Tanzania haikuwa colony bali protectorate chini ya muingereza. Nini tofauti ya colony na protectorate?

Tanzania haikuwa colony bali protectorate chini ya muingereza. Nini tofauti ya colony na protectorate?

Ni makoloni yote yaliyokua ya ujerumani kabla vita vya kwanza ... yaliyochukuliwa chini ya uangalizi wa nchi zilizoshinda vita
So kwenye haki na utawala hayana tofauti na makoloni asilia?
 
Kenya wameendelea nini!?..ulishafika?!..watu hawawezi kujilisha wenyewe unasema wameendelea!!..barabara mbovu,kula shida
Kenya wanaioverrate sana kuliko uhalisia wenyewe .
 
Na UGANDA 🇺🇬, protectorate ilikua ni kingdom moja tu ya Buganda nyingine zote hazikua na hiyo favour
Uko sahihi kabisa. Mkataba wa Buganda wa 1900 ulikuwa baina ya Waganda(Abaganda)waliowakilishwa na Kabaka Daudi Chwaa na Waingereza waliowakilishwa na Sir Harry Johnston gavana wa kwanza wa Kiingereza Uganda. Kwahiyo hizo falme nyingine hazikuwemo kwenye mkataba huo. Hilo limeendelea kuitesa Uganda mpaka leo Waganda halisi hawa wa Kabaka ambalo huwadharau sana hizi jamii nyingine. Na hata wakati wa ukoloni wao walipendelewa kuliko jamii nyingine. Leo Museveni ambaye ni Mnyankore toka Mbarara nguvu aliyobaki nayo ni vyombo vya ulinzi lakini waganda wa Buganda wana kila kitu.
 
Baada ya vita ya kwanza ya dunia, league of nations wakaiweka Tanzania kuwa protectorate chini ya muingereza. Sasa kuwa namna hii na kuwa koloni kama zilivyokuwa Kenya na Uganda kuna tofauti gani?

Nini faida tulizopata na hasara tulizopata ukilinganisha na makoloni kama Uganda na Kenya?
Iwe tulikuwa nani au nini doesn't make sense now...
Kinachoonekana ni kuwa kupewa uhuru kwa njia tuliyopewa kumetudumaza sana akili!!
Pili tumezidi kuwa wakoloni wakandamiza wa watu wa Zanzibar!!
 
Tulikuwa tunaangaliwa mpàka tuwe nanuwezo wa kujitawala. Huwa nashangaa watu wanaposema Nyerere "alipigania" Uhuru. Uhuru tungelipata maana tulikuwa tunalelewa, tukue, tuwe na akili za kutosha kujitawala, waingereza waondoke watukabidhi nchi. Au nakosea?
 
Back
Top Bottom