Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Punguza kuwa nabii wa majanga (prophet of doom). SSH ameamua kuongeza mishahara ni suala zuri kuliko kuumiza mamilioni ya watu wakaishi kwa vinyongo wakati maisha haya ni mafupi.

Unazilipiaje? Wewe na wenzako kwenye serikali hii? Mtuambie. Ni rahisi sana kumuita mtu majina ukikosa majibu.

Hakuna binadamu , Mtanzania ambaye hapendi Watanzania wote wawe na maisha mazuri.

Mapato yanapungua, matumizi yanaongezeka.

Tuonyeshe hizi pesa zitatoka wapi, mikopo? Kodi zingine zaidi?
 
Punguza kuwa nabii wa majanga (prophet of doom). SSH ameamua kuongeza mishahara ni suala zuri kuliko kuumiza mamilioni ya watu wakaishi kwa vinyongo wakati maisha haya ni mafupi.

Kwanini mmetoa ruzuku kwa wakulima ambao ndio wengi 70% ya Watanzania.

Mshaurini vizuri SSH kwenye vikao vyenu. Kukuza uchumi kwa kasi punguzeni kodi, ukiritimba, milolongo, biashara zitashamiri.
 
Wewe ni mchawi!
 
Kaka minimum wage ndio imepandishwa kwa hiyo asilimia 23.3. High earners watakuwa na asilimia ndogo sana. Kupandishwa mishahara ni haki ya mtumishi yeyote.
 
We hamnazo kweli pia una chuki binafsi n watumishi, soma vzuri ile barua, wamesema mishahara imeongezwa kwa watumishi wa umma kwa 23.3% ikiwemo kima cha chini.Hapo anamaanisha ombi la tucta la milioni moja na elfu kumi limekataliwa kwahiyo Kila mtumishi basic yake atazidisha kwa 23.3 na kugawa kwa 100%.Pongezi kwa Rais wetu na sio yule Babu yenu.
 
Kwanini mmetoa ruzuku kwa wakulima ambao ndio wengi 70% ya Watanzania.

Mshaurini vizuri SSH kwenye vikao vyenu. Kukuza uchumi kwa kasi punguzeni kodi, ukiritimba, milolongo, biashara zitashamiri.
Mkuu yule aliyepita ambaye nafikiri ndio mnamuona alikuwa sahihi alishawahi kuwajali hao wakulima unakwasema hapa?

Lakini pia, unataka kuniambia kwa njia yoyote ile serikali inakosa/itakosa nyongeza ya Billion 130 kwa mwezi ya hii nyongeza ya mshahara? Kama bwana yule aliweza kilipa trillions ndani ya mwaka kwa ajili ya ndege tena Cash kwanini nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi inakuwa nongwa?

Au hii ni vita tu kwakuwa yule hakuongeza na mnaona kama legacy yake inachafuliwa??
 
Zinalipwa kwa kuongeza ufanisi zaidi. Mshahara mkubwa ni motisha ya kazi, unapoongezwa muajiri anategemea ongezeko la tija kutoka kwa mwajiriwa.

Tunalalamika mno watanzania. JPM hakuongeza mshahara miaka yote sita na haiikumnyima usingizi hata kidogo. SSH ameamua kuongeza mshahara mnakuja na malalamiko mengine!.

Sio ajabu tutakwenda ndani ya makaburi tukiwa na malalamiko mengi tu.
 

Vita gani tena. Vita iko Ukraine. Hapa tunachambua vitu kama watu huru.

Kuhusu wakulima hata JPM alikosea sana infact serikali zote toka awamu ya pili hazijawahi kumsaidia mkulima kwa dhati.

Nilimkosoa sana JPM kuhusu kilimo, kodi, mazingira ya biashara. Alikuwa vizuri sana kwenye miundombinu kama maji, umeme, barabara. Nidhamu serikalini, kuthibiti mfumuko wa bei, kwa hayo tulimpongeza.

130bn kwa mwezi kwa mwaka ni kiasi gani? 1.5Trillioni permanent imeongezwa ndani ya matumizi ya serikali. Kwanini usingeongeza kidogo kidogo, manageable sums of money say 5%, kila mwaka unaongeza uchumi ukikuwa unaongeza zaidi.

