Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Kwa taarifa yako Watumishi wengi hawana fedha kwani fedha zao zinabaki Bank walishazikopa.
Na wewe hujui kitu. Benki wanakata actual money. Hawakati asilimia. Kama benki ilikuwa inakukata sh. Laki moja ukiwa na mshahara wa laki tano, hata ukilipwa milioni tano, wataendelea kukata laki hiyo hiyo.
 
Say agin and again! Matokeo ya wenye upeo mdogo kupewa uongozi. Unaambiwa hata Mwingulu eti ni waziri wa fedha na mambo ya uchumi! Kweli hatujipendi!
Hili la Mwigulu umesema kweli. Mwigulu Ni empty head, chokoraa la singida. Sina ukabila au kidharau Kabila fulani, lakini singida hakuna mtu wa weledi wa level hiyo kushika nafasi nyeti Kama hiyo. Exception Ni Lisu Basi!
 
Roho mbaya imekujaa...
Wafanyakazi walipokaa miaka 7 Bila kuongezewa Chochote Ndio maendeleo yalikuja??
Nibora hasinge ongeza mishaara mfumuko wabei utakuwa mkubwa Sana vitu vita panda bei mfano Kodi ya Nyumba chumba cha 50,000 kitapanda mpaka 60,000.
 
Ndugu mtoa mada una point ya msingi ingawa bahati mbaya mada yako imevamiwa na waimba ngonjera.......lakini kimantiki hili ongezeko halipatani na uhalisia....nadhani ni muendelezo wa wanasiasa wa nchi kujiandalia mazingira ya uchaguzi ujao......bila kuangalia matokeo ya maamuzi yao.......haya ni moja ya matokeo ya kuwapa nafasi ya kufanya maamuzi watu wenye uwezo mdogo wa akili kwa niaba ya taifa kwa ujumla......
Pesa za nyongeza za mishaara zitatokana na mikopo kutoka world Bank
 
Naona mfanyishwa kazi unafurahia tangazo na unachukia ukweli wa tangazo.
Sasa sikiliza wewe mfanyishwa kazi, alichoeleza mleta mada ni kwamba ongezeko hilo haliwezekani. Maana pato jumla la mwezi ni dogo kuliko mahitaji jumla ya mwezi.
Litawezekana tu kwakukopa nje ya nchi
 
Usijiangalie wewe,angalia pia vitu vimepanda bei-malalamiko yote haya ni kutokana na vipato vya watu kuwa vidogo ndio maana unaona kelele nyingi ya vitu kupanda bei.So,sote tunajua the only solution to that ni kuongeza fedha mtaani ili watu waanze kufanya production.

Kama Serikali una njia 2 za kuweka hela kwenye mzunguko ni either utekeleze miradi ambayo itakayopeleka hela kwa watu au uongeze mishahara.Kumbuka 80% ya miradi yetu Wakandarasi ni wa nje hivyo fedha zote ukizotoa kwenye hiyo miradi zinahama kwenda Nchi zingine na huku fedha za ongezeko LA mishahara mostly zitaenda kwenye shughuli nyingi zinazomilikiwa na wazawa.
Vicious circle hiyo!

Bei za vitu ikipanda, dawa huwa ni kupunguza fedha mitaani siyo kuongeza. Mabenki hupandisha interest rates ili kupunguza fedha mitaani. Sasa wakati bei inapanda wewe unasema utaongeza fedha mitaani maana yake ni kuwa bei zinapanda maradufu.

Bei kupanda maana yake ni kuwa kuna fedha nyingi mitaani kuliko thamani ya bidhaa zinazouzwa, kwa hivyo bei inapanda ili thamani ya bidhaa iwe sawa na hela zilizoko mitaani. Hayo ni maelezo mepensi kwa lunga rahisi watu wa uchumi wanaweza kutoa details zake.
.
 
