AndrewMwanga
Member
- Jan 9, 2009
- 37
- 1
hapana mkuu ni baada ya FORM SIX nadhani mkuu mmoja amesema uzalendo na kujitegema kwa taifa letu NI VYEMA UKAanzie kwenye familia, nakubaliana nae kabisa.
AM
AM
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ibrah, DARUSO imefutwa. Haipo tena. Wataaam wa sheria wanasema walioifua hawana mamlaka ya kuifuta, sasa tungoje kuona nini kitafuata baada ya wanafunzi kurudi ila kwa hali ya sasa hakuna any legal body inayoitwa DARUSO.
Kuwasupport wanafunzi wa prive universities ni jambo ambalo kwa sasa haliepukiki. Sababu ni kwamba public universities ni chache mno kuweza kukidhi mahitaji, jambo ambalo linapelekea wanafunzi waliofaulu kukosa nafasi kwenye public universities. Kwa mfano chuo cha udaktari cha seriksli nchini ni kimoja tu! lakini vipo vingine vinne privete, mwanafunzi aliyepata division one anaweza kukosa nafasi muhimbili lakini akapata nafasi IMTU, sasa iwapo serikali itaacha kumuwezesha huyu wa IMTU na kuassume kuwa amechoose luxury itakuwa haifanyi jambo sahihi. Kusoma private niversity Tanzania sio luxury kama ilivyo katika nchi zilizoendelea ambapo ''matajiri'' huamua kuwapeleka watoto wao kwenye shule za private ili kuwapatia special privilage.Hivyo basi uamuzi wa kuwawezesha wanafunzi wa private universities ni uamuzi sahihi na mpaka sasa umeshawezesha kwa kiwango kikubwa kuongeza idadi ya graduates nchini Tanzania.
hebu tuchambue hoja yenyewe wala tusinganganie kukosoana! unajua kama vita unaisikia kwenye vyombo vya habari huwezi kuona kama ni kitu chenye madhara sana ni kama hakikuhusu nadhani hizi asilimia 40% za uchangiaji zitakapo ugusa mfuko wako ndio utaelewa machibya na wengine wanaomuunga mkono kwenye hoja 100% wanamaanisha nini! Tanzania hii sio masikini sana kama tunavyodhani bali ni vision za viongozi wetu na mambo gani kuyapa vipaumbele( priorities) ndio shida kubwa inayotutesa!
Ukweli ni kwamba hata yule anayeendesha range rover vogue angependa serikali iwe inamuwekea mafuta kwenye gari kwa asilimia 100. Cha msingi ni je hawa wanaotaka hizo asilimia 100 kuanzia wanafunzi, wafanya biashara mpaka wakulima na jobless wanaweza kutekelezewa matakwa hayo na serikali. Msilazwe na usingizi mkadhani kuwa wanaotamani kuhudumiwa asilimia 100 na serikali ni wanafunzi wa chuo kikuu peke yao. Huu ni mwanzo tu wa tabia ambayo ikiendekezwa itazagaa kama ukoma nchi nzima. Siku moja mtasikia wanajeshi nao wanataka watimiziwe mahitaji yao kwa asilimia 100, na lugha zenyewe kama ndio hizi kuwa wasipotimiziwa Tanzania haikaliki basi tujiandae na mabaya huko mbele. Tabia hii inapaswa kukemewa, huu sio muda wa mambo ya kitoto. Mtoto ndio akitaka kitu analia mpaka apewe vilevile anavyotaka bila conditions.
Mkuu hujajibu swali langu, nimeuliza shilingi ngapi inahitajika ili kuwapa wanafunzi loan ya asilimia 100?? naomba jibu mkuuu!!!, hii post uliyokopi imekuja baada ya kupost mimi, nahitaji msaada wako tafadhali mkuu!
NItapata raha kujua kiasi gani ili niweze kuachangia kwa ufahamu wangu mdogo.
waberoya
Swali lako halina jibu la moja kwa moja kwa sababu haliko specific. Kiasi cha pesa kinachohitajika kinabadilika kwa kasi sana kiasi kwamba hakiwezi kukadirika. Kwa mfano chuo Tumaini kilikuwa na wanafunzi mia mbili miaka 11 iliyopita na sasa kina wanafunzi elfu 8. hivyo basi kutoka sh. 600 milioni walizukuwa wanahitaji miaka 11 iliyopita sasa hivi wanahitaji mara 40 zaidi ambazo ni sh. bilioni 24 (hii ni kama thamani ya pesa imebaki ileile kwa miaka 11). Hiyo ni hesabu ya wanafunzi wa Tumaini. Kuna vyuo vingi,na kuna wanafunzi wanaosoma nje ya nchi. Idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama nilivyosema inabadilika kwa kasi kubwa.Tutarajie baada ya miaka miwili Tumaini watakuwa na wanafunzi elfu Kumi! UDSM kuna wanafunzi elfu 21
Hivyo basi kwa kukadiria tu, wanafunzi wote kuanzia Tumaini,IMTU, SAUT, SUA, UDSM, Ardhi University, MUHAS, Kairuki, Dodoma, Chuo kikuu Huria, CBE, AIA, MUM,Exchange Programme wa Uganda, Algeria, China, Ukraine,Urusi etc. wanahitaji kama bilioni 1200 ili kuwakamilishia mahitaji yao kwa asilimia 100 kwa mwaka mmoja.
