''...Tanzania haitakalika''

''...Tanzania haitakalika''

Wakati mwingine nikweli serikali inakosea kwa kuwa ni wajibu wake kuwasomesha watanzania bure ili kuinua kiwango cha elimu nchini. Lakini pia wanafunzi na wazazi wanatakiwa kujua kuwa wanatakiwa kuchangia elimu ili kuwapa responsibility na machungu ya kupata pesa ya elimu.

Nje ya nchi watanzania wanabeba box na kujisomesha wenyewe kuanzia UG mpaka PG au hawa sio watanzania ambao wanafaamu umuhimu wa elimu na kuamua kujisomesha wenyewe, ili linawezekana hata kwetu kwani swala ni kujituma. Nina uhakika kwetu hata kama mishahara itaongezwa kiasi gani hakuna mwanafunzi atakayekubali kufanya kazi kujilipia ada.

Tunatakiwa kuangalia nani anapata side effect ya migomo wakati watoto wa wakubwa wakiwa nchi za nje wanasoma kwa raha wanafunzi mlimani wanagoma na kufukuzwa bila huruma na kuongeza matatizo kwa wazazi wao.

tufanye financial analysis ya gharama ya kufukuzwa chuoni in terms of money utakuta inalingana na pesa wanayotakiwa kulipa kama 40% na hii gharama wamelipa bila hata kulalamika lakini hiyo 40% ndio wanalalamika na ukiongeza time costs utakuta mwanafunzi hata kama amerudishwa yeye ndio amekula hasara zaidi.

watoto wa wakulima wengi hawana pa kukaa dar walipofukuzwa either walirudi nyumbani au walikaa kwa ndugu tuone wataramu wa pesa wanaweza kutusaidia simple estimates za gharama walizoingia kurudi kwao au kukaa kwa ndugu zao.

all in all serikali ina wajibu wa kusomesha watu wake lakini sometimes tusijitoe sadaka kwa vitu ambavyo tunajua kweli kuwa hatutapata support kutoka kwa watanzania wengine. sasa hivi watanzania wanafocus kwenye kuondoa ufisadi kuliko kitu kingine chochote.
 
....Criteria ya kutoa udhamini kwa mwanafunzi dunia nzima ni moja tu, kufaulu vizuri! Serikali itoe mikopo na udhamini kwa wanafunzi waliofaulu vizuri bila kujali mtoto wa mkulima au wa tajiri.
...
Serikali isomeshe wanafunzi kwa 100% kwa kuzingati viwango vyao vya kufaulu mpaka pale uwezo wake unapoishia!

Hapa tupo ukurasa mmoja mkuu! Mara nyingi nimekuwa nikisikiliza kipindi cha "Je, tutafika?" kinachorushwa hewani na kituo kimoja cha runinga. Huwa napenda sana kumsikiliza Dr. Azaveli Feza Lwaitama (iwapo amealikwa kwenye panel). Siku zote anapotoa maoni yake kuhusu jukumu la serikali katika elimu, huwa anasisitiza elimu iwe lazima katika shule za msingi na sekondari, na elimu ya Juu iwe kwa wachache ambao serikali itamudu kuwasomesha hata kama ni kwa mkopo, lakini iwe kwa 100%.
 
Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly.

Kama umekuwa ukifuatilia mijadala yao (bodi ya mikopo na wanafunzi) kwa makini na kuwaelewa wanachosema ni kwamba "maskini wasaidiwe na matajiri wajilipie kulingana na hali yao". Hapo ni sawa kabisa.

Lakini wanafunzi wanachosema ni kwamba njia inayotumika kujua nani hana uwezo na nani ana uwezo iko 'flawed' na hivyo inasababisha baadhi ya watoto wa vigogo kusoma hiyo mikopo na wale wa wazazi wasio na uwezo kukosa na wakati huohuo serikali inadhani mambo yanaenda vizuri kabisa. Hili linawauma sana!

Ndiyo maana wanafunzi wa UDSM wanashauri kama ni hivyo ni bora serikali iwakopeshe wanafunzi wote - wenye uwezo na wasio na uwezo - kwa asilimia 100 kwa vile baadaye wanapaswa wazirudishe (na siyo bure kwa maana kwamba hawatazirudisha) kwani serikali inao uwezo wa kufanya hivyo.