Sawa tu kuliko jiwe lenu lilikaa miaka 7 bila hata 1% nyongeza, roho mbaya tu, Sasa imemfikisha wapi?
Yeye alizibiti mfumuko wa vitu muhimu, baada ya miezi miwili huduma muhimu zitakuwa juu, mfano Hospital galama Zita panda, bill ya maji, umeme, Kodi ya Nyumba.
 
Walimsifia uhuru Kenyata kutaja asilimia ya ongezeko, tena alitaja asilimia 15, Samia kaenda mbali, kaongeza 23 percent
Kima chachini cha Kenya na Tanzania ni Sawa? Moka watu wafanishe %?
 
Ukisoma vizuri kitabu cha WHY NATIONS FAIL ( The Origins of Power,Prosperity & Poverty) cha DARON ACEMOGLU na JAMES A.ROBINSON utajua kwa uhakika ni kwa nini Tanzania yetu ni masikini hivi na itachukua muda mrefu kubadili hali hii.

Kwa ufupi ni kwamba tunacho kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maendeleo katika Nchi yetu kasoro watu wenye maarifa na taasisi imara.

Hata watu wachache wenye maarifa tulionao pia wana maarifa yaliyopitwa na wakati (obsolete) au waliyo karirishwa tu! Tunaweza kusema maarifa yao hayo ni USELESS KNOWLEDGE tu.

Nchi bila uzalishaji na kuingiza Nguvu kazi kubwa katika uzalishaji ili kuongeza tija ni kazi bure tu.

Viongozi wetu na wachumi wetu waliwasoma akina Adam Smith kwenye THE WEALTH OF NATIONS kwa ajili ya kukariri kujibia mitihani tu!

Watu wetu hata wasomi wakubwa hawajui kutafsiri hata vitu basic kabisa!

Watu wanaambiwa kima cha chini la Mshahara kimeongezeka kwa asilimia 23.3% ,wao wanakimbilia Rais ameongeza Mishahara kwa asilimia 23.3% ( akili za Ki- Mwijaku Mwijaku)!

Jiulize kwanza kama Mishahara itaongezwa kwa asilimia 23.3% yote ,Wage Bill yetu itakuwa Shilingi ngapi?!

Wage Bill ikifika bilioni 900 kwa mwezi na madeni tunayolipa kwa mwezi ni bilioni 900 wakati Mapato yetu kwa mwezi Trilioni 1.5 ( bilioni 1500) Nchi itakwendaje?!

Ukitaka kujua Nchi hii ina tatizo kubwa katika Wealth Creation angalia utitiri wa tozo katika mafuta!

Kwahiyo ukifuatilia sasa mjadala ni asilimia 23.3% ya ongezeko la Mishahara ni kwa kima cha chini pekee au Mishahara yote!

Atalipia hizi gharama vipi? How is she going to afford it?

Tufafanuliwe. Kama ni nia ni kuonekana unajali angeongeza kwa asilimia mbili tatu. Huu ni kutojua sheria za kibiashara, uchumi, dunia.

Mfanyabiasha makini hawezi kuongea liabilities kijinga hivyo kwa 23%. Wakati income yake ukiondoa gharama za matumizi iko negative. Mkopaji, anaongeza liabilities. Anajua biashara yake itakufa siku hiyo hiyo.
 
Mkuu
Mi Binafsi sioni tena kutangazwa bkwa miradi ile mikubwa ya kimkakati!
Sijui nini kumetokea hadi sasa!
NAJIULIZA
Mwenye majibu naomba!!

Hata miradi ya sasa hakutakuwa na pesa ya kuiendeleza. Yote itakufa.

Tutachukua mikopo kulipia hili tangazo.
 
Something has to give ndio mwisho wa miradi mikubwa ya barabara na other necessary infrastructure za kuchochea uwekezaji maeneo yote ndani ya Tanzania.

Hawa ni short sighted sio nation builders wapo kwa sababu ya kupigiwa makofi sio kuangalia Tanzania ya kesho.

Well kupanga ndio kuchagua, wanajibebesha majukumu based on optimistic scenario which is usually highly unlikely ya kukuwa kwa mapato.

