Tanzania Government Bans Sending of Messages With The Word 'Tundu Lissu' in the Text

Tanzania Government Bans Sending of Messages With The Word 'Tundu Lissu' in the Text

Alafu tunashangaa watu wanakosa Uzalendo na nchi yao, kumbe wachache ndio wanatengeneza watu wa namna hio, huwezi kuonea baadhi ya watu alafu ukategemea kusiwe na reaction, Tanzania ya wachache haiwezi kuwa Tanzania ya WENGI.
Punguza jazba, mbona TCRA wameshatolea ufafanuzi?, tatizo lenu mnaogopa hadi vivuli vyenu

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Haya makampuni yote mnaoyaona na Mali zote zinzoonekana sio za watu wengine zaidi ya Makada wa CCM walioifilisi nchi kwa miaka 60 .

Kidogo JPM alitaka kujaribu kupambana na Majizi lakini majizi hayo hayo yakatumia mbinu za kuwatumia akina Musiba kusema kuwa adui wa nchi hii ni Wapinzani na mabeberu kutoka nje huki akisahau kuwa Kuna mabeberu wa ndani ambao ni wengi na wamejaa kila mahali ndio wanaohonga wasimamizi wa uchaguzi ili kuvuruga uchaguzi na kuwahonga baadhi ya watu kwenye vyombo vya dola.
 
Punguza jazba, mbona TCRA wameshatolea ufafanuzi?, tatizo lenu mnaogopa hadi vivuli vyenu

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
kutolewa ufafanuzi ndio kunaondoa tatizo lililotendeka? Kwahio kila jambo bovu likifanyika likitolewa ufafanuzi basi linaondoa ubovu uliofanyika?

By the way ufafanuzi wa temporary suspension of bulk sms unaendana vipi na kutuma neno Tundu Lissu? au Tundu Lissu ni Bulk SMS hata ukituma sms moja na wengine hawana hio Bulkiness?
 
kutolewa ufafanuzi ndio kunaondoa tatizo lililotendeka? Kwahio kila jambo bovu likifanyika likitolewa ufafanuzi basi linaondoa ubovu uliofanyika ?

By the way ufafanuzi wa temporary suspension of bulk sms unaendana vipi na kutuma neno Tundu Lissu ?, au Tundu Lissu ni Bulk SMS hata ukituma sms moja na wengine hawana hio Bulkiness?
Kuna mdau ameonyesha hapo kwamba hata akituma neno Magufuli pia inagoma. Mimi nikutuma sasa hivi majina yote mawili inakubali. Kwanini mpo very suspicious kiasi hicho?, kila kitu mnahisi kuonewa,, coal down, hii ni technolojia mpya huku Africa, bado kuna changamoto zake.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Sasa atasemaje serikali ya Tanzania? Kwani haya makampuni yanatoa huduma kwa maelekezo ya serikali?
Usipoelewa utakuwa na haja kichwani.
IMG_20201024_095457.jpg
 
Alafu tunashangaa watu wanakosa Uzalendo na nchi yao..., kumbe wachache ndio wanatengeneza watu wa namna hio..., huwezi kuonea baadhi ya watu alafu ukategemea kusiwe na reaction...., Tanzania ya wachache haiwezi kuwa Tanzania ya WENGI.......
Acha malalamiko yasiyo na maana umejaribu kutuma jina la Magufuli likaenda? Wakati mwingine tumieni akili zenu mlizopewa na Mungu vizuri kuliko kushikiwa akili na wanaharakati.
 
Sasa atasemaje serikali ya Tanzania? Kwani haya makampuni yanatoa huduma kwa maelekezo ya serikali?
Ndio ni kwa maelekezo ya serikali ya Tanzania...Serikali ina regulator wa mawasiliano...
Yaani wewe leo utapigwa spana kwenye nyuzi zako zote utakazofungua kwa sababu hauna akili ya kufikiri,

Nimejaribu muda huu kuandika JOHN POMBE MAGUFULI nikatuma ikagoma kwenda,

Nikaandika pia TUNDU LISSU nikatuma ikagoma kwenda,

Kama nadanganya atokee Mtanzania yoyote ajaribu kama mimi,

Ukiambiwa wacha kufanya page za wanaharakati uchwara source za nyuzi zako husikii...ona sasa unapigwa spana bure. View attachment 1610301
Huna salio kwenye simu....
 
Sasa atasemaje serikali ya Tanzania? Kwani haya makampuni yanatoa huduma kwa maelekezo ya serikali?
Huko duniani gani jamaa,wakati Jiwe anasema alidukua mawasiliano ya Lisu,na watu wa Barrick,unafikiri aliwezaje,kwa taarifa yako,TCRA,Wana mitambo yao imefungwa kwenye kila network,wanaona kila sms inayotumwa.
 
Kuna mdau ameonyesha hapo kwamba hata akituma neno Magufuli pia inagoma. Mimi nikutuma sasa hivi majina yote mawili inakubali. Kwanini mpo very suspicious kiasi hicho?, kila kitu mnahisi kuonewa,, coal down, hii ni technolojia mpya huku Africa, bado kuna changamoto zake.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
Acha malalamiko yasiyo na maana umejaribu kutuma jina la Magufuli likaenda? Wakati mwingine tumieni akili zenu mlizopewa na Mungu vizuri kuliko kushikiwa akili na wanaharakati.

Teknologia ya Bulk SMS ni mpya ?, kwanini waizime sasa hivi wakati watu ndio wanahitaji?, kwanini wazingeizima kabla ?, huenda Magufuli hatumii hii njia ndio maana hajalalamika (kwa media zote alizoziteka sidhani kama anahitaji mitandao) aliye na kisima hawezi kulalamika mvua isiponyesha sababu hatakosa maji ya kunywa....

Sasa hao ambao mitandao ndio njia pekee ya kuwasiliana huoni hili jambo linawabana wao kuliko wengine....
 
Sasa atasemaje serikali ya Tanzania? Kwani haya makampuni yanatoa huduma kwa maelekezo ya serikali?

Ndio umemaliza kufikiri utopolo? TCRA ni mali ya nani? Unajua kazi ya TCRA?
 
Back
Top Bottom