''...Tanzania haitakalika''

''...Tanzania haitakalika''

ZeMarcopolo,

Unaposema gharama ni zaidi ya mil 2.7 kwa mwanafunzi na hivyo serikali haiwezi una maana gani? Kama serikali haiwezi je wakulima wataweza?

Lengo mojawapo la serikali kukusanya kodi ni kujaribu kugawanya kipato kutoka kwa mwenyenacho kwenda kwa asiyenacho kupitia huduma za kijamii kama elimu.

Hivi unaamini kwa dhati kabisa elimu ni mojawapo kati ya vipaumbele vya serikali yetu? Binafsi naamini tuna tatizo kubwa katika kuweka vipaumbele na kukosa viongozi makini na wenye uzalendo na nchi yao.

Kwa nchi changa kama Tanzania Elimu haipaswi kuwa previlege bali nyenzo ya maendeleo. Elimu ambayo nimeipata haininufaishi peke yangu bali nalitumikia Taifa kwa manufaa ya wote. Hivyo si dhambi kwa serikali kubana matumizi mengine na kuwekeza zaidi kwenye elimu. Na hapa hatuzungumzii kusomesha bure (ingawa hili pia linawezekana) bali kukopesha kwa asilimia mia moja. Nguvu zao waweke kwenye kukusanya madeni naamini watafanikiwa.

umesema kweli lakini hawa jamaa wanafanya kichwa ngumu hila waache wachukulie poa sisi hatutasita kuwaelimisha ili mpiganie haki yenu kisawasawa maana binafsi siko tayari kushuudia Tanzania ikitafunwa na mifisadi dawa ipo jikoni. hao mado na wahakikishieni watasoma tu! labda mlima kilimanjaro utoweke.
 
alichokosea ni kuwa hata kwa sasa haikaliki....umeme shida, maji, mafuta hakuna, wakazi wa changanyikeni wamekuwa wakimbizi kwao kisa chuo kikuu Dar hawataki wapite... jamani kweli nchi haikaliki tena!!!!

ni kweli hapakaliki kafanye assesment hao wanaoweza kujilipia wengi wao ni wale walionunua pepa, watoto wa masikini hela ya kulipia mtihani walikuwa hawana unadhani wanaweza kuwa na hela ya kununua paper, mlioko maofisini mnaelewa, watu wa chuo kikuu fikira darasa la saba labda kwasababu waliweza kusoma mpaka darasa la saba bila mtihani wa kufanya siku moja kabla ya tarehe ya mtihani..
 
On a lighter note...karibuni Kenya... huku ndio kabisa hakukalikiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii,
 
Swali lako halina jibu la moja kwa moja kwa sababu haliko specific. Kiasi cha pesa kinachohitajika kinabadilika kwa kasi sana kiasi kwamba hakiwezi kukadirika. Kwa mfano chuo Tumaini kilikuwa na wanafunzi mia mbili miaka 11 iliyopita na sasa kina wanafunzi elfu 8. hivyo basi kutoka sh. 600 milioni walizukuwa wanahitaji miaka 11 iliyopita sasa hivi wanahitaji mara 40 zaidi ambazo ni sh. bilioni 24 (hii ni kama thamani ya pesa imebaki ileile kwa miaka 11). Hiyo ni hesabu ya wanafunzi wa Tumaini. Kuna vyuo vingi,na kuna wanafunzi wanaosoma nje ya nchi. Idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama nilivyosema inabadilika kwa kasi kubwa.Tutarajie baada ya miaka miwili Tumaini watakuwa na wanafunzi elfu Kumi! UDSM kuna wanafunzi elfu 21

Hivyo basi kwa kukadiria tu, wanafunzi wote kuanzia Tumaini,IMTU, SAUT, SUA, UDSM, Ardhi University, MUHAS, Kairuki, Dodoma, Chuo kikuu Huria, CBE, AIA, MUM,Exchange Programme wa Uganda, Algeria, China, Ukraine,Urusi etc. wanahitaji kama bilioni 1200 ili kuwakamilishia mahitaji yao kwa asilimia 100 kwa mwaka mmoja.

