P02: MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI
Lina wizara 14, Mawaziri 14, hakuna Manaibu Mawaziri
Wizara hizo ni:
1. Ofisi ya Rais (menejimenti ya utumishi wa umma, katiba sheria na utawala bora)
2. Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano, mazingira)
3. Ofisi ya waziri mkuu(sera, bunge, uratibu)
4. Afya Jamii (afya, maendeleo ya jamii, jinsia, makundi maalumu)
5. Elimu
6. Uchumi (mipango, uwekezaji, viwanda, biashara)
7. Kazi (kilimo, ufugaji na uvuvi)
8. Mali asili (maji, ardhi, utalii)
9. Ujenzi na uchukuzi (+nyumba, makazi)
10. Nishati na Madini
11. Mambo ya nje
12. Mambo ya ndani(+utamaduni, michezo, habar)
13. Ulinzi na jkt
14. TAMISEMI
Baraza la Mawaziri la Tanzania ni ngazi ya juu ya serikali au mkono wa utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mfumo wa mgawanyo wa madaraka.
Baraza hili linaundwa na rais, makamu wa rais, rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri wote. (Manaibu mawaziri si sehemu ya baraza.) Mwanasheria Mkuu anashiriki katika mikutano ya baraza lakini hana haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.
Muundo wa wizara:
Tanzania haina muundo rasmi wa wizara kikatiba, na hivyo kila Rais huunda baraza lake kwa jinsi aanavyo inafaa kurahisisha utendaji wake. Hii imepelekea kuwa mabadiliko mbalimbali ya kimuundo wa wizara na idadi ya mawaziri na hata manaibu mawaziri
Tuangalie mifano ya awamu tatu za mwisho za uongozi:
KIKWETE 2005
Wizara 25, Mawaziri 29, Manaibu 31
KIKWETE 2010
Wizara 28, Mawaziri 33, Manaibu 20
MAGUFULI 2015
Wizara 18, Mawaziri 19, Manaibu 16
MAGUFULI 2020
Wizara 23, Mawaziri 23, Manaibu 23
SAMIA (sasa)
Wizara 26, Mawaziri 26, Manaibu25
Kwahiyo, kama nchi ifike pahala tukubaliane njia ya kupita ili kuwa na uelekeo mmoja.
Ufanisi wa serikali haitegemei uwingi wa viongozi, isipokuwa kuwa na viongozi bora wenye uthubutu na uzalendo wa kweli.
Kuwa na baraza dogo la mawaziri kutapunguza matumizi makubwa ya kuendesha serikali na hii imekuwa kiu na matamanio ya wananchi walio wengi. Ni muda wa kuwa na mfumo au muundo maalumu.
Ningepata nafasi ya kumshauri Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, basi hizo ndizo idadi ya wizara ambazo ningeshauri. Wakati mwingine unaweza kuwa na watu bora wengi ambao ungependa uwatumie hivyo kuwa ngumu kupunguza na kubaki na idadi hiyo, lakini kwaajili ya Nchi yako naamini itakuwa ni maamuzi sahihi endapo jambo hili litakupendeza.
Pili, ikikupendeza hata kama sio kwa idadi na muundo sawa na huu, ni vema utaratibu unaofanana na huu ukaundwa na kuwekewa sheria au katika katiba kabisa ili siku zote na awamu zijazo nchi iendeshwe kwa mfumo huu wa kuwa na baraza dogo.
Makatibu wakuu wa wizara wanaweza kuwa hata wawili kutegemea na ukubwa wa wizara.
NAWASILISHA. ASANTE
Nakaribisha kukosolewa, maoni, mapendekezo na mitazamo tofauti
Why70278@gmail.com
Kwembe-Ubungo, Dar es salaam kwa sasa