''...Tanzania haitakalika''


Mkandara please !
Idadi ya wanafunzi wa Kenya waliosoma ama wanaosoma nje ni mara kumi ya idadi ya Watanzania sijui hapo utasema nini. Ukweli ni kuwa sisi ni vilaza what ever excuse we may have. Wakenya wana take opportunity ya kila nafasi inayopatikana tofauti na sisi ambao hata tunapopata scholarships za bure tunazifungia makabatini. Hatuna tu umasikini wa mali, tuna umasikini mbaya wa mawazo, period kama tunavyoshuhudia kwenye post ifuatayo.


Hivi ndivyo tulivyo na hii post ni position waliyo nayo watanzania wengi. Tuna maelezo mepesi ya kutetea hali yetu duni. Eti tunajali quality education ndiyo maana idadi ya graduates wa Tanzania ni asilimia kumi tu ya wale wa Kenya - my foot !! How hollow an argument and how low can we get. Samahani kwa lugha kama hii, lakini misimamo kama hiyo ndiyo inanifanya nihamaki, sorry.
 

No, nasema hivyo kwani mkuu, mawazo yakko tangu ulipoanza mpaka sasa hayaonyeshi kama unawafahamu watanzania, hivyo inabidi nitumie tecknic ya kuanza kueleweshana kwa mifano halisi, lakini siyo kukulazimisha kwa maana ya kutumia nguvu, -hiyo ni lugha ya picha tu mkuu. Ama sivyo ingenilazimu nihamishe ubongo wako nikupe wa mag, yoyo au wengine.

Maana yangu ni kuwa unaangalia upande mmoja tu, sioni ukitoa point zxa kuisaidia serikali kuwa watekeleze hili swala bila matatizo. sijaona point yeyote notable toka kwako, ambayo naweza kusimama sehemeu nikasema niwasaidie watz wenzangu, nimeona point za TV na tuition. ile ni lugha ya picha usijali.

Tusaidie wewe unayejua nini kifanyike kuongeza idadi ya wasomi??? katika dunia hii ya ushindani, by the way hujajibu bado umesoma chuo gani mkuu hapa Tz mkuu! nisije nikawa naongea na mtu ambaye secondari kasoma marekani, degree kachukua ulaya, kazi anafanya Tanzania!
 

supported Mag3

wengine wanasema sisi maskini lakini tuna Amani!!!

elimu ni uwezo wa kutawala maziingira na kuyaweka bora zaidi kuliko yalivyo kwa wakati huo, ndio tunapata nenio maendeleo

tunaishi katika nchi amabayo ni gofu au pori, hatuna viwanda vya kuringia, hatuna umeme, barabara,kwa kifupi tuko katika nchi maskini bora duniani

still mtu nasema tuna quality nzuri ya elimu!!!!!!!!!! kwa sababu tunachapisha majarida mengi, yako wapi aua majarida ya kisayansi, yanafanya nini?? au watu wanafnaya research wapi?? data wanachukua wapi?? jamani fungukeni macho.

umeshawaza siku moja kuwa tuna special schools za mzumbe, kibaha, na ilboru na wengi wanaomaliza PCM, huko wanasoma kompyuta na uhandisi wa umeme!!!! unajua hali yetu ya umeme Tz??

ukisema viongozi ndio tatizo , nao wamesoma wapi???

maendeleo ya nchi ndiyo yanaekezxa kama mnawasomi au la la sivyo zero, i mean sifuri.

nikauliza tena, sijapata jibu hivi quality nzuri ya elimu ni watu kusoma kwa kiswahili, na kurudia hayohayo kwa kiingereza form one na two?? wengine wanaanza tangu utotoni na lugha moja, kisha wanasoma kwa muda mfupi tunaona kama wanachemsha!!! jamani mko wapi??

waberoya
 
MzalendoHalisi,

..unasema graduates wetu ni bora kuliko wale wa Kenya lakini inapofika kwenye masuala ya ajira wakenya wanatupiga bao!!

