Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Hahaha unajua kuna mambo unaweza kutazama unabaki kucheka tu unajiuliza hii watu wanafanya siasa au ni kweli ndio uwezo wao wa kufikiri!!!?....sisi waafrica tuna ulemavu wa akili hayo ni maumbile mkuu.

Sisi hatufanani kabisa na aina nyingine za binadamu ni hivyo tu ukisema unaweza onekana sio.
Watu wa kulalamika kwa kila Jambo litendwalo na Serikali hataisha.Yaani Serikali imeamsha ari kwa wafanyakazi wake lakini BADO Kuna watu hawaoni jitihada hizi
 
Jana nilimsoma sana jamaa mmoja wa kuitwa DINHO, nikaijuliza serikali ina mapato gani ili kuweza kuongeza 23.3% flat rate. Yaani anywpata 3,000,000 aongezewe 23.3% sawa na yule wa 270,000? Kwamba mtu wa 3mil aongezewe almost 700k kweli? Kwa uchumi gani tulionao.

Mleta mada naamini upo sahihi kabisa. It'll never be flat rate, lakini pia huo uchumi wetu ni mdogo sana.
Yaani Hadi tume iliyoundwa kukasimu nyongeza ya mshahara mnadhani haukuwa terms?Acheni Serikali ithamimi watumishi wake positively.Asingeongeza mngesema Serikali haijali wafanyakazi
 
Hakuna namna, either anakuja mwingine kama JPM kurekebisha mahesabu, kubana matumizi, kuweka vipaumbele sahihi kwa nguvu za kidikteta (hakuna mbadala) au tutauzwa jumla jumla.

Options nyingine ni kama ya watu wa Sri Lanka.
Yaani roho mbaya tu...waacheni watumishi nao waenjoy nchi Yao...mbona nyie mnapiga pesa ndefu na hatusemi?
 
Punguza kuwa nabii wa majanga (prophet of doom). SSH ameamua kuongeza mishahara ni suala zuri kuliko kuumiza mamilioni ya watu wakaishi kwa vinyongo wakati maisha haya ni mafupi.
Uko sahihi...yule dictator wao ambaye hakuongeza hata 10/- Yuko wapi Sasa hivi!?..acheni watumishi nao waenjoy nchi Yao
 
Makusanyo ni 1.5 trilion kwa mwezi na matumizi ya kulipa madeni na mishahara tuu ni 1.8 trillion kwa mwezi, hapo hakuna kuchomoka tutakuwa watumwa tuu wa mabeberu , kitakachofuata mabeberu wakataa kutukopesha itabidi tuchapishe za kwetu inflation itapiga 1000% na mkate utakuwa milioni mbili then watu itabidi waingie mtaaani halafu either tutapata dictator la kututesa au smart wa kuturudisha mstarini, sikujua kama hali ni mbaya kiasi hicho
Mbona ww mshahara wako ni 1.2M take home ...Ila umekopa 20M halafu inabaki 300k take home na matumizi yako ni 500k kwa mwezi!! Lakini mbona watu wanaishi?
 
Ukisoma vizuri kitabu cha WHY NATIONS FAIL ( The Origins of Power,Prosperity & Poverty) cha DARON ACEMOGLU na JAMES A.ROBINSON utajua kwa uhakika ni kwa nini Tanzania yetu ni masikini hivi na itachukua muda mrefu kubadili hali hii.

Kwa ufupi ni kwamba tunacho kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maendeleo katika Nchi yetu kasoro watu wenye maarifa na taasisi imara.

Hata watu wachache wenye maarifa tulionao pia wana maarifa yaliyopitwa na wakati (obsolete) au waliyo karirishwa tu! Tunaweza kusema maarifa yao hayo ni USELESS KNOWLEDGE tu.

Nchi bila uzalishaji na kuingiza Nguvu kazi kubwa katika uzalishaji ili kuongeza tija ni kazi bure tu.

Viongozi wetu na wachumi wetu waliwasoma akina Adam Smith kwenye THE WEALTH OF NATIONS kwa ajili ya kukariri kujibia mitihani tu!

Watu wetu hata wasomi wakubwa hawajui kutafsiri hata vitu basic kabisa!

Watu wanaambiwa kima cha chini la Mshahara kimeongezeka kwa asilimia 23.3% ,wao wanakimbilia Rais ameongeza Mishahara kwa asilimia 23.3% ( akili za Ki- Mwijaku Mwijaku)!