Hii inatokana na ukweli kwamba baadhi ya wale wanaopata hiyo mikopo siyo wale wanaohitaji. Ndiyo maana wanakazania sera ya mikopo ifanyiwe marekebisho kwa vile haitimizi lengo lake.

Hata mimi naunga mkono kwa maana kwamba - "If the theory doesn't fit the practice ignore the theory".

Kwa bahati mbaya kila wanafunzi wakitoa hoja zao tunashindwa kuelewa wanachokisema ni nini. Tunabaki tu kupotosha wanayosema na kuweka siasa kwa namna inayotupendeza. Lakini hatuoni kuwa tunaendelea kuharibu taifa letu sisi wenyewe.

Solution ya UDSM siyo FFU wenye silaha. Huu ni ubabe tu kuonyesha "Might is right". Lakini siyo njia ya kupata suluhisho la migomo vyuo vikuu. Suluhisho ni kusikiliza na kujadili kwa pamoja nini kifanyike. Baadhi ya mawazo ya wanafunzi yanaweza kusaidia sana katika kutatua matatizo yanayojitokeza pale mlimani na siyo tu wanafunzi kulazimishwa kufyata mkia.
 
Kama umekuwa ukifuatilia mijadala yao (bodi ya mikopo na wanafunzi) kwa makini na kuwaelewa wanachosema ni kwamba "maskini wasaidiwe na matajiri wajilipie kulingana na hali yao". Hapo ni sawa kabisa.

Lakini wanafunzi wanachosema ni kwamba njia inayotumika kujua nani hana uwezo na nani ana uwezo iko 'flawed' na hivyo inasababisha baadhi ya watoto wa vigogo kusoma hiyo mikopo na wale wa wazazi wasio na uwezo kukosa na wakati huohuo serikali inadhani mambo yanaenda vizuri kabisa. Hili linawauma sana!

Kwa bahati mbaya kila wanafunzi wakitoa hoja zao tunashindwa kuelewa wanachokisema ni nini. Tunabaki tu kupotosha wanayosema na kuweka siasa kwa namna inayotupendeza. Lakini hatuoni kuwa tunaendelea kuharibu taifa letu sisi wenyewe.

Mkuu, iwapo wanafunzi wangekuwa na hata nusu ya uwezo wako kujielezea, hili suala wala lisingekuwa gumu. Mtu akisoma bandiko lako anapata mwanga zaidi kuliko vitisho vinavyotolewa na hao Daruso (au labda vyombo vya habari-ambavyo wengi ndimo tunapata taarifa, vinachagua cha kuandika).
Hoja unayoieleza hapa, kwamba mfumo upo flawed inaeleweka sana lakini hilo halihalalishi kuwa kila mwanafunzi apatiwe 100% loan.
Kama mfumo uko flawed, solution ni nu kufanya revision. Lakini kikubwa ambacho kinasikika kutoka kwa wanafunzi ni kutaka loan kwa asilimia zote. hatutafika kwa mtindo huo
 
Mpita Njia,
Wanasiasa siku zote hubadili maneno ili kuidhnisha wanayotaka. Ulivyosikia kuwa wanataka wote wapewe mikopo, ilikupitia akilini au swali kwa nini wanataka iwe hivyo? Ndiyo maana Zemarco akasema kuwa wanaji-contradict. Ni kweli unaweza kuona hivyo kwani kuna habari HUPEWI ili uwaone hawa DARUSO kuwa ni VIBWENGE fulani.
Nilitoa mfano wa NYERERE aliposema kuwa wanamshambulia kuwa anachagua mawaziri WAKATOLIKI tu, ingawa watu walisema anachagua WAKRISTO tu. Asingelisema Wakristo tu kwani ingelikuwa kweli. Akaligeuza na kusema Wakatoliki wenzake. Hawa ndiyo wanasiasa..........
Kama Msomi, usimeze tu, jaribu kutafuna maana hapo unaweza kugundua wali unamchanga na ukautema, vinginevyo subiri uuguwe APPENDIX.
 
Hii mikopo ya elimu ya juu imeanza kutolewa tangu 1994(kama sijakosea)... Serikali ituambie mpaka 2008 imeshatoa mikopo kwa watu wangapi, wangapi wamehitimu, na kiasi gani cha hiyo mikopo kimeshalipwa kwa ajili ya vizazi vinavyofuata.