..there are some serious problems in our education system that need to addresed. we can not keep execusing ourself that we put more emphasis on the quality than quantity of the graduates.

..nimechukulia madai yako kwamba kwasababu waalimu wetu wa UDSM wana-publish kuliko wenzao walioko Kenya, basi tunapaswa ku-conclude kwamba UDSM ina waalimu bora/vipanga kuliko wenzetu wa Kenya. sasa kwanini graduates wa UDSM wanafanya vibaya in the job market wanaposhindanishwa na wenzao wa Kenya ambao wamefundishwa na waalimu vilaza?

..nadhani vyuo vyetu vya elimu ya juu vinapaswa kujichunguza kuanzia mitaala yake, mbinu za ufundishaji, upatikanaji wa vifaa etc etc. inaelekea kwamba quality ya graduates wetu imeshuka as it is evidenced in the job market kulinganisha na ya washindani wetu toka nchi jirani.
 

Katika mjadala huu nimerudia mara kadhaa point zangu.

1. Serikali iongeze kasi ya kuboresha mfumo wa utoaji mikopo ili kuainisha wale wanaostahili kusadiwa na viwango wanavyostahili.
2. Wanafunzi waachane na tabia ya kugoma kipuuzi. Swala la kila mwanafunzi kukopeshwa asilimia 100 halipo katika karne hii.
 
Katika mjadala huu nimerudia mara kadhaa point zangu.


2. Wanafunzi waachane na tabia ya kugoma kipuuzi. Swala la kila mwanafunzi kukopeshwa asilimia 100 halipo katika karne hii.

This is good one, I nearly support it, but it seems you are supporting migomo, ila wasiwe na sababu za kipuuzi, unafikiri ni sababu gani zisizo za kipuuzi zinaweza kukufanya ukubaliane nao?

Pili unaposema katika karne hii, una maana gani, karne hii nani kaileta? hii ni karne ya nini vile?? can we say we are living in this century, or just imitating and forced by so called glabalisation kuwa tunaishi katika karne hii??

Hivi hali za maji, barabara, hospitali, uongozi ni kuwa tunathibitisha kuwa tuko kwenye karne ya sayansi na teknolojia??

Zemarcopolo, hivi tuna siasa gani vile, ujamaa na kujitegemea au ubepari, au transition?if ubepari unajua ubepari wana sera gani?? poor they will always be poor man!! je tumepitia ujima mpaka hap tulipo au tumedesa na kulazimishwa kuingia kwenye hiki kijiji cga globalisation?? unajua tunaweza kuringa kuwa tumepita hizo hatua , maana hatua hizo ziliendana na maendeleo husika wakati Europe wamekuja kuchukua malighafi huku miaka ya 1800, katika kipindi cha mapinduzi ya viwanda, sie hatuna leo hii miaka ya 2008! hata walivyoleta wazungu vimekufa, achilia mbali kuwa hatuna vyetu vyenyewe. wanaposema tunaishi katika kipindi cha sayansi na teknolojia sisi hatumo humo hata kidogo!.We dont deserve this ZeMarcopolo, we dont have our own industries, innovations, tumeishia kukopi tu na kununua mpaka pini inayotoka china, yet you seem to say this century we dont deserve to give 100% loan to student!!!!!! poorest country and remarkable country in the world like TZ, au ndio nyie mnaona kuwa ukiwa na uwezo wa kusurf, umeajiriwa na mzungu Zain au Voda, unapewa sh. 500 kwa mwezi , una tv, gari la mkopo na nyumba ya kuanga sinza BASI TUMEENDELEA, ILI MRADI UNAUWEZO WA KULA CHIPS NA KUKU ! steers. Never mention about Tanzania who lives in rural areas!

Tumedumazwa mawazo yetu, nawe wamekupata, tulishindwa, can you tell me why in 1960 we had same economical leve with many coutris in Asia, including Korea, now they are remotely far ahed of Tz, what made them to develop so fast in almost 40 years??

