a wakaidi.
  • Mapato yote ya majengo watakuwa wanakusanya wao.
TEFA (Tanzania Economic Freedom Advocacy) ni wakina nani????
Ni jamii yenye malengo ya kupigania Tanzania itumie rasilimali zake kiukamilifu ili kuondoa umaskini unaosumbua kaya nyingi.

MAONO (Vision)
Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Safi sana mkuu, naunga mkono hoja. Ni vizuri haya mawazo yakiwafikia wenye mamlaka/watoa maamuzi.
 
Nyie mumeshajenga hicho kiwanda kuonesha mfano au mnabwabwaja ujinga wenu tuu?

View: https://x.com/MwananchiNews/status/1898077481002799233?t=XsZBteoG1S07nIRymVmsXw&s=19
 
Mwekezaji asijenge tu kiwanda cha kuchakata gesi asilia (natural gas refinery), bali ajenge na kiwanda cha petrochemical kwa pamoja.
 
Usitumie chatgpt kwenye kuwakilisha hoja tumia akili yako
NDUGU,

Hii si ChatGPT...

Ni koherensia ya Ufikirifu, Uono na Ufikirifu Mifumo.

Wewe kama mtu, una unaivu katika mafikara na udhanifu wako.

Humu wadau kadhaa wanaingilia kati mashauri na mitazamo yako kwa kheri lakini wewe kama mtu 'umejifungia kiakili' na kucheza mchezo wa kujihami--kujihami mno isivyolazima.

Si kila mtu anachangia kwenye nyuzi zako kwa kuwa wewe una nidhamu na adabu stahiki ya kimazungumzo--HAUNA!

Alhamdulillah, mashauri yako ni mbegu ya kuvutia watu makini--unawavutia wengi kwa ujuaji na unaivu wako pia.

Siyo Kesi kivile... Kwa kuwa Unasaidia wengine kufahamu mambo ilivyobora--wewe Je?

Ulijizima data kwenye hili:

Maono mazuri Dennis...

PIA,

Fanya mazoezi ya umodelishi wa viwanda vidogo vidogo halafu viwe ndani ya mtandao wa viwanda vya 'ukubwa wa kati' na 'ukubwa kabisa' halafu ushiriki mawazo.

Japo uadilifu na usanifu wako unajikita kwenye 'kutengeneza fedha na ajira kwa jamii ya Watanzania fanya mazoezi ya kuimajinisha sura ya namna ya 'uchumi wa kazi'.

Namna ya kuuona uchumi wa kazi: fikiria namna tofauti ya wanajamii kustawi pasipo dhana khasa za 'fedha ama kujenga ukwasi' bali kujishughulisha kwa ajili ya mahitaji yao ya karibu na muhimu ya kila siku--pesa inaweza kuwa ni matokeo tu; ama umiminishi wa hazina/pumzi/mtaji wa shughuli...

Mahitaji ya karibu na muhimu, ukiyaotea, yataelekea kwenye ujenzi/uboreshaji/uendelezaji wa makazi na uzashalishaji wa vyakula, bidhaa za chakula, madawa n.k -- pia mavazi.

Jenga ujuzi wa matumizi ya 'Akili Bandia' ili kuchungua mipangilio ya shughuli na mahitaji ya ujuzi ama/na kujengea ujuzi kwa wadau wa maendeleo--kwa hivyo hili linataka ujiandae kwa ujenzi wa mtandao wa mafundi wa mipango na mameneja wa miradi...

JITAHIDI KUJENGA MTANDAO WA JUHUDI NA UTENDAJI wa kutimiza maono--watu shughuli zao na maendeleo...

Unaweza, humu humu JF, kuibua mawazo, kufanya utunzi/ubunifu wa mbinu-kazi, na basi kuratibu vitendo kwa ajili ya uendelezi wa vipaji na uwezo wa kujisuka kitaasisi--kugema utayari wa wanajamii wenzako wanaoweza kuwa na dhamira na mapenzi ya kuleta mabadiliko katika jamii.

Unahitaji ujuzi na utundu wa kujipangilia na kujisukuma mbele kitaasisi; hili linakutaka uzingatie matumizi bora ya rasilimali zozote zilizopo na tena uwe na ujuzi na upeo kubaini vipaji, ujuzi na umahili wa wengine unaoweza kuwafikia/wakakufikia.

Chukulia kuwa JF inaweza kuwa ni sehemu mojawapo ya wewe kuweza kuwafikia/kuwapata wadau wa utekelezaji wa maono yaliyoko kwako. Livalie njuga hili suala hili, kinamna hii, ili upate wepesi kuibadilisha sura na mwenendo wa jamii yetu kwa 'Hamadi kibindoni...'

Hmmm​

Halafu tena:

UMEKAZA NIA SANA KWENYE 'UZALISHAJI" na UZALISHAJI MALI' KULIKO WATU WENYEWE

Haudhani hivi?

