Bishanga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2008
- 15,321
- 10,075
Mimi naona we have a problem kwa sababu hapa tuna mafungu mawili ya wanafunzi/wazazi.Fungu la kwanza ni la kina sisi hoe yakhe na la pili ni la wenye nazo.Unapofunga chuo wote wanaumia waliojilipia na wanaosoma kwa mikopo.Suluhisho lipo, mzazi mwenye uwezo amlipie mwanae asiye nao alipiwe hata 100% .Njia rahisi ya ku control hii ni ku publish kwenye magazeti orodha ya wanafunzi WOTE waliopitishwa kupewa mikopo,anwani zao na za wazazi/walezi wao kisha umma wa watanzania upewe fursa ya kutoa pingamizi kwa siri.Watanzania tunajuana, atakayesema mzazi wake ni lofa wakati zimemtembelea umma utamuumbua,na adhabu ya ku cheat iwe ni kifungo bila faini,akifungwa mzazi mmoja/mtoto mmoja wengine tutashika adabu.TRA wahusishwe maana vibopa wote wa nchi hii wana TIN number.Mambo ya pangu pakavu tia mchuzi tuachane nayo.mnasemaje wadau?