Nimekuelewa sana ila nafikiri unachanganya mambo, kwa nchi ambazo ni developed kama Japan, EU, USA & Co. ni ngumu sana hata kupata hata tu 2% economic growth, lkn kwa nchi masikini ambayo ndiyo kwanza inaendelea kukuwa kwa 5% hakutokani na kukomaa kwa Uchumi bali ni kwa nchi husika kushindwa kukua zaidi labda kwa sababu ya sera, skills, upatikanaji wa nishati ya kutosha, corruption, miundombinu n.k.
Hivyo kwa kifupi Kenya au hata TZ tuna nafasi ya kukuwa hata kwa 20% kama tukijipanga, lkn nchi kama Japan akipata 5% Dunia nzima itashtuka, kwani ni ngumu sana kwa developed economy kukuwa kwa kasi kwa sababu karibia kila kitu kipo, sasa growth itatokea wapi?
Lkn kwa nchi kama Kenya/TZ kuna mengi sana bado hayajafanywa hivyo kukuwa kwa 5% ni ndogo sana na ndo maana unaona wengi hawaoni tofauti kwa sababu uchumi haukuwi kwa kiasi cha kuweza kuwafikia, ...