Common Folk
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 909
- 4,050
Baba wa taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema "Wapo viongozi wakishindwa kukubalika kwa sera basi wanaamua njia mbalimbali ikiwemo Ukabila na Udini. Ukitumia Dini au Ukabila kukubalika unagawa watu, kazi ya uongozi ni kujenga watu wawe kitu kimoja".
Kwanza dini zote zinamuabudu Mungu mmoja, kasoro namna ya kuabudu tu.
Pia makabila yote tuko sawa tu, maisha yetu ni yale yale, hakuna upendeleo wa kikanda au kikabila. Naweza kutoka mkoa wowote na nikaenda kuishi popote bila shida yoyote ile.
Mitaani tunaishi watu wa dini zote, lakini tuna umoja sana. Matukio ya kijamii kama harusi na misiba tunashirikiana sote kama jamii. Ukienda msibani mawaidha anayotoa Padri, Mchungaji, Sheikh yanafanana mrengo, kwamba kifo kitukumbushe hapa duniani tunapita tu na tuishi kwa kufanya mema ili tufike Mbinguni au Akhera.
Katika karata Baba wa Taifa alizichanga vyema basi ni katika hili eneo. Hapa apewe maua yake!
Ndiyo maana jamii nzima inawashangaeni nyie viongozi wa serikali mnaotumia DINI kujaribu kuhalalisha UPUMBAVU wenu!