Jiulize kwanza kama Mishahara itaongezwa kwa asilimia 23.3% yote ,Wage Bill yetu itakuwa Shilingi ngapi?!

Wage Bill ikifika bilioni 900 kwa mwezi na madeni tunayolipa kwa mwezi ni bilioni 900 wakati Mapato yetu kwa mwezi Trilioni 1.5 ( bilioni 1500) Nchi itakwendaje?!

Ukitaka kujua Nchi hii ina tatizo kubwa katika Wealth Creation angalia utitiri wa tozo katika mafuta!

Kwahiyo ukifuatilia sasa mjadala ni asilimia 23.3% ya ongezeko la Mishahara ni kwa kima cha chini pekee au Mishahara yote!

Ongezeko la bajeti kwa ujumla ni 19.51% maana yake ni nini?
 
Unauliza swali au umetoa hoja?

Something has to give ndio mwisho wa miradi mikubwa ya barabara na other necessary infrastructure za kuchochea uwekezaji maeneo yote ndani ya Tanzania.

Hawa ni short sighted sio nation builders wapo kwa sababu ya kupigiwa makofi sio kuangalia Tanzania ya kesho.

Well kupanga ndio kuchagua, wanajibebesha majukumu based on optimistic scenario which is usually highly unlikely ya kukuwa kwa mapato.

It is not rocket science kuona matatizo waliyoamua kujitwisha ili kufurahisha kadamnasi nadhani Tanzania ndio nchi pekee iliyoingeza mishahara wakati dunia nzima ina pambana na kushusha inflation with subsidising policies bei ya bidhaa ziwe stable.
Ndani ya miaka saba maendeleo gani yalichochewa?

Acheni roho mbaya
 
Hesabu za kihasibu siku zote zina sura mbili, unapoongeza ni lazima uwe umepunguza au itapunguza mahali.
Ongezeko la 23.3% ambalo kwa vyovyote litagusa kima cha chini ni sharti liende sambamba na punguzo la 23.3% kutoka kwenye vipato vya watumishi wote wa ngazi za juu kwenye mihimili yote na hasa taasisi ya Urais.
 
Mishahara ni sehemu ya fiscal policy and monetary policy kwa sehemu. Wewe unataka kuleta classical economics pekee na kidogo Macro economics.

Wage na employment zina sehemu pia katika kuchangia uzalishaji.
Wewe unataka underemployment ambayo haina nafasi katika uchumi.
Kwa nchi zetu ambazo middle class ni ndogo au hakuna kabisa, namna pekee ya kuboresha purchasing power(kufungua vyuma) ni kwa kuongeza mishahara kila mwaka.
Kwa namna hiyo itasaidia kutengeneza wajasiriamali wadogo na watu wa kujitanua kidogo.
Waajiriwa wa nchi wamebeba sehemu kubwa ya maskini wengine.
Ukiongeza mishahara maanake na PAYE inaongezeka na hivyo TRA
NYUMA YA KILA MTUMISHI MMOJA KUNA WASIO WATUMISHI 8+
 
Mkuu
Mi Binafsi sioni tena kutangazwa bkwa miradi ile mikubwa ya kimkakati!
Sijui nini kumetokea hadi sasa!
NAJIULIZA
Mwenye majibu naomba!!
SGR haijamalizika, Stigler bwawa sijui Nyerere Hydropower haijamalizika, na miradi aliyoiacha mwendazake haijamalizika, unataka ianzishwe mingine? Tumalize hiyo kwanza
 
IMG_6421.jpg
 
Yaani Hadi tume iliyoundwa kukasimu nyongeza ya mshahara mnadhani haukuwa terms?Acheni Serikali ithamimi watumishi wake positively.Asingeongeza mngesema Serikali haijali wafanyakazi
Uwe unajifunza kusoma na kuelewa mkuu, kuna mahali umenisoma napinga nyongeza ya mishahara au unakurupuka.
 
Hatutaki ujinga, kama kima cha chini ndicho kimeongezwa basi watu waelezwe ukweli bayana na siyo sifa za kijinga za akina Mwijaku!
Tanzania hatuna uwezo wa kuongeza Wage Bill yetu hata kwa 10% kwa sasa!
Mbona barua ya Ikulu imesema wazi kuwa hiyo asilimia iliyoongezwa ni kwa kima cha chini? Tatizo linaanzia wapi? Miaka yote mishahara inapoongezwa hutangazwa asilimia inayoongezwa kwa kima cha chini na inaenda inapungua kadri mshahara unavyokuwa mkubwa. What is the problem this time?
 
Back
Top Bottom