Hivi kweli tunaweza kufananisha madai ya Mandela na madai ya hawa vijana wanaotaka pesa nyingi zaidi ya pesa za wizara ya Elimu???
Hivi kweli tunaweza kumfananisha Martin Luther King Jr. na viongozi wanaotegemea vita kuwa suluhisho la mambo? Hivi kweli tumefika mahali tunaona vita ni bora kuliko kuweka utaratibu wa kuwalipisha ada wale wenye uwezo na kuwakopisha wale wasio na pesa???
Hivi kweli tunaweza kutegemea kupata ''akina Obama'' toka kwenye kizazi cha wanafunzi wanaobuni sababu ya mgomo kila kipindi cha mitihani kinapokaribia.
Hivi tunategemea kupata great people among watu ambao wanaona ni bora kununua TV kuuuubwa kuliko kujilipia ada? Hivi kuna haja gani kila mwanafunzi awe na TV yake pale mlimani. Je, TV Moja haitoshi kwa block nzima ya wanafunzi ambao wanaclaim kuwa ni masikini???
Mifano yako haiko relevant kwenye situation iliyo mbele yetu. Viongozi wa DARUSO ni watu dhaifu sana kiroho na kimwili na hawapaswi kufananishwa na Mandele, MLK Jr wala Barack Obama.
Mkuu, asante kwa mawazxo yako unayoyaonyesha humu ndani!
Mkuu, nimekuwa nikidodosa mwasali mengi na kufuatilia nione unafika wapi kumbe hapa!
1. Sikupenda kusema hivi, lakini acha niseme mimi ni assitant lecturer hapo mlimani, niko chuo cha uhandisi, masomo ya ujenzi. Nikiwa katika harakati za kuwasajili wanafunzi mwaka uliopita, tulipewa order , kuwa wanafunzui wasiolipa asilimia wanazodaiwa wasiingie madarasani.
Katika kitivo cha ujenzi chenye wanafunzi zaidi ya mia moja, ni asilimia 25, waliweza kulipa fedha za ada husika, asilimia 30 walipata mikopo asilimia 100, na asilimia 45 hawakuweza kusajiliwa, japo walipata mikopo kwa asimia zao!
Nilipewa dhaman ya kuwasajili hawa tukiwa na junior wenzangu kama 4. deadline ilipofika, hapo ndipo mwanzo wa picha nzima nilivyoipata.
Binti akiwa amevaa ushungi, mtoto mdogo amefaulu kutoka shule moja maarufi ya special school, akija ukweli akiwa anatoa machozi! alisema anasubiri wapewe mikopo na serikali, katika ule mkopo (posho ya chakula)atakaopewa ndio atakayokata alipe asilimia 40 anayodaiwa! mimi ni mtu mzima, na ndoa yangu changa, nilimwacha yule binti pale na kwenda chooni kutoa machozi kidogo. nikamuuliza sasa utakula nini? akasema sijui, kwao morogoro, dar hana ndugu, ila kuna watu anatoka nao kijiji kimoja, labda atakuwa akienda kwa katika nyakati za shida.
Nilimsikiliza wa pili,wa tatu, wa nne, mpaka wote 20. Moyo wangu ulijaa simanzi. hadithi kama hizi zipo nyingi na wengi wanazifahamu kama umekuwa karibu japo kujua wanafunzi hawa wanatoka wapi. uzuri ni kuwa waliwaruhusu waingie madarasani! kwenye uongozi huu, huu!!!
Well chuo kikuu, wanakuja watu wametoka makazini, wengine kweli kwao wanafedha, hivyo swala la TV, halitakosekana, kugeneralise kuwa wanafunzi wataka TV kuuuuubwa, ni kufanya makosa makuuuuuuuuuubwa ambayo hata kama siioni sura yako lakini value yako haina tofauti na watu wa kijiweni.
nimesoma malimani, nimekaa hotseli za mabibo, nimekaa main campus , I hereby saying si wanafunzi wote wana TV!!!!!!!, Hayo ni mawazo ya wasiofika vyuo vya juu!! wasiojua kuwa kuna level mbalimbali za watu na haziepukiki.
Kama kuna linaloumiza usilolijua ni kuwa kuna wanafunzi wamendikwa wanapata asilimia 60, lakini ukweli wanapata asilimia 90 au 100. fedha za juu zinaenda kwa wajanja wachache waliobodi ya mikopo. Kuna watu nawafahamu ambao ni mayatima with death certificates of thei parents, lakini wanapata asilimia 60, 80.
Labda kwa kukusaidia kidogo mkuu, wazo la asilimia lina work tu kama aina ya mfumo tulio nao unaruhusu mtu yeyote kufanya kazi katika level yeyote ilimradi adeliver, pili kama mfumo wetu wa elimu unaruhusu mtu kujiajiri akimaliza form six. ukienda vodacom customer care unakuta graduates! na pia unawakuta form six, waliotoka international school! kwani wanajua kiingereza!
Hilo PIA LINA WORK KAMA CHUO HAKINA MFUMO WA DISCO,KUWA WEWE SOMA, PIGA KAZI SOMA, ILI MRADI MALIZA CHUO KWA WAKATI WAKO NA TUPE MKOPO WETU. NOT NOW! NOT TANZANIA! NOT WITH THIS KIND OF SYSTEM!!
ebu futa hilo la TV kwanza nione kuwa ngau umesoma vyuo vyetu, kama IFM, MZUMBE, MLIMANI, TUMAINI N.K! kusema wanataka fedha kwa ajili ya TV, ni kukosa la kusema