''...Tanzania haitakalika''

Mimi naona we have a problem kwa sababu hapa tuna mafungu mawili ya wanafunzi/wazazi.Fungu la kwanza ni la kina sisi hoe yakhe na la pili ni la wenye nazo.Unapofunga chuo wote wanaumia waliojilipia na wanaosoma kwa mikopo.Suluhisho lipo, mzazi mwenye uwezo amlipie mwanae asiye nao alipiwe hata 100% .Njia rahisi ya ku control hii ni ku publish kwenye magazeti orodha ya wanafunzi WOTE waliopitishwa kupewa mikopo,anwani zao na za wazazi/walezi wao kisha umma wa watanzania upewe fursa ya kutoa pingamizi kwa siri.Watanzania tunajuana, atakayesema mzazi wake ni lofa wakati zimemtembelea umma utamuumbua,na adhabu ya ku cheat iwe ni kifungo bila faini,akifungwa mzazi mmoja/mtoto mmoja wengine tutashika adabu.TRA wahusishwe maana vibopa wote wa nchi hii wana TIN number.Mambo ya pangu pakavu tia mchuzi tuachane nayo.mnasemaje wadau?
 
Ndugu zangu wa JF;
Kwanini Vyuo vya umma tu? Ina maana vyuo vingine, Binafsi, havifaidiki na Bodi ya mkopo? Why? Kwani huko Tumaini hakuna maskini? Au ndio yaleyale, myths, ya zamani?

Je watanzania tungekuwa wa kweli, wakati wa ujazaji wa form za mkopo haya yote yangetokea? je Kuficha ukweli, hasa wa vipato vyetu, ndio tatizo?
 
mikopo inatolewa kwa vijana wote bila kujali chuo ni public au private.
 
mikopo inatolewa kwa vijana wote bila kujali chuo ni public au private.

Nalifahamu hilo, lakini nataka kujuwa kwanini vyuo vya umma tu? Namanisha hii mikikimikiki, kama funga chuo kwasababu ya % ipo zaidi kwenye public universities? Kwanini?
 
1. Hivi utoaji Vitambulisho vya taifa vimefikia wapi?

2. Kumekuwepo na oungo..ktk ujazaji wa hizi form...kutambua nani maskini na yupi anauwezo. Huu ni utamaduni mbaya wa kusema uongo na kupeta tu bila kuchukuliwa hatua za sheria!

Waliodanganya waainishwe na kuchukuliwa hatua!
 

Mkuu interesting proposal, sina uhakika na practicability yake...mwendo kichina china tu.
 

Umenena mkuu Mzalendohalisi. Mambo haya yamigomo, kurukushani hutokana na tabia yetu sis Watanzania ya kusema uongo. Nadhani yatupasa kujadili swala la "UONGO WETU WATANZANIA NDIO UNAOTUWEKA KATIKA MATATIZO" Nisieleweke vibaya, kuna wengine ni wakweli, ila niwangapi? Je ninaweza kusema Tamaa ya vitu uharaka wa kupata (mfano fedha, TV, simu nzuri, niwe na kiwanja, nguo n.k) ndio inayochangia uongo katika mambo mengi tunayoyafanya"? Je hatujalishishwa maadili ya ukweli? Je na hao bodi ya mkopo, kwa kuwa ni watanzania, na wenyewe ni waoungo? Inawezekanaje watoto wa first year mapacha, pale UDSM (2007/2008)-saizi wapo 2nd year, wakapewa moja D na mwingine B wakati wamejaza sawa kasoro majina? Bahati nzuri wamesoma same schools (A-level, O-level, Primary)?
 
Mkuu hii hesabu ya kwamba zinahitajika Ths Bilioni 1200 unaweza kusubstantiate or else kuelezea source maana sijawahi kuisikia mahali pengine.

Pitia mjadala vizuri utakuta page ambayo nimederive hiyo billion 1200.
 
Mfano wa Cuna hauendani na mjadala wa wanafunzi wa Tanzania , kwa sababa Cuba wanafunzi wanasoma bila kulipa ada, lakini hawapewi pesa ya chakula wala pesa ya accomodation. Utaratibu huu unatumiwa na nchi nyingi tu za Ulaya. Wanafunzi wa Tanzania wanataka kupewa aslimia 100 ya mahitaji yao na siyo asilimia 100 ya ada.