You are not living in this very century take this note and spread to 100 Tanzanian! la kamaunaamini hivyo wewe si mtanzania na hauijui Tanzania!!

waberoya
 

If there was ever a time when poor Tanzania needed to invest in education, it is right now even if it means kuwakopesha wanafunzi wote 100%. Dont bury your head in the sand ZeMarcopolo unless unafaidika na hizo hela ambazo hutaki wanafunzi wakopeshwe. Katika karne hii ya 21 kuendelea kuvumilia mipango ya kipuuzi ambayo haileti tija ni ulimbukeni usio na utetezi.

Nimepitia post zako zote kwenye hii mada na nimegundua unavyoshindwa kuelewa kuwa ni jukumu la serikali kuwapa elimu vijana wetu na umuhimu wa wao kupata hiyo elimu. Hivi unasukumwa na nini - ni chuki yako kwa watoto wa wakulima kupata elimu ama kuna zaidi.

Nakumbuka miaka ya nyuma watu kama wewe walizagaa serikalini na hasa wizara ya elimu. Serikali ilikuwa inaweza kupokea schorlaships kutoka taasisi na nchi mbali mbali lakini maofisa wakazifungia makabatini eti vijana hawapo.
Je, inawezekana tuna watu wana hofu kwa vijana wasomi serikalini ?

Mfano mzuri ni huu -kuna wakati India ilikuwa inatoa schorlaships karibu kwa vijana wa kitanzania 10 kila mwaka lakini waliokuwa wanapewa ni watatu ama wanne. Je ni wizu, chuki ama upendeleo zilizokuwa zinawatuma kufanya hivyo - mimi nadhani walitawaliwa zaidi na ujinga.

Gharama ambayo serikali itaingia kusomesha vijana wake leo si chochote mbele ya faida ya investment ya namna hiyo. Ni ufinyu wa mawazo kuogopa hizo gharama halafu pesa zenyewe zikaishia mifukoni mwa mafisadi. Huo ndio ukweli na nashawishika kuamini kuwa ndicho hasa kinakutuma wewe kutetea.

Maendeleo bila elimu - wapi na wapi.
 

wachache sana wenye kuangalia mambo kama wewe! asante kaka you have made my weekend.
 

1. Taabu moja ndugu confidence wanafunzi wetu inakuwa ndogo kwani wanatishiwa zaidi disco..so at the end wanakuwa na confidence kidogo na woga hence low marketalibility ktk soko ila wakipata kazi Watz ni wazuri sana angalia Botwana, SA , Lesotho n.k tunaheshimika sana pamoja na kuwa tu wachache!
2. UD has been a sucess story kwa scorlarly independent thinking ktk Afrika kwa mda mrefu tangu wakati wa Mwalimu..sema hali ibadilike sasa!

This is a quality aspect..ila kwa quantitity Kenya wana graduates wengi wenye confidence zaidi na English safi zaidi ktlk soko!

Ndo nikauliza quality or quantity do we Tz need kwa sasa? It is a fact Tz ktk machapisho ya kisayansi tuko juu zaidi ya Kenya na Ug.

Is this what in Tz we need?
 
Last edited:

Hey, punguza jazba na usome vizuri michango inayotolewa.

Hakuna aliyekataa umuhimu wa elimu, kinachojadiliwa hapa ni utaratibu unaofaa kutumika katika kulipia gharama ya elimu ya juu. Swali la msingi ni je, wanafunzi wote wapewe asilimia 100 ya mahitaji yao bila kujali uwezo walio nao wa kujigharimia?

Na hakuna mahali nilipowakataza wanafunzi kuomba asilimia 100, ila kinachonishangaza ni tabia yao ya kukataa kuingia darasani mpaka wapewe hizo asilimia 100. Kilichofanya nianzishe hii thread ni pale walipoenda mbali na kutishia kuwa iwapo hawatatekelezewa wanachotaka basi ''...Tanzania haitakalika''.

