Tanzania Haijashinda Medali yoyote Olympics kwa takriban miaka 40. Shida iko wapi?

Tanzania Haijashinda Medali yoyote Olympics kwa takriban miaka 40. Shida iko wapi?

Tatizo kubwa ni viongozi wa riadha hasa hivi vizee vya TOC, Filbert Bayi ( huyu hataki mtu avunje rekodi yake ya uwanjani) , kuna kizee kingine kinaitwa Henry Tandau ( hiki kina kiburi sana na kujifanya kinawajua viongozi wote) na Ghulam Rashid wa Zabzibar.

Hivi vizee ni tatizo kubwa kwenye riadha tanzania
Kwanini hao wazee wasiondolewe hapo hata kwa kutumia nguvu maana hakuna chochote walichokifanya cha maana?.... hii nchi bhana.

Yaani mtu anatumia wadhifa alionao kufanya jitihada za kuhakikisha kwamba hakuna mtu aneyevunja record yake? Wakati malegends wa maana kama wakina Usein Bolt huko kwao wanafungua marathon clinics hili wapate wakina Usein bolts wengine hapo baadae...!!?

Kweli mbongo ni mtu mwenye roho ya kishetani sana na ndio maana hata taifa hili limelaaniwa kwenye michezo
 
Unashindana na watu wako camp for three years kwa mashindano haya, wakati nyie mnakusanyana kwenda kushiriki halafu utegeme miujiza. Pathetic
 
Shida ni CCM. Chanzo Cha Matatizo yote nchini
Hakika umeandika ukweli.
Nani alifuta UMITASHUMTA na UMISSETA!!??
Viwanja vya wazi vilivyokuwa vikitumiwa na watoto mitaani kwa ajili ya kucheza vimeuzwa na nani!!??
Masomo mpaka saa 11 jioni hivyo kusababisha watoto kukosa muda wa kupumzika ni sera ya nani!!??
Hivi walimu wa michezo mashuleni bado wanaendelea kuzalishwa kule Malya na UDSM!!!??
Wazazi na walezi kuwapa muda mrefu watoto wa kutumia teknolojia.
 
Kwa nchi zilizo serious alipaswa afukuzuzwe. Unakosaje hata medali moja.
Tumeshindwa na nchi ambazo hazina hata watu... Singapore...
Cyprus...kuna vinchi vidogoo ila vimepta medali...Sisi tuna ujinga mwingi Sana...

Mtapata medali na waziri ndo huyu Ngumbaro?
 
Ikiwa Mashindano ya Olympics yamemalizika leo Agosti 11, 2024 Wawakilishi wa Tanzania katika Mashindano ya Olympics nchini Ufaransa watarejea nchini bila ushindi wa Medali yoyote

Tanzania ilipeleka timu ya Wanariadha 7 kwenye Mashindano hayo

Aidha mara ya mwisho Tanzania kupta Medali ya fedha kupitia mwanariadha Filbert Bayi na Suleimani Nyambui mwaka 1980.

Soma Pia: Watanzania 7 kupeperusha Bendera ya Tanzania katika Olimpiki 2024 huko Paris

Mdau unadhani ni hatua gani zichukuliwe ili Tanzania iweze kuchukua medali ikishiri tena Mashindano haya 2028?
Kama tumeshindwa kuongoza kwenye mauzo ya madini ya Tanzanite ambayo hakuna mahali pengine duniani hupatikana, unadhani tunaweza kufanya vizuri kwa hayo mengine?

Siyo Olimpiki tu, ni wapi kwingine tulifanya vizuri au tunafanya vizuri? Tusiwabebeshe zigo watu wa Olimpiki wakati kwingine kote mambo hayaendi.

Ova
 
Back
Top Bottom