Bajeti ya nchi ya mwaka 2007/2008 ni sh. Trilion 6(bilion 6000). Wizara elimu imepewa kipaumbele kwa kupata asilimia 18 ya bajeti ambayo ni sh. trilion 1.08(bilioni 1080).Wanafunzi wanagoma wakitak wa[ewe bilioni 1200 ambazo zimezidi bajeti nzima ya wizara. Hivi kweli tunakuwa reasonable tunapowaunga mkono wanafunzi hawa. Hata kama bajeti nzima ya wizara ingetumika kulipia ada za wanafunzi wa chuo kikuu bado isingetosha, wakati huohuo bajeti hiyohiyo inategemewa kuhudumia elimu ya msingi, sekondari ,vyuo mbalimbali na kulipa mishahara ya watumishi wote kuanzia mlinziwa shule mpaka waziri.
ZeMarcopolo katumia mahesabu yasiyo sahihi. Takwimu za fedha wanazopashwa kulipa wanafunzi zinapatikana hapa:
http://www.udsm.ac.tz/admission/bachelors2008_2009/RevisedTuitionFees2008_09.pdf
Utaona toka hizo takwimu kwamba mwanafunzi Mtanzania anatakiwa kulipa jumala ya sh 2.479 million.
Tunazungumzia malipo katika vyuo vya umma, vya Tanzania. Hatuzungumzii malipo kwenye vyuo binafsi. Na ugomvi ulioko sasa ni kuhusu hii milioni mbili na nusu.
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma Tanzania ni kiasi cha 30,000. Ili kuwalipia wote kwa 100%, zinahitajika shilingi 74.37 billion only. Hizi ni robo ya fedha zinazokusanywa na TRA kwa mwezi!
==================================================
Nabandika kwa wasiwasi kwani Moderator ameshafuta posting yangu nyingine leo. Sijui kama na hii atafuta!
ZeMarcopolo katumia mahesabu yasiyo sahihi. Takwimu za fedha wanazopashwa kulipa wanafunzi zinapatikana hapa:
http://www.udsm.ac.tz/admission/bachelors2008_2009/RevisedTuitionFees2008_09.pdf
Utaona toka hizo takwimu kwamba mwanafunzi Mtanzania anatakiwa kulipa jumala ya sh 2.479 million.
Tunazungumzia malipo katika vyuo vya umma, vya Tanzania. Hatuzungumzii malipo kwenye vyuo binafsi. Na ugomvi ulioko sasa ni kuhusu hii milioni mbili na nusu.
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma Tanzania ni kiasi cha 30,000. Ili kuwalipia wote kwa 100%, zinahitajika shilingi 74.37 billion only. Hizi ni robo ya fedha zinazokusanywa na TRA kwa mwezi!
==================================================
Nabandika kwa wasiwasi kwani Moderator ameshafuta posting yangu nyingine leo. Sijui kama na hii atafuta!
Halafu unapotumia estimates za ada ya UDSM kujua ada ya wanafunzi wa Tanzania unakosea sana. Ada ya mwanafunzi wa udaktari sio 2.7 mili. Na ada ya private universities haiwezi kuwa sawa na ya UDSM, kwa sababu vyuo hivi unlike UDSM vinaendeshwa kwa ada za wanafunzi. Ili kulipa mishahara ya wafanyakazi, bili mbalimbali na kununua vifaa vya kufundishia, ada ya vyuop hivi inakuwa kubwa zaidi ya UDSM. Hivyo estimates kwamba mwanafunzi mmoja anahitaji 2.7 mil, kwa kigezo kuwa hiyo ndio inayohitajika UDSM, ni lame.
ZeMarcopolo,
Unaposema gharama ni zaidi ya mil 2.7 kwa mwanafunzi na hivyo serikali haiwezi una maana gani? Kama serikali haiwezi je wakulima wataweza?
Lengo mojawapo la serikali kukusanya kodi ni kujaribu kugawanya kipato kutoka kwa mwenyenacho kwenda kwa asiyenacho kupitia huduma za kijamii kama elimu.
Hivi unaamini kwa dhati kabisa elimu ni mojawapo kati ya vipaumbele vya serikali yetu? Binafsi naamini tuna tatizo kubwa katika kuweka vipaumbele na kukosa viongozi makini na wenye uzalendo na nchi yao.
Kwa nchi changa kama Tanzania Elimu haipaswi kuwa previlege bali nyenzo ya maendeleo. Elimu ambayo nimeipata haininufaishi peke yangu bali nalitumikia Taifa kwa manufaa ya wote. Hivyo si dhambi kwa serikali kubana matumizi mengine na kuwekeza zaidi kwenye elimu. Na hapa hatuzungumzii kusomesha bure (ingawa hili pia linawezekana) bali kukopesha kwa asilimia mia moja. Nguvu zao waweke kwenye kukusanya madeni naamini watafanikiwa.