Asilimia 100 ya mahitaji ya wanafunzi wote wa kitanzania wanaosoma elimu ya juu ni sh. billioni 1200 kwa mwaka.bajeti ya wizara ya elimu ni sh.billion 1080. pesa wanazotaka wanafunzi ni zaidi ya asilimia 18 ya bajeti ya nchi kwa mwaka.Je, ni sahihi kwa vijana hawak usema hawataingia darasani mpaka wapewe zaidi ya asilimia 18 ya bajeti ya nchi nzima?

Wanafunzi wa mlimani wakitaka wana haki ya kuomba hata asilimia 100 ya bajeti ya nchi, lakini kusema kuwa wasipotekelezewa matakwa yao basi ''..Tanzania haitakalika'' sio jambo la kuungwa mkono na wanaoitakia nchi yetu mema.
 
ZeMarcopolo kwa hiyo unakubali part time bongo ngumu??
Na hoja ya tuition hayana msingi wowote?
Suggestion yako ni ipi kwa wanafunzi wasiokuwa na ada na hela ya matumizi??
 
Quote:
"..nimechukulia madai yako kwamba kwasababu waalimu wetu wa UDSM wana-publish kuliko wenzao walioko Kenya, basi tunapaswa ku-conclude kwamba UDSM ina waalimu bora/vipanga kuliko wenzetu wa Kenya. sasa kwanini graduates wa UDSM wanafanya vibaya in the job market wanaposhindanishwa na wenzao wa Kenya ambao wamefundishwa na waalimu vilaza?

..nadhani vyuo vyetu vya elimu ya juu vinapaswa kujichunguza kuanzia mitaala yake, mbinu za ufundishaji, upatikanaji wa vifaa etc etc. inaelekea kwamba quality ya graduates wetu imeshuka as it is evidenced in the job market kulinganisha na ya washindani wetu toka nchi jirani."


Mkuu, mimi siamini wakenya kutupiga bao kwenye job market maanayake ni kuwa wakenya wako better trained au wana better skills kuliko graduates wetu.

Sababu kuu ni kuwa wenzetu wamekuzwa kwenye Capitalist mentality, ya "you have to sell yourself", wakati watanzania tuna ile tabia ya kuogopa kujiuza kwa kuogopa kuonekana arrogant au mpenda sifa(wengine husema kujishaua).... Multinational recruiting companies wamejifunza hii the hard way pale walipokua wanaona U.S graduates always did much better kwenye interviews kuliko Far east groomed graduates, hata kama academically vyeti vya wachina/wajapan walionekana more superior candidates. Sababu ni culture yao haiwafanyi wajikuzekuze kama americans ingawa ni very competent. Pale walipopewa nafasi walikua wanaperform kwelikweli. Na sasa hivi haya makampuni yameshastukia janja ya graduates wamarekani na wameweka different standards za kuwa asses wale wa far east.

Tukirudi kwetu, bado waajiri wengi(hasa wageni) wanaendekeza kasumba ya fluency ya language ya kiingereza na sio actual technical know how. Halafu Kuna hali ya kuona ukimuweka mkenya au foreigner kwenye kampuni yako, itaonekana more sophisticated.Na hii inatokana vilevile na attitudes za maofisa uajiri watanzania "kubabaika".

Trust me, nimefanya kazi na wakenya na waganda kwa miaka kadhaa siku za nyuma. HAWANA anything cha ajabu kulinganisha na graduates wetu, tena wengine ni watu wa kufojifoji na plagiarism kwelikweli when it comes to developing written materials. Lakini utakuta ndio boss!!!... My foot.

Recently nimetokea kuwa kwenye interviewing panels mbalimbali. Ha huko ndio nilipokuja kuamini kuwa watanzania tuna tatizo la kujisell. Kijana competent lakini hasemi kitu anachokijua mpaka umchokonoe sana, mpaka inaboa. Sasa mtu kama huyu akipambanishwa na mtu aliye rehearse jinsi ya "kujiuza" all night. Obviously utamuona mkenya anafaa, lakini sio kwenye actual ujuzi. Halafu akimask na fluent english hapo ndio kabisaaa wabongo tunamuabudu.

