Tanzania haimo kwenye nchi kumi zenye miundombinu bora Afrika!

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
4,291
Reaction score
5,786

Miaka 60 baada ya uhuru, bado hatuna miundombinu iliyo bora kuifanya nchi angalau kutajwa tu kati ya nchi kadhaa zinazofanya vizuri kwenye barabara.

Pamoja na kuwa na taasisi kama Tanroad na sasa Tarura bado hatujengi barabara zinazoweza kutolewa mifano.

Kwenye maliasili ghafi kama dhahabu, almasi, tanzanite pia hakuna popote tunapotajwa zaidi ya tambo kutoka kwenye vinywa vyetu na wanasiasa wetu.

Hivi Tanzania kama nchi tunaweza nini?.
 
He!
Mbona wafuasi wa Jiwe wanasema Marehemu wao alijenga barabara za lami nchi nzima!?
 
Senegal inawezaje kuwa na miundombinu mizuri kuliko Tanzania? Hii list ni fake
 
Tanzania ipo top 10, taarifa zako za zamani sana.
Hiyo ni ranking ya 2022, hata Kama ilikuwepo mwaka jana, barabara zetu zilithaminiwa kwa ubora upi? Ranking ya mwaka huu 2023 hata ikiwemo tuna barabara zipi kwa umbali gani zenye ubora?
 
Miaka 60 baada ya uhuru, bado hatuna miundombinu iliyo bora kuifanya nchi angalau kutajwa tu kati ya nchi kadhaa zinazofanya vizuri kwenye barabara.

Pamoja na kuwa na taasisi kama Tanroad na sasa Tarura bado hatujengi barabara zinazoweza kutolewa mifano.

Kwenye maliasili ghafi kama dhahabu, almasi, tanzanite pia hakuna popote tunapotajwa zaidi ya tambo kutoka kwenye vinywa vyetu na wanasiasa wetu.

Hivi Tanzania kama nchi tunaweza nini?.

Hapo no ukweli kama tunajenga Kwa kuripua harafu bei kubwa na tunajenga kidogo ni wazi hatumo..

Mfano Hilo li Msalaba hapo Ubungo unaita interchange ni matusi ,mchoro ulikuwa mzuri Engineer Mwendazake akaharibu Kila kitu.
 
Senegal inawezaje kuwa na miundombinu mizuri kuliko Tanzania? Hii list ni fake
Sasa unashangaa nini? Hata kama hujawahi fika jaribu ku google tuu..

Senegal Ina Hadi toll roads expressway za 8 lanes ambazo nyie mnaita Barabara za tozo hamtaki Serikali ijenge 😄😄

Senegal Ina viwanja vikali ,Tanzania Ina nini?
 
Kama TanRoads wamepiga matrilioni ya fedha za miundombinu wewe unafikiri tutaingiaje kwenye top ten.
 
Tatizo miradi mingi imekufa kipindi hiki.kama miradi mingi iliyoanzishwa isingekufa kwenye awamu hii naamini tungeingia kwenya 10 bora
 
Hapo no ukweli kama tunajenga Kwa kuripua harafu bei kubwa na tunajenga kidogo ni wazi hatumo..

Mfano Hilo li Msalaba hapo Ubungo unaita interchange ni matusi ,mchoro ulikuwa mzuri Engineer Mwendazake akaharibu Kila kitu.
Yani ubungo interchange unaita msalaba? Nimecheka Sana.

Weka hapa ramani ya before and after Magufuli kuharibu structure Kama anavyodai.
 
Mkuu Tanzania ingekuwepo hata namba kumi ungesikia nderemo zake. Hakuna "Complex" ya aina yote ile angalia upya video hapo juu ni ya 2023, hatuna barabara kuu yenye kilometa hata 40 iliyojengwa kwa viwango vinavyotuwezesha kuingia kwenye "Ranking"
Tatizo lenu mna inferiority complex na mnaingiza siasa katika kila kitu. Tanzania imepiga hatua kubwa sana katika ujenzi wa barabara na katika nchi za Afrika, ipo top 10 kwa kushika namba 9. Huo ndiyo ukweli.
 
Tunajenga barabara ndio, kwa thamani ipi kulingana na ubora? Labda... Tuendelee kusubiri hiyo "Highway ya kulipia Hadi Morogoro... Lakini huyo anayetujengea atajenga kwenye viwango au kulingana maono yetu kuwa na barabara ili mradi inapitika mwaka mzima?.
 
Kama TanRoads wamepiga matrilioni ya fedha za miundombinu wewe unafikiri tutaingiaje kwenye top ten.
Mkuu hakuna kitu kinanikera kama hii tabia ya udokozi wa pesa ya umma huku mwisho wa mwaka wanadai watu walipe kodi.
 
Kwasababu hawachukuliwi hatua zozote na kuna wengine wana akaunti China wamezificha fedha za kupora.
 
Hapo no ukweli kama tunajenga Kwa kuripua harafu bei kubwa na tunajenga kidogo ni wazi hatumo..

Mfano Hilo li Msalaba hapo Ubungo unaita interchange ni matusi ,mchoro ulikuwa mzuri Engineer Mwendazake akaharibu Kila kitu.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nchi inahitaji la kufumuliwa na kusukwa upya, vinginevyo maendeleo kama nchi tutayaona kwa jirani kupitia runinga.
 
Tz ni nchi ya 31 kwa ukubwa Duniani. Huwezi kuijenga nchi yote kirahisi ivyo...
 
Back
Top Bottom