Bajeti ya nchi ya mwaka 2007/2008 ni sh. Trilion 6(bilion 6000). Wizara elimu imepewa kipaumbele kwa kupata asilimia 18 ya bajeti ambayo ni sh. trilion 1.08(bilioni 1080).Wanafunzi wanagoma wakitak wa[ewe bilioni 1200 ambazo zimezidi bajeti nzima ya wizara. Hivi kweli tunakuwa reasonable tunapowaunga mkono wanafunzi hawa. Hata kama bajeti nzima ya wizara ingetumika kulipia ada za wanafunzi wa chuo kikuu bado isingetosha, wakati huohuo bajeti hiyohiyo inategemewa kuhudumia elimu ya msingi, sekondari ,vyuo mbalimbali na kulipa mishahara ya watumishi wote kuanzia mlinziwa shule mpaka waziri.

wawabane wale waliosoma kwa mkopo waanze kurudisha jamani acheni fikira za kizamani kama wameshindwa kuokota hela zote za wanafunzi zilizokopeshwa toka mwaka 1994, si upumbavu huo, hebu watueleze wameweza kurudisha hizo hela walizokopesha kiasi gani, hapa kwangu kuna zaidi ya wafanyakazi 200 na wote wamekopeshwa ni juhudi gani zinafanyika maana naona kama wako tu wamejikalia tu wanabaki kusema serikali haina hela hamna haja ya kutumia hela za serikali mi nimeboreka kweli na shughuli za nchi hii zinavyoendeshwa bora njiwa anaweza kutafutia watoto wake chakula na kuwatunza mpaka wanapoweza kujitegemee uongozi wetu wala mnakalia kujenga majumba kumikumi na magari mia, wanawake malukuki, na kuuza nchi then mtafaidi nini unalala kwenye chumba kimoja na unaendesha gari moja unakula chakula sahani moja yote hayo ni upuuuzi na kujilisha uchafu afadhali mkufe wote
 
Nafikiri mjadala usiwe kwa huyu mwanafunzi bali kilichosababisha mpaka hali ikafikia hapo ilipo. Swali ni kwamba uongozi wa chuo njia waliyoichukua kukabiliana na hali ya hapo chuoni ni sahihi? Hakuna kweli solution mbadala ambayo ingeleta suluhisho la hilo tatizo bila kutumia ubabe?(FFU and the so called stringent measures kuwafanya wanafunzi wasithubutu hata kukohoa!). Acha inconvenience kwa wafanyakazi,waalimu na wakazi walio karibu na maeneo ya chuo! Environment iliyotegenezwa sasa hivi kwa maono yangu hayana tofauti na ya Robert Mugabe. Ilivyo sasa hivi kwa hapo chuoni inanikumbusha enzi zetu tukisoma primary wakati viboko nje nje! Ukimwona mwalimu kapressure kanapanda. What are the think tanks at the parent minisry and the loan board doing? Can't they bang their head and come up with an amicable solution? They are being paid for that. After all, the loans being advanced to the students have to be repaid and we the taxpayers are the one coughing up for them not the Mkandalas or something. Hey guys and gals, what do you think? Have your say!

mkandala unaliona hilo, ngoja uone kama hao wanafunzi wa private utawapata watakimbilia kule kwenye amani, na mmiss Luhanga alikuwa mkorofi ila pale kwenye madai yenye akili alikuwa akijirudi, huyu mshomire gundu tupu
 
Hivi SMU unaamini kuwa wanafunzi wote hawawezi kuafford kujisomesha chuo kikuu? Wapo wanaoweza na wasioweza, ndio maana umewekwa utaratibu kwa kumsaidia kila mwanafunzi kulingana na mahitaji yake. Wanachotaka wanafunzi hawa cha kila mwanafunzi kupewa 100%, kinahitaji pesa nyingi kuliko bajeti ya wizara, kama unavyoona hapo juu. Ninaunga mkono sera ya kuwawezesha watanzania kulingana na mahitaji yao na ninapinga kwa nguvu zote madai ya kutaka kila mwanafunzi apewe 100% ya mahitaji yake kwa sababu wale wenye uwezo wa kujilipia wanapaswa kutuelezea kama hawataki kujilipia wataka kufanyia nini hizo pesa???kununua iPod? Adidas? au wanataka kwenda ''kujirusha''. Tukumbuke kuwa jukumu la serikali sio kusomesha wanafunzi tu. Malaria inasubiri matibabu, Barabara mbovu, Mipaka inatakiwa kulindwa, Wakulima wanahitaji pembejeo na mbolea etc.