Tatizo watanzania hatuna utamaduni wa kulipa mikopo, in other words hii mikopo ni kama scholarships kwa majority ya wanayoipata. Bila kukusanya madeni kwa waliokopa siku za nyuma... huu "mradi wa mikopo" hauwezi kuwa sustainable. Na matatizo ya migomo yatakuwepo kila mara. Ukiona rationing ya nani apewe na nani asipewe basi ujuwe chungu cha fedha hakitoshi kwa wote. What if kingetosha, hii rationing ingekuwepo?

Napendekeza sisi wakubwa tuliomaliza kusomeshwa kwa mikopo tuanze initiative ya kulipa mikopo yetu ya elimu yote ili vijana wetu wa sasa nao wanufaike badala ya kulalamikia kila siku serikali as if serikali ina exist in space. Sisi wananchi ndio serikali yenyewe.
 
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine

Tungekuwa na uhuru tungesilizwa
Tungekuwa na upendo tungehurumiana
Tungetaka amani tungewalinda Watanzania wetu

lakini watu wengine wana uhuru wa kufanya watakalo hakuna wa kuwauliza
wanaupendo na familia yao tu hawajali jirani zao maskini
Hwana imani na wenzao,,,,,, kwa nini?

Waachwe Watanzania waseme,,,, ndo uhuru wao wa kusema hata kama hawatasikiliza. Lakini ukweli kama wewe ni wa Maskini wafa,,,, huna lako.
Hatutaki kusema tu,,,, hata wengi walio kwenye top position wameshikwa mkono na fulani,,,,,,Nisieleweke vibaya sijasema wote ila wengi
Watanzania tutumie uhuru wetu wa kuongea,,,, ujumbe utafika tu!
 
Sera ya nchi ni kwamba masikini watasaidiwa kwa kupewa asilimia ya mkopo wanayohitaji na tajiri atajilipia mwenyewe. Hiki ndio wanachokipinga hawa wanafunzi kwa madai kwamba watanzania wote ni maskini hivyo wote wapewe asilimia 100 ya mkopo. sasa anaposema wanaorudishwa ni matajiri anajichanganya mwenyewe, kama anajua kuna matajiri kwa nini aliongoza mgomo wa kutaka wanafunzi wote wapewe mkopo asilimi 100%? Hiyo maana ulizoweka hapo ni yako wewe, angetaka ieleweke hivyo angeelezea explicitly.

hiyo sera ni mbvovu kani kama kweli wangekuwa wanawalipia maskini wote, na matajiri wanajilipia basoi kusingekuwa na mtoto wa kufukuzwa chuo. Kama kweli lengo lake ni kuhakikisha kuwa watoto wa watanzania wote wanapata elimu kadri ya uwezo wao, basi kuwepo kwa wanachuo wanaoufukuzwa chuo kwa ajili ya kushindwa kulipa ni dalili kuwa sera hiyo ina walakini.
 
Kwanza tujikumbushe kabla ya board ya mikopo mambo yalikuwaje?. Kimsingi itakumbukwa kabla ya kuanzishwa board ya mikopo mkombozi wa mtoto wa mkulima kwenda shule 'elimu ya juu' ilikuwa nikuhakikisha anafauru vizuri hivyo kujihakikishia udhamini wa serikari (under shadow loan system).

Uanzishwaji wa Board ya mikopo ilikuwa ni kitu chema japo niukweli hakukuwa na mikakati endelevu kuhakikisha smooth running ya board hii kwa kuzingatia mahitaji. Tukisamehe political decision 'si mtoto wa tajiri wala wamasikini wote watasoma kwa mkopo' pamoja na ufisadi unaoendelea kuleta mkanganyiko juu ya swala la mikopo elimu ya juu, nivema tukatambua kuwa uwezo wa nchi yetu bado haujustify 100% loans higher education. Hivyo swala la uchangiaji elimu nchini kwetu haliepukiki. The country needs to be modeled to the exitent of being certan to recoup its funds from debtors as well as narrowing non tax compliance before it can be able to issue 100% loans.

Kauli ya kwamba watanzania wote ni masikini vile vile si ya kiungwana kwani is obvious GIN coeficient ya nchi yetu inabehave kama nchi za kipepari, yaani gap kati ya walionacho na wasionacho nikubwa sana na linakuwa kwa kasi. Hivyo ni ukweli kuwa kunafamilia za kitajiri na familia za kimasikini
Tanzania. Mfano kuna watoto hapo Bongo wanasoma Primary ada Milion we know. Shida hapa ni namna yakumtambua masikini na mwenyenacho katika mazingira yaliyoshiba rushwa hilo ndio tatizo kwangu. Hivyo nawashauri urgument zilenge huko maana at the end of the day pamoja na makosa ya serikari ambayo tunayajua wote mwathilika namba 1 ni mwanafunzi husika na familia yake..

