Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Usijiangalie wewe,angalia pia vitu vimepanda bei-malalamiko yote haya ni kutokana na vipato vya watu kuwa vidogo ndio maana unaona kelele nyingi ya vitu kupanda bei.So,sote tunajua the only solution to that ni kuongeza fedha mtaani ili watu waanze kufanya production.

Kama Serikali una njia 2 za kuweka hela kwenye mzunguko ni either utekeleze miradi ambayo itakayopeleka hela kwa watu au uongeze mishahara.Kumbuka 80% ya miradi yetu Wakandarasi ni wa nje hivyo fedha zote ukizotoa kwenye hiyo miradi zinahama kwenda Nchi zingine na huku fedha za ongezeko LA mishahara mostly zitaenda kwenye shughuli nyingi zinazomilikiwa na wazawa.
 
Ndugu mtoa mada una point ya msingi ingawa bahati mbaya mada yako imevamiwa na waimba ngonjera.......lakini kimantiki hili ongezeko halipatani na uhalisia....nadhani ni muendelezo wa wanasiasa wa nchi kujiandalia mazingira ya uchaguzi ujao......bila kuangalia matokeo ya maamuzi yao.......haya ni moja ya matokeo ya kuwapa nafasi ya kufanya maamuzi watu wenye uwezo mdogo wa akili kwa niaba ya taifa kwa ujumla......
 
Roho mbaya imekujaa...
Wafanyakazi walipokaa miaka 7 Bila kuongezewa Chochote Ndio maendeleo yalikuja??
Naona mfanyishwa kazi unafurahia tangazo na unachukia ukweli wa tangazo.
Sasa sikiliza wewe mfanyishwa kazi, alichoeleza mleta mada ni kwamba ongezeko hilo haliwezekani. Maana pato jumla la mwezi ni dogo kuliko mahitaji jumla ya mwezi.
 
Mishahara ni sehemu ya fiscal policy and monetary policy kwa sehemu. Wewe unataka kuleta classical economics pekee na kidogo Macro economics.

Wage na employment zina sehemu pia katika kuchangia uzalishaji.
Wewe unataka underemployment ambayo haina nafasi katika uchumi.
Kwa nchi zetu ambazo middle class ni ndogo au hakuna kabisa, namna pekee ya kuboresha purchasing power(kufungua vyuma) ni kwa kuongeza mishahara kila mwaka.
Kwa namna hiyo itasaidia kutengeneza wajasiriamali wadogo na watu wa kujitanua kidogo.
Waajiriwa wa nchi wamebeba sehemu kubwa ya maskini wengine.
Ukiongeza mishahara maanake na PAYE inaongezeka na hivyo TRA kukusanya zaidi.
 
Sawa tu kuliko jiwe lenu lilikaa miaka 7 bila hata 1% nyongeza, roho mbaya tu, Sasa imemfikisha wapi?
 
Lakini nakubaliana na wewe kwenye eneo la uzalishaji na kuongeza fedha za kigeni bila kutegemea utalii, mikopo na misaada peke yake.
Watu watasema tumeachwa kiteknolojia.
Lakini kuna maeneo tunaweza. Kwa mfano kuna vitu vina soko sana humu nchini na tunaweza kuzalisha badala ya kutumia akiba ya fedha za kigeni kununua. Kuna vitu kama vile:
1. Ngano
2. Alizeti
3. Mafuta ya chakula
4. Sukari
5. Samani za maofisini na majumbani
6. Pombe/Vileo za aina mbali mbali
 
Umeandika ujinga tupu, hao watumishi hawafanyi kazi ya kanisa, wanastahili kupata kipato Cha kuwafanya waendeleze maisha yao, na kipato hicho kitaingia mtaani na kitazunguka na serikali itapata faida
 
mnaoponda wafanyakazi kuongezewa mshahara mnamioyo ya korosho na ya kichawi mlifurahi sana kipindi Cha miaka SITA bila nyongeza ya mshahara nyambafuu mtakula hizo Barabara zenu mnazotaka zijengwe
Halafu unakuta ni hao hao wanaowapinga mizinga watumishi mitaani au wanawasengenya kwamba wakati wa Utumishi wao hawajafanya maendeleo
 
su
sukuma gang mnatabika mkiwa pande zipi za Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…