Nadhani cha kufanyika ni kubadilisha sera kidogo na kusema utaratibu wa kuwapa wanafunzi posho ya chakula, malazi, vitabu na stationary ufutwe ili tuweze kusomesha wanafunzi wengi zaidi.
 

Mkuu hapo unakosea Cuba accomodation ni free na zipo vyuoni, msosi wa serikali, vitendea kazi vyote bure except for few private students coming from other countries. Sasa hapa msosi hamna, accomodation hazitoshi na chache zilizopo zinalipiwa. Ukikaa nje ya chuo kuna ishu ya nauli. Kumbuka uchangiaji upo wa kiaina maana nauli ya kutoka kwenu kanyigo unajilipia, hata hizo hela za mkopo hazireflect market price ya chakula na bei za kurent nyumba hivyo basi the rest unachangia, siku hizi facuulty requirements unajitegemea, na kumbuka maisha si accomodation na chakula tu!
 

Utanisamehe iwapo nitakosea lakini juu ya hiyo asilmia 100 ya bure wanapomaliza masomo hawajali maslaha ya Taifa bali hujali maslahi yao binafsi. Ndio hawa unapokuwa na haja wanakwambia kwanini ulilala wakati wenzio wanasoma? Ndio hawa wanakuja wakatwambia kuwa kilichowafikishs daraja hiyo ni akili zao si chengine na ndio hawa watakaoamuwa kufanya kazi nchi za nje kwa kisingizio cha maslaha madogo.

Ni haki yao kuja kutwambia hayo yote iwapo sasa watajihudumia lakini sasa pesa ya wananchi wakishafaulu wako huru kufanya watakavyo.
 

Cuba unayoizungumzia ni ya kati ya mwaka 1961-1979. Kuanzia mwaka 1979 kuna wanafunzi kibao tu ambao hawakai vyuoni, wengine wanakaa nyumbani wengine wanapangisha etc. na serikali haiko responsible kwa chakula wala malazi yao.Kwa sababu mfumo wa Cuba wamecopy toka Urusi, tofauti iliyopo ni kwamba Urusi kuna Private Universities. Wanafunzi wote wa Public universities Urusi hawalipi ada, ila their accomodation, chakula etc. wanajigharimia wenyewe.

Kuanzia mwaka 1961 Cuba vyuo vikuu vyote vinamilikiwa na serikali, baada ya kutaifisha vyuo binafsi. Tanzania chukua mfano wa medicine, kuna vyuo vinne vinavyotoa degree ya medicine wakati chuo cha serikali ni kimoja tu! Ukitaka serikali implipie kila mtu mahitaji yake yote, utasababisha serikali ipange bei za ada,accomodation na huduma nyingine kwenye vyuo binafsi. Je, government control ya kiasi hiki ndio tunayoitaka? Je, governement ikishaingiza mkono wake kiasi hicho mashirika na watu binafsi watavutiwa kuwekeza kwenye vyuo vikuu binafsi Tanzania?

Cuba admission ya university wanapewa kwanza members wa communist party, kama sio mamber unaweza usipate course unayoitaka. Is this what we want to emulate?
 
Cuba admission ya university wanapewa kwanza members wa communist party, kama sio mamber unaweza usipate course unayoitaka. Is this what we want to emulate?

Unahitaji kuwa na kumbukumbu vizuri hakuna mtu aliyesema nataka tuwe kama Cuba issue ni kwamba kuna nchi masikini zinazozingatia umuhimu wa elimu na mfano ikawa ni Cuba. Na hili la wacuba wanapanga nyumba mtaani na kujinunulia chakula usilifanyie assumptions au kuliopianate. Kuwa na facts not just mfumo wa Urusi umekopiwa. Je unafahamu kwamba nyumba zote after revolution zilikuwa ni za serikali, Unafikiri Daktari anayelipwa equivalent of 20 USD anarent nyumba $ ngapi, na watoto say anao wawili kwenye tertiary institutions tofauti miji tofauti aanawalipia $ ngapi kwa rent, msosi n.k

kumbuka hamna boksi kule........
 