Hivyo tutumie nguvu kidogo kama itahitajika lakini umakini zaidi nimuhimu katika swala hili ''is so technical and very political''
 
Wakati USA, leo hii Obama anakuwa mtu atakayeifanya NDOTO ya Dr. King kuwa kweli na hivyo kuimaliza hizo ndoto, Tanzania tumeanzia kwa Obama na kwenda nyuma kwenye wenye nazo na wasio nazo. Matabaka yanazidi kutanda. Wengine wanafikiri matabaka kila sehemu yapo na Tanzania lazima yawepo. Ni kweli ila details ndiyo zinaleta shida siku zote. Wanasema "Demokrasia ni udikteta kwa walio wachache".
Nchi zilizoendelea, matajiri na watu wa hali ya kati ni wengi kuliko masikini. Tanzania ni kinyume chake. Hii inapeleka kuwa na Watusi (10%) kuwatawala Wahutu (90%). Amini usiamini, siku moja mapanga yatatembea. Na wala hutajua yalianza-anzaje. Ila kama masikini ni 10%, hawawezi kutembeza mapanga kwa watu 90%.
Haihitaji kuwa na akili sana au msomi sana ili kuelewa maneno ya kijana. Kama ni kijijini basi utasifiwa kuwa na wewe ni NABII kwani ulijua mapema kuwa hili litatokea. Ikumbukwe kuwa sisi hatupishani sana na Wakenya. Utalaani vyama vya upinzani weee lakini Mkenge umeutaka mwenyewe kuukalia.

Huyokijana kama angetabiri huo utabiri wake kwa kigezo cha wafanyakazi dhidi ya waajiri, wakulima dhidi ya serikali, chama tawala dhidi ya wapinzani, matajiri dhidi ya masikini basi hayo unayoyasema yangeleta maana lakini kuwa Tanzania isikalike kwa kikundi cha wanafunzi ambao nao wako katika harakati za kukwea kwenye tabaka la walionacho nafikiri Watanzania tuna akili ya kuchaguwa zuri na baya.
 
Yes, serikali uwezo wake mdogo sana.
Mashangingi ya bei mbaya 700 kwa mwaka mmoja. Kukodisha ndege mbovu za ATCL, zilizopelekwa Kiwira kimya kimya, za safari, za vikao, washa, seminar, kongamano................ Kweli serikali uwezo wake mdogo, AMEN!!

Tujue kuwa serikali si kijiwe bali serikali ina dhamana kwa nyanja zote na tunalazimika kugawa tulichonacho katika nyaja hizo na ndio maana mashangingi yananunuliwa ili miongoni mwa hao wanaosoma sasa watakapoingia serikalini wayatumie. Warsha na semina pia wanaonufaika nazo ni haohao wanaotoka vyuoni . Fedha inazalishwa na mkulima lakini mkulima hanufaiki nayo lakini tunaziba midomo tunaposikia unyanyashaji wa wakulima. Serikali ni yetu na ni sisi wenyewe tunaotowa ubavu kwa viongozi watuchagulie namna ya kutumia fedha zetu. Hebu natuwatetee wakulima na sio hawa wanaogombania kupanda daraja la watawala.
 
Kwanza tujikumbushe kabla ya board ya mikopo mambo yalikuwaje?. Kimsingi itakumbukwa kabla ya kuanzishwa board ya mikopo mkombozi wa mtoto wa mkulima kwenda shule 'elimu ya juu' ilikuwa nikuhakikisha anafauru vizuri hivyo kujihakikishia udhamini wa serikari (under shadow loan system).

Uanzishwaji wa Board ya mikopo ilikuwa ni kitu chema japo niukweli hakukuwa na mikakati endelevu kuhakikisha smooth running ya board hii kwa kuzingatia mahitaji. Tukisamehe political decision 'si mtoto wa tajiri wala wamasikini wote watasoma kwa mkopo' pamoja na ufisadi unaoendelea kuleta mkanganyiko juu ya swala la mikopo elimu ya juu, nivema tukatambua kuwa uwezo wa nchi yetu bado haujustify 100% loans higher education. Hivyo swala la uchangiaji elimu nchini kwetu haliepukiki. The country needs to be modeled to the exitent of being certan to recoup its funds from debtors as well as narrowing non tax compliance before it can be able to issue 100% loans.

