''...Tanzania haitakalika''

hapana mkuu ni baada ya FORM SIX nadhani mkuu mmoja amesema uzalendo na kujitegema kwa taifa letu NI VYEMA UKAanzie kwenye familia, nakubaliana nae kabisa.

AM
 
Ibrah, DARUSO imefutwa. Haipo tena. Wataaam wa sheria wanasema walioifua hawana mamlaka ya kuifuta, sasa tungoje kuona nini kitafuata baada ya wanafunzi kurudi ila kwa hali ya sasa hakuna any legal body inayoitwa DARUSO.

Ukipitia tangazo la chuo halisemi moja kwa moja kwamba DARUSO imefutwa. Ilichofanya UDSM ni kutengua sheria zake ambazo zilikuwa zinaitambua DARUSO pamoja na jumuiya nyinginezo za wanafunzi. Nadhani kuna maswala kadhaa ya kujiuliza:

Je uwepo wa DARUSO unategemea kutambuliwa na UDSM? Jibu linaweza kupatikana kwenye katiba ya DARUSO. Kama jibu ni ndiyo basi tangazo la UDSM kutoitambua DARUSO kimsingi linaifuta DARUSO.

Je chuo kina /sheria/utaratibu wa kusajili jumuiya au vyama vya wanafunzi? Sheria/taratibu hizi zinaruhusu unilateral decision kama ambavyo UDSM imefanya?

Je jumuiya na taasisi nyingine zinaweza kuendelea kuitambua DARUSO hata kama UDSM haiitambui?

Hata kama DARUSO, technically,haijafutwa lakini kitendo cha UDSM kutoitambua kitaathiri kwa kiasi kikubwa uwepo wake na uwezekano wa kuweza kutimiza majukumu yake. Hali hii itakuwa ni sawa tu na kufutwa.

Uamuzi wa UDSM wa kutoitambua DARUSO hauonekani kama ni uamuzi wa busara hasa hasa katika hali hii ya mvutano. Mtu wa nje unapata picha ya ubabe zaidi wa UDSM (na Serikali) kuliko busara na maamuzi yaliyopevuka. Mtu unajiuliza maamuzi haya ni kwa maslahi ya nani?
 
Jamani tunahimizwa kwenda shule tukafute ujinga, ila sasa huyu nafikiri hakuna kilichofutika zaidi ya kuongeza.

Tunahitaji kumuomba mungu sana tupate hekima, mambo mengine ni mapito tu, huyu anayesema tanzania haitakalika inabidi achukuliwe ahojiwe atoe maelezo kwa nini haitakalika. May be ana mambo kaandaa ili isikalike.

Maneno yasiyo na mpango yanaponza.
 
Nafikiri mjadala usiwe kwa huyu mwanafunzi bali kilichosababisha mpaka hali ikafikia hapo ilipo. Swali ni kwamba uongozi wa chuo njia waliyoichukua kukabiliana na hali ya hapo chuoni ni sahihi? Hakuna kweli solution mbadala ambayo ingeleta suluhisho la hilo tatizo bila kutumia ubabe?(FFU and the so called stringent measures kuwafanya wanafunzi wasithubutu hata kukohoa!). Acha inconvenience kwa wafanyakazi,waalimu na wakazi walio karibu na maeneo ya chuo! Environment iliyotegenezwa sasa hivi kwa maono yangu hayana tofauti na ya Robert Mugabe. Ilivyo sasa hivi kwa hapo chuoni inanikumbusha enzi zetu tukisoma primary wakati viboko nje nje! Ukimwona mwalimu kapressure kanapanda. What are the think tanks at the parent minisry and the loan board doing? Can't they bang their head and come up with an amicable solution? They are being paid for that. After all, the loans being advanced to the students have to be repaid and we the taxpayers are the one coughing up for them not the Mkandalas or something. Hey guys and gals, what do you think? Have your say!
 