Sijakuelewa kabisa mkuu, nafanya review za mitihani ya Kenyatta university, sikuelewi unaposema kuwa Kenya hakuna quality ya Elimu!! hii notion isiyo sahihi inaletwa na watawala kuwadumaza watanzania.Hivi ili tuonyeshe tuna elimu nzuri kuliko kenya tufanye nini? elimu ni nini hasa? clarify please,kuwa we have good quality ya elimu than kenyans!!!

Ukishindwa kutoa vithibitisho na notion hizo za vijiweni, usiseme tena sentensi hii kwa watu wengine. In short hao wenye elimu ndogo ndio wana mabenki nchini kwenu, wana NGO, organisation mpaka wana miliki magazeti ndani ya nchi yako!, ndio hao managers kwenye foreign companies nyingi ninazozifahamu, ndio wengine tunao Mlimani, I can not mentin their names, we too have professors that they studied in Kenya!

sikuelewi, nini kinatufanya turinge tuna elimu nzuri, kusoma kwa kiswahili darasa la sita na saba!, halafu kurudia kwa kiingereza form one na two??? is that what you are talking???
 
Zemarcopolo, nimejaribu kukuelewesha kama mwana JF ambaye ameingia kwenye mijadala si kwa lengo la kubisha bali la la kueleweshana, na kuangalia vitu in 3D.

NILIKUELEZA HAJA YA SERIKALI KUBADILISHA MIFUMO YA ELIMU, NA KUJITAYARISHA katika hili swala na sio kukurupuka. Nikatoa mifano ya Tz na Canada na kuona tofauti ya aina ya wanafunzi na system zilivyotofautiana. nikapendeza nini kifanyike.

To my surprise nachelea kusema, uko upande ambao wewe hukutakiwa kuwa. umetoa mfano ambao sikutegemea wa kufundisha tuition! DSM, as if everyone have that capability! they have same conditions na wanasoma kozi za aina moja-Hili sikutegemea kabisa useme.

Niliuliza kama umesoma vyuo vya elimu ya juu Tz, kwa ile hoja yako ya "TV" nilitaka ngau utaje chuo gani halafu nikichambue, sijui pengine uliishia form six, na hujasoma elimu ya juu TZ!

Maana kama swala la ratiba ya masomo unajua vyuo vyetu viliyotaight, sikutegemea kabisa useme hivi, though nilijua point zangu za kuondoa "Disco" labda zilikuingia kumbe bado hukuzisoma na kuzielewa na kuzichukua.

Nitapost tena zile hatua ambazo serikali ilitakiwa kuzifanya, na pia nini chuo wanatakiwa kufanya kwa sasa!

wakati unaongelea swala la serikali kutoweza kuwapa 100% n kuisupport serikali, na kuoa mifano ya nchi kana kwamba chochote wafanyancho wengine na sisi tuige, basi nina kuongezea swali lingine tena.

JE SERIKALI IMECHUKUA HATUA GANI YA KUZIHUSISHA BENKI KUTOA MIKOPO YA ELIMU NA WAO WAKAWA WADHAMINI????? maana to be honest sio wote wana kipato cha kila mwezi, sio wote wana magari na nyumba, sio wote wana viwanja, na mikopo ya benki mingi inatakkiwa ilipwe ila mwezi, je nchi ambazo mabenki yanatoa mikopo ya elimu kwa wanafunzi wanafanyaje? nani katoa wazo kama hilo kwetu?? serikali haijui??

kwa nini serikali inakuwa kama baba na mama wa kambo wa hawa wanafunzi, kweli there is no any other solutions?

wewe unatakiwa kubadilika mtazamo wako, au itabidi tuchukue another very effective way za kumlazimisha mtu kama wewe kuelewa na ili siku nyingine uelewe haraka zaidi!
 