Kauli ya kwamba watanzania wote ni masikini vile vile si ya kiungwana kwani is obvious GIN coeficient ya nchi yetu inabehave kama nchi za kipepari, yaani gap kati ya walionacho na wasionacho nikubwa sana na linakuwa kwa kasi. Hivyo ni ukweli kuwa kunafamilia za kitajiri na familia za kimasikini
Tanzania. Mfano kuna watoto hapo Bongo wanasoma Primary ada Milion we know. Shida hapa ni namna yakumtambua masikini na mwenyenacho katika mazingira yaliyoshiba rushwa hilo ndio tatizo kwangu. Hivyo nawashauri urgument zilenge huko maana at the end of the day pamoja na makosa ya serikari ambayo tunayajua wote mwathilika namba 1 ni mwanafunzi husika na familia yake..

Hivyo tutumie nguvu kidogo kama itahitajika lakini umakini zaidi nimuhimu katika swala hili ''is so technical and very political''
 
Tujue kuwa serikali si kijiwe bali serikali ina dhamana kwa nyanja zote na tunalazimika kugawa tulichonacho katika nyaja hizo na ndio maana mashangingi yananunuliwa ili miongoni mwa hao wanaosoma sasa watakapoingia serikalini wayatumie. Warsha na semina pia wanaonufaika nazo ni haohao wanaotoka vyuoni . Fedha inazalishwa na mkulima lakini mkulima hanufaiki nayo lakini tunaziba midomo tunaposikia unyanyashaji wa wakulima. Serikali ni yetu na ni sisi wenyewe tunaotowa ubavu kwa viongozi watuchagulie namna ya kutumia fedha zetu. Hebu natuwatetee wakulima na sio hawa wanaogombania kupanda daraja la watawala.

Ngekewa,
Unachosema ni sawa. Ila kwa mawazo yako, hayo Mashangingi, EPA, DEEP GREEN, Mwananchi Gold, Radar, Ndege ya Rais, Helcopiter za jeshi, Kiwira, Richmonduli, IPTL, ATCL, Meremeta na hizo zote Blingbling...... kwako wewe ni SERIKALI au KIJIWE CHA MAFISADI? Ngoja tusubiri na sisi Yesu wetu aje na kuwafukuza watu wote walioifanya Tanzania kuwa PANGO LA WANYANGANYI. Vibaka wakubwa. Hawana hata aibu kutaka kuifufua ATCL tena bila woga ila wanafunzi ambao kesho watalipa madeni na kulipa kodi wanaambiwa kwa kimyakimya YOU CAN GO TO HELL.
Naona mwenzetu una NGEKEWA zako. Haya hayakuhusu na wewe kila kitu ni NGEKEWA. Wengine kila kitu lazima tukaze misuli ....
Wangelikuwa wako makini, hi;i lisingelitokea. Wangelionyesha mfano kuwa tukaze mikanda, mie ningelikuwa wa kwanza kuwalaani wanafunzi. Ila wao ndiyo kwanza Pinda kasema ananunua Mashangingi ya mwisho 700, juzi wanatangaza tenda ya mashangingi mapya..... Eti serikali si KIJIWE!!!
 
Huyokijana kama angetabiri huo utabiri wake kwa kigezo cha wafanyakazi dhidi ya waajiri, wakulima dhidi ya serikali, chama tawala dhidi ya wapinzani, matajiri dhidi ya masikini basi hayo unayoyasema yangeleta maana lakini kuwa Tanzania isikalike kwa kikundi cha wanafunzi ambao nao wako katika harakati za kukwea kwenye tabaka la walionacho nafikiri Watanzania tuna akili ya kuchaguwa zuri na baya.

Yaleyale.... kuwadharau vijana. Nyie Vigogo siku zote mnahau historia. Wenzenu walisema hivyohivyo. Wakawaona vijana wanachemka. Vijana walivyoanza mavituz ikawa tayari too laite. Uliona juzijuzi wanafunzi wa shule ya msingi walivyoji-organise?? Angalia mabadiliko yaliyotokea Uholanzi, Ufaransa na Europe in general. Vijana wakaanza kuchoma na kubomoa nyumba huko Ufaransa. Wee kaa na kusubiri watabiri kwa wakulima. Ndiyo ubaya na uzuri wa vijana wa unga/bangi. Siku wakianza kudai haki zao, wala hawaogopi kitu. Watachoma na kubomoa hayo mahekalu ya MAFISADI na kibaya zaidi ni kuwa wanaweza kuwabeba hata waliochuma mali zao halali.
The day will come. Ngoja nimsikilze Obama.......
 