Mdogo mdogo, fanya mazoezi ya 'Kuwaona watu'--watu na mawezekano; haya ya viwanda unaweza 'kuyaweka kiporo'--ama kuyarudia upya unapokuwa na mwangaza bora... Ama kuyasukuma kama 'mpango wa kando'.

Chochote ukifikiriacho, weka watu kama ndiyo 'Taa na Dira' ya maisha na kujichagulia...

Ulimwengu wa leo hili, hutafundishwa hili 'Shuleni' ama 'Chuoni'--huko sana sana mtu/mwanajamm anaweza kugeuzwa 'mtumika' wa 'mifumo ya mali' na 'uzalishaji mali'....

Hili lina mazuri na mabaya yake wakati mmoja hata mwingine--japo kwa ujumla, SI JAMBO BORA kwa maana hili ni shauri rahisi lenye nasibu ya kutweza 'heshima ya utu wa mtu/mwanajamii'...

Mambo ya 'Mnyonge hana Haki' ni tunda bovu la mfumo wa biashara wa jamii; kuna namna yake ya ubayana wenye kuleta hata muktadha akilifu wa kana kwamba: hata wewe unaweza kuwa 'umeathirika na unyonge' -- ndiyo basi maana ya mapelekeo ya dhana rahisi ya kuibuka na madhumuni ya 'made in Tanzania'... hili lawa ni 'shauri la faraja'/kuwazia Tanzania Imara kwa msingi wa viwanda kama vya 'mabeberu'...

Hakuna ubaya kuhusu kudhamiria 'Ubeberu'; sema huu huja kwa utundu na ujuzi wa kuruhusu mifumo ya 'wenyekuwa nacho' na 'wasio nacho' wakati wote... Ni vema kuwa na akili kama beberu, lakini jiongeze ili kujiangazia mawezekano ya Ujamaa.

Ulimwengu ulipo sasa, Ujamaa unawezakana--unahitaji tu 'wanajamii na taasisi zao' kujiongeza--kujua ilivyobora.

Inawezekana kuthubutu kufikiri tofauti...

Kwa hivyo unaweza kuimarisha upeo na uelewa wako juu ya wanajamii na jamii... Maendeleo ni watu halafu vitu; mtaji mkubwa wa jamii ni 'akili zao' kwa hivyo kadiri unanyoshikiri yale yaliyo ndani ya wanajamii wenyewe 'kujiongeza' basi unakuwa umeonesha njia khasa...

Hmmm
NASHAURI, usiogope kupewa changamoto ya kile unachodhani 'UMEMALIZA KIMAWAZO NA UJUAJI' na kumbe, kwa wakati huu, unako kule kujua mambo kwa sehemu tu;

Na tena, ujumla wa shauri lako ni Utoto/Ujuvinali wa Kujiwazia Ubab' Kubwa kwa kule tu kujidhania eti Umeshika 'Bunduki fulani Kubwa';

Unaweza kujisahihisha, kwa kuwa bado una nafasi ya kujipanga na kujipangua kimawazo na utashi ili uwe ni mtu mwenye kujua ilivyobora.

Hakuna ubaya kuachana ni mienendo ya kijuvinali...

Je, Unataka 'Umimi katika Ujuaji-Juvinali' ama nidhamu bora ya kujiweka kiakili na adabu kwa ajili ya nasibu ya 'Tujuzane hata ikibidi kwa Kuleeana na Shauri Bora'?

... Amua mwenyewe.

Hmmm
 
NDUGU,

Hii si ChatGPT...

Ni koherensia ya Ufikirifu, Uono na Ufikirifu Mifumo.

Wewe kama mtu, una unaivu katika mafikara na udhanifu wako.

Humu wadau kadhaa wanaingilia kati mashauri na mitazamo yako kwe kheri lakini wewe kama mtu 'umejifungia kiakili' na kucheza mchezo wa kujihami--kujihami mno isivyolazima.

Si kila mtu anachangia kwenye nyuzi zako kwa kuwa wewe una nidhamu na adabu stahiki ya kimazungumzo--HAUNA!

Alhamdullilah, mashauri yako ni mbegu ya kuvutia watu makini--unawavutia wengi kwa ujuaji na unaivu wako pia.

Siyo Kesi kivile... Kwa kuwa Unasaidia wengine kufahamu mambo ilivyobora--wewe Je?

Ulijizima data kwenye hili:

Halafu tena:

NASHAURI, usiogope kupewa changamoto ya kile unachodhani 'UMEMALIZA KIMAWAZO NA UJUAJI' na kumbe, kwa wakati huu, unako kule kujua mambo kwa sehemu tu;

Na tena, ujumla wa shauri lako ni Utoto/Ujuvinali wa Kujiwazia Ubab' Kubwa kwa kule tu kujidhania eti Umeshika 'Bunduki fulani Kubwa';

Unaweza kujisahihisha, kwa kuwa bado una nafasi ya kujipanga na kujipangua kimawazo na utashi ili uwe ni mtu mwenye kujua ilivyobora.