Hawa wanafunzi message wanayoipelekea serikali ya muungwana ni kwamba, nchi ina resources nyingi hata kumudu kuwasomesha wanafunzi wote bure!! People have been made to be believe that the government will solve the people's problems, that is not true ; the truth is that THE GOVERNMENT is the problem!!.Angalia jinsi wanavyotumia resources bila mpangilio mzuri; Pinda anasema hawataagiza mashangingi tena; hapo hapo mashangingi 700 yanapakuliwa bandalini kwa serikali hiyohyo. Sasa wanafunzi wanasema wao wanatozwa hizi ada kwasababu serikali sio makini katika matumizi yake ama sivyo wangekuwa makini rasilimali zetu zingetosha kuwasomesha wao vyuo vikuu bila shida. Hiyo ndio hoja yao. Misallocation of national resources ndio italeta matabakaka katika jamii ambayo in the long run itapelekea nchi yetu isikalike!!
 

Mkuu,

Naamini una ufahamu sana kwenye eneo hili hata kufikia kuanzisha thread. Hivi ni shilingi ngapi hasa zinahitajika kwa mwaka kuwapa loan asilimia 100, hao wanafunzi? na unafikiri ni kiasi gani wanakusanya kwa mwaka kwa waliowakopesha mmoja wao mimi , nakatwa fedha kila mwezi kulipa hili deni na nimemaliza 2005 tu!.

thanks

waberoya
 
Serikali masikini hiyoooooooooooooooo:----



WIMBI la ufisadi linaendelea kuiandama Serikali ya Awamu ya Nne, baada ya kugundulika matumizi mabaya ya sh bilioni 13 kwenye mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, uliopo mkoani Mbeya.

Mbunge wa Kishapu, Fred Mpendazoe (CCM), ndiye aliyeibua tuhuma hizo nzito alipotaka kujua fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kukarabati mgodi huo zilivyotumika kutokana na matatizo katika mgodi huo kuzidi kushamiri siku hadi siku.

Mapendazoe ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ipo mkoani hapa chini ya Mwenyekiti wake,William Shelukindo, alihoji hayo kwenye kikao kilichowakutanisha wakuu wa wilaya za Ileje, Kyela na wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama kama wamewahi kusikia au wana taarifa kwamba serikali ilitoa sh bilioni 13 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya mgodi huo.

“Ndugu Mwenyekiti, ninachofahamu kupitia ripoti ya Jaji Mark Bomani, sh bilioni 13 zilitolewa kwa ajili ya ukarabati wa mgodi wa Kiwira, tunaambiwa mpaka sasa hivi hakuna chochote kilichofanyika, je, fedha hizo zilifikishwa au zimeishia wapi?” alihoji Mpendazoe.
 
hebu tuchambue hoja yenyewe wala tusinganganie kukosoana! unajua kama vita unaisikia kwenye vyombo vya habari huwezi kuona kama ni kitu chenye madhara sana ni kama hakikuhusu nadhani hizi asilimia 40% za uchangiaji zitakapo ugusa mfuko wako ndio utaelewa machibya na wengine wanaomuunga mkono kwenye hoja 100% wanamaanisha nini! Tanzania hii sio masikini sana kama tunavyodhani bali ni vision za viongozi wetu na mambo gani kuyapa vipaumbele( priorities) ndio shida kubwa inayotutesa!
 

Ukweli ni kwamba hata yule anayeendesha range rover vogue angependa serikali iwe inamuwekea mafuta kwenye gari kwa asilimia 100. Cha msingi ni je hawa wanaotaka hizo asilimia 100 kuanzia wanafunzi, wafanya biashara mpaka wakulima na jobless wanaweza kutekelezewa matakwa hayo na serikali. Msilazwe na usingizi mkadhani kuwa wanaotamani kuhudumiwa asilimia 100 na serikali ni wanafunzi wa chuo kikuu peke yao. Huu ni mwanzo tu wa tabia ambayo ikiendekezwa itazagaa kama ukoma nchi nzima. Siku moja mtasikia wanajeshi nao wanataka watimiziwe mahitaji yao kwa asilimia 100, na lugha zenyewe kama ndio hizi kuwa wasipotimiziwa Tanzania haikaliki basi tujiandae na mabaya huko mbele. Tabia hii inapaswa kukemewa, huu sio muda wa mambo ya kitoto. Mtoto ndio akitaka kitu analia mpaka apewe vilevile anavyotaka bila conditions.
 