Ngekewa,
Unachosema ni sawa. Ila kwa mawazo yako, hayo Mashangingi, EPA, DEEP GREEN, Mwananchi Gold, Radar, Ndege ya Rais, Helcopiter za jeshi, Kiwira, Richmonduli, IPTL, ATCL, Meremeta na hizo zote Blingbling...... kwako wewe ni SERIKALI au KIJIWE CHA MAFISADI? Ngoja tusubiri na sisi Yesu wetu aje na kuwafukuza watu wote walioifanya Tanzania kuwa PANGO LA WANYANGANYI. Vibaka wakubwa. Hawana hata aibu kutaka kuifufua ATCL tena bila woga ila wanafunzi ambao kesho watalipa madeni na kulipa kodi wanaambiwa kwa kimyakimya YOU CAN GO TO HELL.
Naona mwenzetu una NGEKEWA zako. Haya hayakuhusu na wewe kila kitu ni NGEKEWA. Wengine kila kitu lazima tukaze misuli ....
Wangelikuwa wako makini, hi;i lisingelitokea. Wangelionyesha mfano kuwa tukaze mikanda, mie ningelikuwa wa kwanza kuwalaani wanafunzi. Ila wao ndiyo kwanza Pinda kasema ananunua Mashangingi ya mwisho 700, juzi wanatangaza tenda ya mashangingi mapya..... Eti serikali si KIJIWE!!!

Nafikiri mada ilianzia kwa kauli ya kitisho, jee kitishohicho kilistahiki?
Kama unavyosema Tanzania tuna msururu wa maudhi kuanzia EPA, Richmond na mengi mengine.
Sasa iwapo sote tutakuwa na kauli hizo hivyo unafikiri tutakuwa na hata nafasi ya kuwakumbuka hao wanafunzi. Kauli ni nzito na tusisahau kuwa kabla ya kufika nafsi ya elimu waliyonayo sasa walipitia elimu ya msingi na sekondari na huko waliwaacha enzao pengine wana uwezo wa kiakili zaidi kuliko wao, kwa sababu ya kukosa ada za shule na wao wakawa wateule. Sasa kipi cha ajanu katika level yao wakawepo wateule kwani si ndivyo tunavyokwenda?
Kuhusu ungekewa nakubali kuwa ni ngekewa inayoniendesha kwani mimi ni mmoja wa wale waliokosa nafasi za elimu ya juu kwa kisingizio cha nafasi chache kwa wakati huo. Nilikuwa na uwezo wa kiakili lakini nafasi zilikuwa chache na sasa nafasi zimeongezwa still lazima kuweko na wateule.
kuhusu uchaguzi wa matumizi ya serikali bado nitaendelea kutetea kuwa serikali ina majukumu mengi na tukianza kuishitumu serikali kwenye matumizi pengine tutafika pahala na kuiuliza serikali kwanini haiwalipi watumishi wake mishahara yakuwakimu kwanza na baadae kuwashughulikai wanafunzi au kwanini serikali hawalip mishahara mizuri walimu au kwanini serikali haiwapi wakulima pembejeo za bure au kwa mikopo ili waweze kutulisha vizuri na kupata pesa za kujenga hayo majengo ya wagomaji.
Tanzania tuna tabia ya kuzungumza kwa maarifa na sio kuanza kutishiana kwani hapo wanafunzi watapoifanya si pahala pa kukalika itasaidia nini kutatuwa msurur wa matatizo yetu. Jee wafanyakazi tunaolipwa mishahara midogo na sisi tuigeuze Tanzania pahala pasipokalika.
SERIKALI SI KIJiWE ni chombo chenye taratibu na taratibu hizo bila shaka haziwezi kuwafurahisha wote.
 