Kulikuwa na ulazima gani kuondoa ruzuku kwenye pembejeo, kuweka tozo mbalimbali?

Kwanini bwawa la umeme kasi imepungua ya kulimaliza,? Ingeleta tija, faida kubwa sana kwa taifa.

Faida hizo ni kama watu kujiajiri, viwanda kujengwa,unafuu mkubwa wa maisha kwa Watanzania wengi. SGR, maji,kodi,barabara, mazingira mazuri ya biashara elimu hivi vitu ndio vinaifungua nchi.
 
Kwanini mmetoa ruzuku kwa wakulima ambao ndio wengi 70% ya Watanzania.

Mshaurini vizuri SSH kwenye vikao vyenu. Kukuza uchumi kwa kasi punguzeni kodi, ukiritimba, milolongo, biashara zitashamiri.
Tukipunguza kodi hayo madaraja na shule hazitajengwa na mtakuja humu mkilalamika kwanini hazijengwi. Ruzuku ni suala la muda, linafanyiwa kazi.
 
Nibora hasinge ongeza mishaara mfumuko wabei utakuwa mkubwa Sana vitu vita panda bei mfano Kodi ya Nyumba chumba cha 50,000 kitapanda mpaka 60,000.
Wewe ni famba mno. Yaani wafanyakazi wa umma wasiongezwe. Watu wengine sijui mpo na akili na roho za namna gani. Haaaaaaaaaa....... wewe ni.mchawi haki ya Mungu
 
Msikilize na umtizame mmoja wa washiriki wa mchakato wa upandishwaji mishahara. Anaseme si kwa kila daraja watapata 23% japo mama samia amejitahidi sana kuanxia mwaka jana mambo ambayo ameyafanya kwenye vipato vya watumishi si madogo
Miaka yote benchmark ya mshahara ni kima cha chini. Then inakwenda kwa discending order hadi mshahara wa juu
 

Unakosea kusema ni malalamiko. Ni vitu muhimu vinajadiliwa. Wananchi siku zote watajadili jinsi serikali yao inavyotumia pesa zao.

Utahoji hata wewe kama mke wako, mfanyakazi wako, mtoto wako anavyotumia pesa zako kama unaona vitu haviko sawa.

Tumewapa dhamana ya muda kutuangalia, kutujengea mazingira sahihi na sisi walalahoi tuinuke kusaidia familia zetu. Kama wewe na wenzako mnavyolamba asali. Mnasahau hata umeme, maji kwa kila familia ni haki yao, kama yako.

Tunawakumbusha
 
Tukipunguza kodi hayo madaraja na shule hazitajengwa na mtakuja humu mkilalamika kwanini hazijengwi. Ruzuku ni suala la muda, linafanyiwa kazi.
Steph Curry. Wakulima na watoto wao wanakufa sasa hivi hawawezi kumudu bei za pembejeo, kuzalisha mazao. kwanini uzitoe in the first place?

Kwanini msipunguze wizi huu CAG aliousema, kupunguza ufisadi, matumizi ya hovyo?

Mkifanya hivyo mtapata pesa nyingi kuweza kuwalipa wafanyakazi wote, kuondoa kodi zinazowaumizi watu wengi wa chini.

Mtapata pesa kulipia afya, elimu, miundombinu.

Kusema ni suala muda ni maneno ya kisiasa. Muda inaweza kuwa miaka 30. JPM alizipata hizi pesa kwa kuthibiti wahuni, mafisadi, rushwa ndani ya miezi michache. Alipambana nao. Fanyeni hivyo.
 
Mshahara ndio umeshaongezwa kwa wafanyakazi wa kima cha chini kama ilivyokuwa ikiombwa na wafanyakazi kwa serikali kwa kipindi cha miaka sita, haya mengine ni maongezi ya kufurahisha baraza.
 
Chochote kitakachofanywa na serikali wa kulalamika mtakuwepo na wa kupongezwa na kufurahia maamuzi watakuwepo pia. Hakuna wa kumfurahisha kila mtu.
 
Unaongelea bei ya mafuta wakati yamepanda kama mwezi mmoja tu uliopita lakini kumbuka wafanyakazi wa se
You are wrong. Hiyo asilimia ni kwa mshahara wa kima cha chini. Asilimia itakuwa inapungua kadri mshahara unavyokuwa mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…