Mkuu hujajibu swali langu, nimeuliza shilingi ngapi inahitajika ili kuwapa wanafunzi loan ya asilimia 100?? naomba jibu mkuuu!!!, hii post uliyokopi imekuja baada ya kupost mimi, nahitaji msaada wako tafadhali mkuu!

NItapata raha kujua kiasi gani ili niweze kuachangia kwa ufahamu wangu mdogo.
waberoya
 

Swali lako halina jibu la moja kwa moja kwa sababu haliko specific. Kiasi cha pesa kinachohitajika kinabadilika kwa kasi sana kiasi kwamba hakiwezi kukadirika. Kwa mfano chuo Tumaini kilikuwa na wanafunzi mia mbili miaka 11 iliyopita na sasa kina wanafunzi elfu 8. hivyo basi kutoka sh. 600 milioni walizukuwa wanahitaji miaka 11 iliyopita sasa hivi wanahitaji mara 40 zaidi ambazo ni sh. bilioni 24 (hii ni kama thamani ya pesa imebaki ileile kwa miaka 11). Hiyo ni hesabu ya wanafunzi wa Tumaini. Kuna vyuo vingi,na kuna wanafunzi wanaosoma nje ya nchi. Idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama nilivyosema inabadilika kwa kasi kubwa.Tutarajie baada ya miaka miwili Tumaini watakuwa na wanafunzi elfu Kumi! UDSM kuna wanafunzi elfu 21

Hivyo basi kwa kukadiria tu, wanafunzi wote kuanzia Tumaini,IMTU, SAUT, SUA, UDSM, Ardhi University, MUHAS, Kairuki, Dodoma, Chuo kikuu Huria, CBE, AIA, MUM,Exchange Programme wa Uganda, Algeria, China, Ukraine,Urusi etc. wanahitaji kama bilioni 1200 ili kuwakamilishia mahitaji yao kwa asilimia 100 kwa mwaka mmoja.

Bajeti ya nchi ya mwaka 2007/2008 ni sh. Trilion 6(bilion 6000). Wizara elimu imepewa kipaumbele kwa kupata asilimia 18 ya bajeti ambayo ni sh. trilion 1.08(bilioni 1080).Wanafunzi wanagoma wakitak wa[ewe bilioni 1200 ambazo zimezidi bajeti nzima ya wizara. Hivi kweli tunakuwa reasonable tunapowaunga mkono wanafunzi hawa. Hata kama bajeti nzima ya wizara ingetumika kulipia ada za wanafunzi wa chuo kikuu bado isingetosha, wakati huohuo bajeti hiyohiyo inategemewa kuhudumia elimu ya msingi, sekondari ,vyuo mbalimbali na kulipa mishahara ya watumishi wote kuanzia mlinziwa shule mpaka waziri.
 

Mbona hiyo pesa ni ndogo, maana serikali ingekuwa na watendaji makini hii haikuwa kazi ngumu, kwasababu wao wanatoa mikopo lakini hawakusanyi ni miongo kadhaa sasa watu hawaja ghalimikia elimu walioipata toka vyuoni, kama wangekusanya pesa kutoka kwakila aliyekanyaga chuo nadhani pesa hizo ni kidogo sana kwa jamuhuri yetu.kikubwa hapa ni watu wanakuwa wavivu na kama ni hivyo basi watoe za mifuko mwao wawape hao watoto wakatoe matongotongo.
 
ZeMarcopolo katumia mahesabu yasiyo sahihi. Takwimu za fedha wanazopashwa kulipa wanafunzi zinapatikana hapa:

http://www.udsm.ac.tz/admission/bachelors2008_2009/RevisedTuitionFees2008_09.pdf

Utaona toka hizo takwimu kwamba mwanafunzi Mtanzania anatakiwa kulipa jumala ya sh 2.479 million.

Tunazungumzia malipo katika vyuo vya umma, vya Tanzania. Hatuzungumzii malipo kwenye vyuo binafsi. Na ugomvi ulioko sasa ni kuhusu hii milioni mbili na nusu.

Wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma Tanzania ni kiasi cha 30,000. Ili kuwalipia wote kwa 100%, zinahitajika shilingi 74.37 billion only. Hizi ni robo ya fedha zinazokusanywa na TRA kwa mwezi!
==================================================

Nabandika kwa wasiwasi kwani Moderator ameshafuta posting yangu nyingine leo. Sijui kama na hii atafuta!
 


Augustine,
Tunapozingumzia kuwawezesha watanzania kupata elimu ya juu hatuzungumzii vyuo vya umma peke yake. Ndio maana nimeanza na mfano wa Tumaini University.Tunazungumzia watanzania wote wanaosoma ndani na nje ya nchi. Makosa yanayofanywa na wanafunzi wa UDSM wao hufikiria chuo chao tu!!! Unaposema vyuo vya umma nchini vina wanafunzi elfu 30 unakosea kwa sababu Bodi ya mikopo inawawezesha wale wanaosoma advanced diploma pia ambao hawako vyuo vikuu(eg. CBE).UDSM peke yake ina wanafunzi elfu 21. Hili swala liangalieni lote kama watanzania. Mnapowafikiria wanaosoma katika vyuo vya serikali peke yao ndipo mnapokosea. Kwa nini mnawatenga watanzania wenzenu??? Ni kigezo gani mnachokitumia kuunga mkono wanafunzi wa vyuo vikuu vya serikali kupewa asilimia 100 ya mkopo na wale wa vyuo binafsi waachwe solemba??? Hii haifai kabisa na inaonyesha dalili ya kilema cha mawazo, hasahasa pale mnapopiga kelele kuwa watanzania ni masikini halafu mnataka kuudanganya umma kuwa umasikini huo uko kwenye vyuo vya serikali tu.
Hizo hesabu nilizotoa ni sahihi kwa sababu zinagusa wanafunzi wote. Hesabu za kugusa nusu ya tatizo zinaonyesha dalili ya kutaka kupindisha uelewa wa umma juu ya swala lililo mbele yetu la uwezeshaji wa upatikanaji wa elimu ya juu kwa WATANZANIA WOTE.
 

Halafu unapotumia estimates za ada ya UDSM kujua ada ya wanafunzi wa Tanzania unakosea sana. Ada ya mwanafunzi wa udaktari sio 2.7 mili. Na ada ya private universities haiwezi kuwa sawa na ya UDSM, kwa sababu vyuo hivi unlike UDSM vinaendeshwa kwa ada za wanafunzi. Ili kulipa mishahara ya wafanyakazi, bili mbalimbali na kununua vifaa vya kufundishia, ada ya vyuop hivi inakuwa kubwa zaidi ya UDSM. Hivyo estimates kwamba mwanafunzi mmoja anahitaji 2.7 mil, kwa kigezo kuwa hiyo ndio inayohitajika UDSM, ni lame.
 
Hizo pesa wanazoiba na hayo mashangingi wanayonunua na hiyo mikataba bomu ya uchimbaji madini na mirabaha hewa pamoja na kodi ya kawaida kabisa vinatosha kuwasomesha hawa washkaji tena serikali isiongee kabisa hawa jamaa wanafahamu wanachokiongea Tanzania haitakalika kwa sababu ya baadhi ya watu kukandamiza haki za wanyonge. Niko upande wa hawa jamaa wa Daruso. Halafu utaratibu wa kuifuta DARUSO ulitakiwa uzingatie demokrasia kwa kuwashirikisha viongozi wake au tuseme ni janja tu ya nyani jamaa wakirudi wanasema ooh tubadilishe jina tuiite DUSO tufanye uchaguzi tuweke mapandikizi. Huu ni ubabe...ambao madhara yake si kwa Mukandala bali ni kwa watanzania.
 
Serikari tunaiomba iwasaidie ni wake kabisa,
Mungu ibariki Tanzania na Kikwete.
 

ZeMarcopolo,

Unaposema gharama ni zaidi ya mil 2.7 kwa mwanafunzi na hivyo serikali haiwezi una maana gani? Kama serikali haiwezi je wakulima wataweza?