It is not rocket science kuona matatizo waliyoamua kujitwisha ili kufurahisha kadamnasi nadhani Tanzania ndio nchi pekee iliyoingeza mishahara wakati dunia nzima ina pambana na kushusha inflation with subsidising policies bei ya bidhaa ziwe stable.
Gang at work, pole Sana, Sasa ni muda wa Watumishi nao kuenjoy keki ya Taifa. Usiteseke Sana my sister

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Ukikuta deni la nchi $42.1 billion na tumewekwa as moderate risks kwa zaidi ya miaka 10.

Ukalishusha deni ndani ya miaka mitatu mpaka $37.4 billion kupewa hadhi ya low risk.

Katika muda wako ukakopa labda $5 billion na ukalipa $5 billion na mpaka unafariki deni la nchi lipo $37.4 billion; maana yake ume maintain the level of debt.

Ni rahisi sana kuwaambia watu, jamaa alikuwa anakopa sana lakini awakwambii katika alichokopa alilipa kiasi gani ndani ya muda wake.

Kwenye uongozi wa Magufuli deni la taifa lilikuwa stable baada ya kulishusha na kuitoa nchi from moderate risk to low risk.

Mwaka mmoja wa maza tumerudi tena kwenye moderate sasa hayo maamuzi yakupanda au kushushwa yanaenda sambamba na dept payments to revenue collection ata wakiongopa makusanyo yameshuka, halafu bado wanajiongeza admin costs.

The nonsense is beyond hivi vitu huwa vinakuja kuumiza mbeleni uwezi vificha vikianza kuuma tupo hapa.

Maumivu yatakuwa makumbwa sana. Tusubiri.

Bond markets ( wale wanaotukopesha) zinasemaje leo, maoni yao yakoje leo. Interest rates imepanda au kushuka.

Sababu hawa jamaa kama hawaamini utaweza kuwalipa, riba inapanda, wakiwa na uhakika na wewe inashuka.
 
Ukisoma vizuri kitabu cha WHY NATIONS FAIL ( The Origins of Power,Prosperity & Poverty) cha DARON ACEMOGLU na JAMES A.ROBINSON utajua kwa uhakika ni kwa nini Tanzania yetu ni masikini hivi na itachukua muda mrefu kubadili hali hii.

Kwa ufupi ni kwamba tunacho kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maendeleo katika Nchi yetu kasoro watu wenye maarifa na taasisi imara.

Hata watu wachache wenye maarifa tulionao pia wana maarifa yaliyopitwa na wakati (obsolete) au waliyo karirishwa tu! Tunaweza kusema maarifa yao hayo ni USELESS KNOWLEDGE tu.

Nchi bila uzalishaji na kuingiza Nguvu kazi kubwa katika uzalishaji ili kuongeza tija ni kazi bure tu.

Viongozi wetu na wachumi wetu waliwasoma akina Adam Smith kwenye THE WEALTH OF NATIONS kwa ajili ya kukariri kujibia mitihani tu!

Watu wetu hata wasomi wakubwa hawajui kutafsiri hata vitu basic kabisa!

Watu wanaambiwa kima cha chini la Mshahara kimeongezeka kwa asilimia 23.3% ,wao wanakimbilia Rais ameongeza Mishahara kwa asilimia 23.3% ( akili za Ki- Mwijaku Mwijaku)!

Jiulize kwanza kama Mishahara itaongezwa kwa asilimia 23.3% yote ,Wage Bill yetu itakuwa Shilingi ngapi?!

Wage Bill ikifika bilioni 900 kwa mwezi na madeni tunayolipa kwa mwezi ni bilioni 900 wakati Mapato yetu kwa mwezi Trilioni 1.5 ( bilioni 1500) Nchi itakwendaje?!

Ukitaka kujua Nchi hii ina tatizo kubwa katika Wealth Creation angalia utitiri wa tozo katika mafuta!

Kwahiyo ukifuatilia sasa mjadala ni asilimia 23.3% ya ongezeko la Mishahara ni kwa kima cha chini pekee au Mishahara yote!