Interview za bongo nyingi haziko sophisticated enough kuchanganua pumba na mchele...utakuta position kubwa, lakini interview ya maana moja au mbili ambazo zote zinafanana in content...tell us about yourself, what do you bring, your biggest challenge so far...Just shitty stuff zinazompa advantage mtu wa rhetoric zaidi.

The rest nakubaliana nawewe kuwa in general tuko nyuma sana katika idadi ya graduates.
 
ZeMarcopolo kwa hiyo unakubali part time bongo ngumu??
Na hoja ya tuition hayana msingi wowote?
Suggestion yako ni ipi kwa wanafunzi wasiokuwa na ada na hela ya matumizi??

Ni kweli kuwa part time kwa wanafunzi wa chuo kikuu ni ngumu kupata. Lakini kuwa ngumu haimaanishi kuwa haiwezekani! Hivi unadhani Marekani ni rahisi kufanya kazi huku unasoma? Wapi duniani ni rahisi kufanya kazi na kusoma. Kwa nini mnataka taifa letu liwe lenye kufuata mteremko tu? Hivi Columbus angekuwa anakimbia mambo magumu angeweza kufika Marekani?

Hoja ya tuition haiwezi kukosa msingi. Kufundisha tuition ni mojawapo ya njia nyingi ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kujiajiri. Swala la tuition ni mfano tu, sasa msiamue kuchukulia kuwa tuition ndio njia pekee. Ukisoma vuzuri mjadala utakuta mahala ambapo nimetoa mifano kadhaa ya vitu anavyoweza kufanya mwanafunzi wa chup kikuu ili aweze kujipatia kipato. Na ni muhimu wanafunzi wa chuo wakaelewa kuwa kazi watakazofanya hazitawaingizia pesa nyingi, lakini zitawawezesha kuimprove uwezo wao wa kujitegemea.

Ushauri gani mwingine unaoutaka kwa mwanafunzi asiyejiweza?? Kuwepo kwa wasiojiweza ndio sababu ya kuwepo kwa utaratibu wa mikopo.
 

Kwa mtindo huu, tukikupeleka muhimbili casuality utakaa masaa mawili tu then utaanza harakati za kutaka serikali ilipie asilimia 100 ya gharama za matibabu ya wagonjwa wote!! Hivi unadhani wanafunzi kama hao Marekani hawapo? Unadhani kwa nini wanafunzi wa Marekani hawasemi nchi yao haitakalika iwapo hawatapewa mahitaji yao kwa asilimia 100?

Nyinyi UDASA hicho chuo mnakiharibu kwa ajili ya siasa mnazokumbatia.
 

Asante mkuu, bado hujanijibu umesoma chuo gani Tz?? ni mara ya nne sasa nauliza , maana unaonekana umemaliza form six, tell me where, when, then from there. unieleze kama unalipa deni, na wanakukata sh. ngapi?
 
Hoja ya tuition haiwezi kukosa msingi. Kufundisha tuition ni mojawapo ya njia nyingi ambazo mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kujiajiri. Swala la tuition ni mfano tu, sasa msiamue kuchukulia kuwa tuition ndio njia pekee.
MKuu umeshaambiwa tuition haifai na haiwezekani unless uchague moja ule discontinue au uache kufundisha hizo tuition.....FYI mimi mfano nimemaliza KLF nitafundisha nini tuition kijana?? jua kwamba tuition zenye wanafunzi wengi ni zile za masomo ya sayansi.....
Mkuu usiteteee tu kwa kuwa unakula "mayai na sambusa" majuu hujui kinachotokea.....
Asante mkuu, bado hujanijibu umesoma chuo gani Tz?? ni mara ya nne sasa nauliza , maana unaonekana umemaliza form six, tell me where, when, then from there. unieleze kama unalipa deni, na wanakukata sh. ngapi?
The dude hajasoma chuo chochote tz..anapata hizi hadithi potofu kwa marafiki zake ambao naweza kuwaita mafisadi(sorry).....
Mtu yoyote aliewahi kusoma tz anajua tunachokiongelea....... sasa hivi suala la kutembea Mabibo to main kampasi ni kitu cha kawaida....
MKuu waberoya unajua kuna mambo ambayo watu wengine hawajui kinachoondelea wakisikia toka mjengoni Dodoma wanajua shwaaari
 