Yaleyale.... kuwadharau vijana. Nyie Vigogo siku zote mnahau historia. Wenzenu walisema hivyohivyo. Wakawaona vijana wanachemka. Vijana walivyoanza mavituz ikawa tayari too laite. Uliona juzijuzi wanafunzi wa shule ya msingi walivyoji-organise?? Angalia mabadiliko yaliyotokea Uholanzi, Ufaransa na Europe in general. Vijana wakaanza kuchoma na kubomoa nyumba huko Ufaransa. Wee kaa na kusubiri watabiri kwa wakulima. Ndiyo ubaya na uzuri wa vijana wa unga/bangi. Siku wakianza kudai haki zao, wala hawaogopi kitu. Watachoma na kubomoa hayo mahekalu ya MAFISADI na kibaya zaidi ni kuwa wanaweza kuwabeba hata waliochuma mali zao halali.
The day will come. Ngoja nimsikilze Obama.......

Ninachosema ni kuwa Watanzania tuna matatizo chungu nzima na kama vita basi hahitaji wanafunzi wa chuo kikuu kwani kule Pemba au Tarime wanafunzi wa chu kikuu ndio waluiobeba silaha?
 
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine
shy ndugu yangu hii ndiyo lugha ya kujidanganya.
Unafahamu kwamba hakuna amani kati ya wabaya?
Huwezi kushinda unahubiri kuwa kuna amani wakati tangu mwaka jana vijana wanafunzi wa chuo kikuu wamefukuzwa shule kwa cheap reasons na hawana amani. Tena kwa kushindwa kusema nao hoja zao simply kwa sababu tu mtu anayehusika anaweza kutuma FFU kuwafukuza.
Tanzania imesahau habari ya amani siku nyingi na sasa amani imebaki ni wimbo wanaimba watu wa aina ya Shy.
Hizi ni propaganda zisizo na faida na wala hazitawahi kuleta hiyo amani mnayoimba. Mtaishia kuwapiga virungu watoto wa watu bure kila mwaka as if wao wametoka kivita kumbe sivyo ila wanadai haki yao.
 
“Hatuogopi vitisho, tuko tayari kufa, kufukuzwa chuo na hata kwenda jela, tutaendelea kutetea watoto wa masikini, kwani kinachoendelea sasa ni kutengenezwa kwa matabaka kati ya masikini na matajiri, tunaomba Serikali iwarudishe wanafunzi wote vyuoni, vinginevyo Tanzania haitakalika

Hayo ni maneno ya Machibya, aliyekuwa Rais wa iliyokuwa DARUSO. Maneno yake yanafanya nijiulize, hivi Machibya anaelewa maana ya maneno anayoyasema? Tanzania haitakalika, kwa hiyo watanzania wataenda wapi??? na nini kitafanya isikalike? Nani anampa huyu mwanafunzi kiburi cha kutishia maisha ya watanzania? Hizi lugha zisizo na busara zinaonyesha aina ya uongozi uliokuwepo DARUSO. Na sasa watanzania hawawezi kushangazwa na uamuzi wa kuifuta DARUSO iwapo huu ndio upeo wa viongozi wake.

Zemarcopolo,
Nini kinakushangaza?
Huyu Machibya kasema ukweli wake wote. Wala hii si hoja. Hivi akisema Tanzania haitakalika shida iko wapi? Mbona hujajiuliza wale polisi karibu woooooote wa Dar nzima wanatafuta nini pale mlimani? Kweli hapa Tanzania imekalika?
Ninaamini kijana huyu si kwamba kasema kwa hasira kama Invisible anavyotaka tuamini, ila kasema kitu cha kweli na kilikuwapo, kipo na kitaendelea kuwapo!
 
Mkuu, iwapo wanafunzi wangekuwa na hata nusu ya uwezo wako kujielezea, hili suala wala lisingekuwa gumu. Mtu akisoma bandiko lako anapata mwanga zaidi kuliko vitisho vinavyotolewa na hao Daruso (au labda vyombo vya habari-ambavyo wengi ndimo tunapata taarifa, vinachagua cha kuandika).
Hoja unayoieleza hapa, kwamba mfumo upo flawed inaeleweka sana lakini hilo halihalalishi kuwa kila mwanafunzi apatiwe 100% loan.
Kama mfumo uko flawed, solution ni nu kufanya revision. Lakini kikubwa ambacho kinasikika kutoka kwa wanafunzi ni kutaka loan kwa asilimia zote. hatutafika kwa mtindo huo

Well, 'review' ya 'system' wanafunzi wameipigia kelele sana lakini kama kawaida serikali haioni haja ya kufanya hivyo. Kusema ni bora serikali itoe mikopo kwa wanafunzi wote na kwa asilimia 100 ni wazo mbadala la wanafunzi kuliko kuendelea na mfumo wa sasa wa kubaini nani anahitaji kwa kiasi gani.