Umeandika vyema, ila makasiriko yanamekuzidi. Unaposema maarifa ya watu wote serikalini ni useless au yamepitwa na wakati , ina maana hata ya kwako pia ni useless kwani wewe ni uzao uleule labda kama una exemption. Au umebaki wewe tu ndiye mwenye maarifa yanayoenda na wakati? Au walioko nje ya mfumo wa serikali tu ndo wenye maarifa yanayofaa?

Ni kweli mshahara utapanda 23.3% kwa kima cha chini, lakini kwa mfumo wa kodi kila mshahara wa mfanyakazi aliyeajiriwa serikalini, ndani yake kuna kima cha chini cha mshahara. Hivyo, ni lazima kuna maelezo ya jinsi ya adjustments zitakavyokuwa.

Pamoja na hayo yote hakuna aliyeweza kutoa maelezo yakinifu kuwa ndani ya kukokotoa hiyo mishahara mingine itakuwaje wakati umepandisha kima cha chini. Je kuna maelezo ya ziada kwa kabrasha husika, nadhani kuna haja ya kusoma document yote kabla ya kuona kuwa kila kitu ni useless. Hapa suala si kutosha au kutokutosha mshahara bali jinsi ya kujenga hoja. Neno IKIWEMO lina maana kubwa kwenye taarifa rasmi.

Pia, haya makasiriko mbona hayakuonekana wakati iliposemwa PAYE imeshushwa to a single digit?? Maana inabeba ujumbe uleule wenye ukakasi pia.
 
Sasa hivi serikali inalipa wafanyakazi wake 500bn kwa mwezi.

Tu assume serikali iwaongezee kila mfanyakazi wake 50% ya mshahara wake.

Hii ina maana wage bili itakuwa 750bn kwa mwezi.

Je serikali haiwezi kupata hiyo 250bn kwa mwezi?

Kwa mwaka ni kiasi gani? 1.5 trillion kwa mwaka. Miaka mitano. Piga hesabu.

Mapato inabidi yakue zaidi ya matumizi ndio unaongeza mshahara kwa kiwango hicho. Angeongeza ila sio kwa kiwango hicho.

Vipi kuhusu miradi ya maendeleo, ya kimkakati kama SGR, barabara, maji, bwawa la umeme litakalokupunguzia gharama ya umeme wako nyumbani. Pesa itatoka wapi?
 
Someni tena ile taarifa ya Ikulu wandugu. Haikusema kilichopandishwa kwa asilimia hiyo ni kama cha chini peke yake. Labda hizi taarifa za Ikulu zianze kutolewa kwa lugha za makabila pia.
 
Gang at work, pole Sana, Sasa ni muda wa Watumishi nao kuenjoy keki ya Taifa. Usiteseke Sana my sister

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app

Unakosea kuleta akili kama hizi ( kejeli, dhihaka, matusi) kwenye mambo muhimu.

Wote tuna ndugu serikalini. Wengine tupo serikalini.

Issue ni kwamba tunaweza kuwalipa hizi pesa baada ya miaka mitatu? Au itabidi wengi wapunguzwe kazi sababu hazina haina pesa.

Elimu bure itaendelea, vituo vya afya vitajengwa. Barabara, umeme maji, miundombinu kutakuwa na pesa ya kuwafikia Watz wengi?
 
Makusanyo ni 1.5 trilion kwa mwezi na matumizi ya kulipa madeni na mishahara tuu ni 1.8 trillion kwa mwezi, hapo hakuna kuchomoka tutakuwa watumwa tuu wa mabeberu , kitakachofuata mabeberu wakataa kutukopesha itabidi tuchapishe za kwetu inflation itapiga 1000% na mkate utakuwa milioni mbili then watu itabidi waingie mtaaani halafu either tutapata dictator la kututesa au smart wa kuturudisha mstarini, sikujua kama hali ni mbaya kiasi hicho
 
Back
Top Bottom