Lengo mojawapo la serikali kukusanya kodi ni kujaribu kugawanya kipato kutoka kwa mwenyenacho kwenda kwa asiyenacho kupitia huduma za kijamii kama elimu.

Hivi unaamini kwa dhati kabisa elimu ni mojawapo kati ya vipaumbele vya serikali yetu? Binafsi naamini tuna tatizo kubwa katika kuweka vipaumbele na kukosa viongozi makini na wenye uzalendo na nchi yao.

Kwa nchi changa kama Tanzania Elimu haipaswi kuwa previlege bali nyenzo ya maendeleo. Elimu ambayo nimeipata haininufaishi peke yangu bali nalitumikia Taifa kwa manufaa ya wote. Hivyo si dhambi kwa serikali kubana matumizi mengine na kuwekeza zaidi kwenye elimu. Na hapa hatuzungumzii kusomesha bure (ingawa hili pia linawezekana) bali kukopesha kwa asilimia mia moja. Nguvu zao waweke kwenye kukusanya madeni naamini watafanikiwa.
 
Naomba kuelimishwa, hawa wanafunzi walipataje nafasi za kuingia chuo?????? Serikali na chuo kikuu hawawasiliani kujua uwezo wa serikali kuwalipia wanafunzi?????
Kwa hiyo swali la kwanza linakuwa
1. Je kama hawa wanafunzi wasingeruhusiwa kujiunga na chuo, ingekuwaje??????
2. Wanafunzi wanaolipiwa wanachaguliwaje???? nafahamu kuna bodi ya mikopo KULIKONI HUKO??????????

Mara nyingi wafanyakazi wavivu wa baadhi ya wizara zetu husika wakikosa muda wakutatua jambo hutafuta "scape goat" na hutengeneza mazingira ya kuficha maovu yao, je haiwezi kuwa lipo jambo kubwa zaidi la linalofichwa hapa.
Hawahawa ni watoto wetu, wadogo zetu inakuwaje tunawasusa sisi wanaserikali, unamsusia nani mwanao.
Nikisoma Mkwawa mwaka fulani, mwanafunzi mmoja alifukuzwa shule, lakini akabaki kwa binamu yake ambae alikuwa mwalimu pale shuleni. Mkuu wa shule akamwuliza yule mwalimu kwanini anampokea mwanafunzi aliyefukuzwa shule?? jibu mtoto wako akifukuzwa shule na nyumbani unamfukuza???????????????? hapana, kwa hiyo yuko nyumbani hapa, huyu kijana nilikabidhiwa na baba na mama yake kule nyumbani, LO Lo ikawa ngumu.

Watoto wa watanzania ni wa watanzania, tunashindwa kutumia busara na hekima kuwalea halafu tunawafukuza KULIKONI?????????????????? WAZAZI WA SIKU HIZI BWANA!!!!!!!!
Nadhani tunahitaji kutatua tatizo la kuwa na migomo kila siku, tunapoteza muda mwingi kujadili na kushangaa yanayoendelea badala ya kujenga nchi yetu masikini
 

Hivi SMU unaamini kuwa wanafunzi wote hawawezi kuafford kujisomesha chuo kikuu? Wapo wanaoweza na wasioweza, ndio maana umewekwa utaratibu kwa kumsaidia kila mwanafunzi kulingana na mahitaji yake. Wanachotaka wanafunzi hawa cha kila mwanafunzi kupewa 100%, kinahitaji pesa nyingi kuliko bajeti ya wizara, kama unavyoona hapo juu. Ninaunga mkono sera ya kuwawezesha watanzania kulingana na mahitaji yao na ninapinga kwa nguvu zote madai ya kutaka kila mwanafunzi apewe 100% ya mahitaji yake kwa sababu wale wenye uwezo wa kujilipia wanapaswa kutuelezea kama hawataki kujilipia wataka kufanyia nini hizo pesa???kununua iPod? Adidas? au wanataka kwenda ''kujirusha''. Tukumbuke kuwa jukumu la serikali sio kusomesha wanafunzi tu. Malaria inasubiri matibabu, Barabara mbovu, Mipaka inatakiwa kulindwa, Wakulima wanahitaji pembejeo na mbolea etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…