Wakuu,
Swala la Elimu halina kipimo nje zaidi ya sisi wananchi wenyewe..Haya maswala ya ku copy Kenya, sijui Cuba na kadhalika hayana mpango kabisa wala hayawezi kutusaidi kitu..
Tanzania tunahitaji Elimu tena - big time, Kenya wanahitaji Elimu na Marekani wanahitaji elimu hivyo lisiwe swala la kulinganisha hata kidogo iwe kwa Quality au Quantity yote yanahitajika kulingana na watu na mazingira..
Swala la kuwa na wataalam wageni wengi ktk sehemu zetu za kazi sio ishara ya kutokuwa na wasomi isipokuwa ni ishara ya opportunity ndani ya nchi husika. Marekani, UK na hata Canada leo hii zina wasomi wengi kutoka nje ktk nafasi kibao na wageni hawa wamesababisha maendeleo makubwa sana nchini humo..
Tofauti kubwa kati ya nchi hizi na Tanzania ni kwamba wenzetu wameweza kujenga miundombinu inayoweza ku accommodate both immigrants na wazawa wakati sisi tunaajiri wageni kwa sababu hatuna imani na wasomi wetu aidha kwa sababu ya kutokuwa na exposure au akili za kimaskini (kushikiwa) zilizotokana na Utumwa wa akili.
Binafsi sikubaliani na hizo statistics zinazotolewa kuhusiana na nchi maskini kwa sababu wasomi wetu wengi wamesoma nje ya nchi badala ya ndani..Tazama toka tupate Uhuru ni hesabu kubwa ya viongozi wetu ktk serikali na mashirika wamesoma nje ya UDSM...hivyo hesabu kamili haiwezi kupatikana kwa kugeza nchi ambazo hazikufuata mfumo kama wetu. Nchi ambazo tayari zilikuwa na University zaidi ya moja na zilitosheleza kwa kiwango fulani mahitaji ya ndani na wakaweza kuchukua wanafunzi toka nchi mbalimbali toka tukitawaliwa...
 
wewe unatakiwa kubadilika mtazamo wako, au itabidi tuchukue another very effective way za kumlazimisha mtu kama wewe kuelewa na ili siku nyingine uelewe haraka zaidi!

Sasa umefika wakati unanichekesha!!!
Kama nakumbuka vizuri ulisema wewe ni mwalimu wa UDSM. Hivi kulazimisha watu ''kuelewa'' kumbe nyinyi walimu ndio mnaowafundisha wanafunzi wenu!!! Nakumbuka kuna wanafunzi walimkata mwenzao na chupa kwa sababu aliwaambia kuwa haungi mkono mgomo.
kweli hivi ndivyo mnavyopaswa kuwa wanazuoni wetu?
Na kwa ukaribu approach yako inafanana na ya mwanafunzi aliyesema ''...Tanzania haitakalika'', anaonekana kulazimisha kuwa anachotaka yeye ndio sahihi na lazima kitekelezwa immediately!!! Msiwafundishe vijana wa kitanzania kulazimisha mawazo, wafundisheni kujenga hoja zinazouzika.

Kuhusu swala la mikopo kutoka bank, ushauri ulioutoa ni mzuri, kwa mfano USA huo ndio utaratibu wanaoutumia. Hata hivyo hali tuliyo nayo ni kwamba bank zina vigezo vyake vya kutoa mikopo. Watanzania waliotmiza hivyo vigezo wanaomba mikopo bank hata hivi sasa. Anayengoja serikali ikamkopee au kumdhamini anapaswa kujua kuwa serikali kwa sasa inatumia utaratibu wa bodi ya mikopo. Utaratibu huu kama nilivyosema awali hauko perfect ndio maana unaboreshwa mara kwa mara. Inaweza ikafika wakati serikali ikaanza utaratibu wa kuwadhamini wananchi wakakope bank, lakini tusitegemee serikali ifanye kila jambo kwa wakati mmoja.
 
Last edited:

Waberoya,
I meant ktk dunia ya sayansi ya leo..Tz tupo mbele ktk machapisho ya kisayansi ukilingalisha na Kenya na Ug. Sasa nini hapo hakieleweke??

One of the reasons.. Tz invested ktk small but quality education..tofauti na kenya na ndo maana nikauliza..do we need qualitative au quantitative change??

Naona Kenya ni quantitative change..na sisi ndo tumeingia ktk hiyo direction..but we compromise quality of output!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…