Serikali ingeweza pia kuona njia nyingine. Lakini walau wanafunzi wame'suggest' hivyo. Kinachotakiwa ni kujadiliana na kufikia 'concesus' bila ya kuwanyima haki ya kuchangia hoja katika kupata suluhisho.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba fedha nyingi za serikali/walipa kodi zinatumiwa vibaya na wachache na hili linamwumiza kila mwananchi mwenye uchungu na nchi yetu.

Leo hii Tanzania tungekuwa mbali sana kama tungetumia raslimali zetu vizuri. Lakini uchu wa wachache umefanya hizi raslimali, kama madini, ziendelee kuwa 'depleted' kwa manufaa ya wachache.

Kwa hiyo, kuliko kuliwa na wachahce ni bora fedha hizo zitumike katika elimu kwani mfumo wa sasa wa utoaji mikopo bado unawanufaisha hao hao wenye uwezo.

Mimi naona bado wanafunzi wana hoja. Kama serikali ingesikiliza ushauri wao na kuufanyia kazi (hata kama siyo exactly jinsi wanafunzi wanavyodai), kusingekuwa na matatizo yanayojitokeza leo hii. Lakini serikali inataka tu kuonyesha kuwa ina nguvu na ikisema kitu lazima kifanyike hivyo.

Hivi kweli kama wanafunzi wameshindwa kulipa ada ukiwalazimisha walipe ada yote kabla ya udahili ndiyo njia bora zaidi ya kuwasaidia wenye uwezo mdogo au kuwaongezea matatizo zaidi/kuwakomoa?

Na mbaya zaidi ni kusikia kauli kuwa wale wanaoshindwa kulipa ni wale wasiotaka kusoma! Pia badala ya kutatua tatizo hili katika context ya Tanzania baadhi ya wasemaji wa serikali wanatoa mifano ya Kenya na Uganda. Kama ni hivyo, mbona kwa mambo mengine ambayo Kenya na Uganda wanafanya vizuri serikali yetu haijaiga?

Mimi bado naona tatizo liko kwenye viongozi wetu. Ingawa ni wasomi sidhani kama wameelemika vizuri kwa maana ya kuwa 'creative and innovative'. Elimu ya kichwani tu haisaidii sana. Inayosaidia ni ile inayobadili mazingira yetu kuwa bora zaidi.

Inasikitisha kuona wanafunzi wakiji'enrol' chini ya ulinzi wa polisi kama wahalifu. Na haya tunayoyafanya kwa sasa tutaendelea nayo tu. Kumbuka Nyerere alikuwa akisema: "Aliyezoea kula nyama ya mtu hawezi kuacha. Akiipata ataila tu."

Hata sisi hivi vitisho vya kutumia silaha - polisi/jeshi - dhidi ya raia hata katika mambo madogo yataendelea tu kwani hakuna njia nyingine viongozi wetu wanayoona inafaa zaidi ya kutumia silaha.
 
maneno aliyotumia kiongozi wa juu wa DARUSO ni kosa kulingana na katiba ya jamhuri wa muungano wa tanzania ya mwaka 1977 toleo la 2005 ibara ya 14,15,na 16 zinazoongozwa na haki ya kuwa hai,haki ya uhuru wa mtu binafsi,haki ya faragha na usalama wa mtu,na uhuru wa mtu kwenda atakako, sheria ya 1984 na 15 ib.6.

Kwa kuzingatia katiba ya nchi hii Vijana wanakosa hekima na busara za uongozi, kwa maana unaweza kuwa na madai ya maana na yenye tija kwa taifa hili isipokuwa wewe kama kiongozi hukashindwa kulead kufikia hizo objectives.

Nashukuru sana serikali inarudisha JKT maana kule kijana anatoka akiwa anaweza kujitegemea na yuko tayari kwa lolote kwa maslahi ya taifa lake.

Naamini maamuzi ya uongozi wa chuo na serikali ni sahihi ,vyama vya wanafunzi vinahitaji kuimarika na kuwa na viongozi matured mentally and philosophically.

Natambua kuwa'Uongozi si kazi ingawa zipo kazi za uongozi'

As leader you need to be proffessional and have high integrity in problem solving skills

AM
 
Last edited:
Back
Top Bottom