Unadhani kwa nini wanafunzi wa Marekani hawasemi nchi yao haitakalika iwapo hawatapewa mahitaji yao kwa asilimia 100?
Mkuu lol! again unafananisha system ya ma USA na Bongo.....nikuulize kinachooombwa naw anafunzi nini?? ni mkopo au ufadhili?
Na hao wa majuu wanapata nini mkopo au wanakosa?....

Mkuu unafanisha system ya loan ya US na Bongo??
 
Elimu ya Tanzania bado ni mgogoro. Haihitaji majibu ya haraka haraka kama ya ndugu yangu Zemarcopolo.

Unajua kama uliwahi kupita pale mlimani ni rahisi kulielewa hili.

Vyuo vyetu bongo (most of them) especailly UD vinaendeshwa kisiasa zaidi. Hata kama mtu alikuwa competent namna gani..akishaingia pale inabidi aface reality check ya kisiasa. Kwa sababu wanasiasa ndo wanatoa pesa. Na wanafunza wameshazoa (tangu enzi hizooo...) kwamba bila confrotation haki haipatikani.

Yes, I agree Tanzania haiwezi kugharimia wanafunzi wote forever. Lazima kipindi kifike watu wachangie elimu yao maana kama wazungu wasemavyo..education is an investment ambayo mtu inabidi atake personal responsibility. Lakini vile vile tunahitaji mkakati wa kujua nani anahitaji msaada. Hii bodi ya mkopo ina longo longo nyingi. Haina water tight criteria za kujua nani ni maskini na nani si maskini. They are LYING! (Sorry for the negative vedict)

I would suggest this:

1. Serikali itoe scholarship on merit. Period. In otherwords kama serikali inauwezo wa kuwasomesha/kuchangia gharama za wanafunzi elfu tatu..basi waangalie nani kafaulu..na huyo ndo asaidiwe. Just kama tunavyoingia university..kama Una dvision one..then una uhakika..kama mko wengi wenye one..basi wanangalia points. Ukiwa na Three..basi inabidi uanze kuitafuta Butimba au Marangu iko wapi... This is the only FAIR way ya kuepusha malalamiko. Hili neno "watoto wa masikini" Liko so vague...you cant easily define it. Precisely because kwa Tanzania yetu...ambapo millions hawajulikani wanafanya nini...zaidi ya kuwa lumped together under the umbrella ya "peasants" basi kigezo sahihi kiwe elimu na cheti cha mtu. Otherwise hii ya kwapa wengine 100%, wengine 20% nk..lazima ilete migogoro na malalamiko mengi sana.

Swala la elimu ya juu halihitaji siasa. This is our future. Watu tuache utani jamani! Hivi mnajua kwamba tuko almost 40 millions heads in this country? na bado watu mnaliongelea hili swala kwa ushabiki?

We can do better as a nation.

Masanja,
 

Sober,

..majibu yako yamenipa moyo kidogo.

..naamini there is room for improvement ktk utoaji wa elimu kwa watanzania.
 

Kweli mkuu atueleze, maana aacha stori za vijiweni. Akinieleza nitamuuliza tena ametoka kijiji gani maana yeye si mzaramo, halafu anieleze hicho kijiji ni wanagapi wamefika chuo, akimaliza hapo anieleze pia hali za watu wa kule kama wanaweza kulipa ada za watoto wao.

Tanzania si ya kufananisha na USA, ila tunatakiwa tuwaige wenzetu toka hatua zao za mwanzo za elimu na si kudesa au kugeza kwa USA ya sasa!, au Kenya ya sasa, wenzetu walipitia hatua mbalimbali, sisi tunakurupuka kuwaiga, na bila aibu tunatoa mifano mbona nchi fulani wanafanya hivi!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…