Hakuna ubaya kuachana ni mienendo ya kijuvinali...

Je, Unataka 'Umimi katika Ujuaji-Juvinali' ama nidhamu bora ya kujiweka kiakili na dabu kwa ajili ya nasibu ya 'Tujuzane hata ikibidi kwa Kuleeana na Shauri Bora'?

... Amua mwenyewe.

Hmmm
We jamaa unaonekana ni mjuvi wa kiswahili
 
NDUGU,

Hii si ChatGPT...

Ni koherensia ya Ufikirifu, Uono na Ufikirifu Mifumo.

Wewe kama mtu, una unaivu katika mafikara na udhanifu wako.

Humu wadau kadhaa wanaingilia kati mashauri na mitazamo yako kwa kheri lakini wewe kama mtu 'umejifungia kiakili' na kucheza mchezo wa kujihami--kujihami mno isivyolazima.

Si kila mtu anachangia kwenye nyuzi zako kwa kuwa wewe una nidhamu na adabu stahiki ya kimazungumzo--HAUNA!

Alhamdulillah, mashauri yako ni mbegu ya kuvutia watu makini--unawavutia wengi kwa ujuaji na unaivu wako pia.

Siyo Kesi kivile... Kwa kuwa Unasaidia wengine kufahamu mambo ilivyobora--wewe Je?

Ulijizima data kwenye hili:

Halafu tena:

NASHAURI, usiogope kupewa changamoto ya kile unachodhani 'UMEMALIZA KIMAWAZO NA UJUAJI' na kumbe, kwa wakati huu, unako kule kujua mambo kwa sehemu tu;

Na tena, ujumla wa shauri lako ni Utoto/Ujuvinali wa Kujiwazia Ubab' Kubwa kwa kule tu kujidhania eti Umeshika 'Bunduki fulani Kubwa';

Unaweza kujisahihisha, kwa kuwa bado una nafasi ya kujipanga na kujipangua kimawazo na utashi ili uwe ni mtu mwenye kujua ilivyobora.

Hakuna ubaya kuachana ni mienendo ya kijuvinali...

Je, Unataka 'Umimi katika Ujuaji-Juvinali' ama nidhamu bora ya kujiweka kiakili na adabu kwa ajili ya nasibu ya 'Tujuzane hata ikibidi kwa Kuleeana na Shauri Bora'?

... Amua mwenyewe.

Hmmm
Sihitaji shauri wako ndugu kwa sababu haukunituma kufanya hichi nachofanya
 
Kuanzia mwaka huu 2025 mwezi march hatutakubali kuendelea kuburuzwa maji shida, umeme haueleweki, huduma za kijamii mbovu safari hii hatukubali tena tutagawana fito.
 
Serikali itafute wawekezaji wazalishe zaidi ya megawatts laki moja (100,000+) za umeme kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vilivyopo nchini.
 
Shule za msingi za serikali kuongeza wigo wa masomo ya kingereza (english) na kuwa matatu nayo ni kingereza, hesabu kwa kingereza na science kwa kingereza huku kiswahili kikifundishwa masomo mawili kiswahili na uraia-hii haitawaacha nyuma watoto wa kimaskin kama ilivyo sasa kwamba kuna watoto wanamaliza msingi wakiwa na msingi mzuri wa lugha ya kingereza huku wengine wakiwa na msingi mbovu wa lugha ya kingereza na mitihani iwe sawa kwa shule za msingi za serikali na binafsi ambazo sio za kimataifa.
 
KILA NINAPOWAZA KUTOKA JAMII FORUM, HUWA MUNGU ANANIKUTANISHA NA MADINI KAMA HAYO...YAANI HAPA HAMNA MAWAZO YA CHAWAA.. SAFII SANA, TENA SANA..
taasisi ya urais iwe inabeba mawazo kama hayo, iachane kutafuta real ID, BALI IBEBE MAWAZO TU YANATOSHA.
 
Serikali kutonunua magari ya kifahari kwa wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi na budget hio kuielekeza sehemu zenye uhitaji.
 
Unit moja ya maji kuuzwa sh 400 mpaka 500
kupiga marufuku wale wanaouza maji na magari mitaani
 
Huduma za dialysis ziwe bure asilimia 100 kwa kila wilaya nchi nzima kwenye hospital za serikali
 
VETA itakuwa na umuhimu kama tutakua na viwanda vingi tofauti na hapo ni uongo sababu hata sahivi tuna watu wengi wamesoma VETA na hawana kazi viongozi waache kutumia shortcut na kauli nyepesi nyepesi ambazo sio na msaada
 
Back
Top Bottom