Ni kweli wapo wanaoweza kujilipia lakini naamini ni wachache sana. Huo utaratibu unaousema umefanikiwa kiasi gani? Matatizo tunayoyashudia hivi sasa kwa sehemu kubwa chanzo chake si huo utaratibu? Tumeambiwa kwa utaratibu uliopo kama una watoto mapacha usishangae wakawekwa kwenye category mbili tofauti! Hili linaweza kutokea Tanzania tu!
 
wawabane wale waliosoma kwa mkopo waanze kurudisha jamani acheni fikira za kizamani kama wameshindwa kuokota hela zote za wanafunzi zilizokopeshwa toka mwaka 1994, si upumbavu huo, hebu watueleze wameweza kurudisha hizo hela walizokopesha kiasi gani, hapa kwangu kuna zaidi ya wafanyakazi 200 na wote wamekopeshwa ni juhudi gani zinafanyika maana naona kama wako tu wamejikalia tu wanabaki kusema serikali haina hela hamna haja ya kutumia hela za serikali mi nimeboreka kweli na shughuli za nchi hii zinavyoendeshwa bora njiwa anaweza kutafutia watoto wake chakula na kuwatunza mpaka wanapoweza kujitegemee uongozi wetu wala mnakalia kujenga majumba kumikumi na magari mia, wanawake malukuki, na kuuza nchi then mtafaidi nini unalala kwenye chumba kimoja na unaendesha gari moja unakula chakula sahani moja yote hayo ni upuuuzi na kujilisha uchafu afadhali mkufe wote

Na ndiyo hapo nilipokuwa nataka nione uwezo wa management alionao Zemarcopolo, pamoja na kuwa nimempa jibu mimi nimemaliza mwaka 2005, lakini sheria ikitekelezeka tangua miaka ya 90, fedha ni nyingi mno, ndio wenzetu wanavyoendesha vyuo vyao na wanawasomi wengi.

Serikali si linyama fulani au kitu fulani cha ajabu, no serikali ni watu, wanaotakiwa wafikirie na si kupambana kama wanayofanya wao, pasi kufikiria. Waziri Kapuya, kwa maneno yake anasema serikali inao uwezo huo!!!! ina maan marcopolo hata hajui ndani ya serikali yenyewe wanapingana kuhusu hili swala. Infact hata kikwete mwenyewe hataki iwe hivyo ni pressure za donors! why?? wanataka tuendelee hivi hivi tuwe na wasmo wa aina ya zemarcopolo, waliotayari kushoot trouble at that time kwa visingizio vingi, pasi kujua kuna solution katika kila swala.

Inshort maada hii inaumiza kwa sababu wengi hawajui situation yenyewe ilivyo chuo. katika eastafrica sisi ndiyo tuna mwendo wa kinyonga kutengeneza wasomi! nchi bila wasomi, tusitegemee miujiza! na hawa ndiyo tumewapoteza tena, taifa halijengeki, maana watatafuta sehemu ya kulipa kisasi kama si kuonea watoto wetu, basi kuwa mafisadi!
 
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine

nachukia hiyo sentensi hapo juu...
 
Hapa naona mchangiaji umeangalia material aspect of development. JKT ina umuhimu mkubwa sana, na wala JKT haihitaji fungu kubwa, vijana wenye nguvu wa JKT wana uwezo wa kuzalisha zaidi ya wanavyotumia. So JKT ni kitega uchumi ikiendeshwa vizuri.

Kwanza hao wanafunzi wa UDSM wasaidiwe na baadaye ije hiyo JKT! Hakuna anayeipinga.
 
Matatizo haya yanasababishwa na viongozi wasiofikiri na waojiona miungu walioko serikalini.Wanajiona kuwa wao ndo watu pekee wenye kufikiri mambo sahihi. Hata kama itaonekana wamekosea hawatakuwa tayari kukubali. Walikimbilia ku-introduce hii sera bila kufanya maandalizi yanayostahili na yakutosha. Kuna matatizo kuanzia upatikanaji wa wapewaji mikopo,utoaji mikopo na namna a kuirudisha.
Mimi nashangaa kwa huu utaratibu wanaong'ang'ania, najiuliza je, mtoto wa Pinda ni wa mkulima na alistahili kuwa katika kundi la wanafunzi wanaopewa mikopo wa asilimia 100.
 
“Hatuogopi vitisho, tuko tayari kufa, kufukuzwa chuo na hata kwenda jela, tutaendelea kutetea watoto wa masikini, kwani kinachoendelea sasa ni kutengenezwa kwa matabaka kati ya masikini na matajiri, tunaomba Serikali iwarudishe wanafunzi wote vyuoni, vinginevyo Tanzania haitakalika

Hayo ni maneno ya Machibya, aliyekuwa Rais wa iliyokuwa DARUSO. Maneno yake yanafanya nijiulize, hivi Machibya anaelewa maana ya maneno anayoyasema? Tanzania haitakalika, kwa hiyo watanzania wataenda wapi??? na nini kitafanya isikalike? Nani anampa huyu mwanafunzi kiburi cha kutishia maisha ya watanzania? Hizi lugha zisizo na busara zinaonyesha aina ya uongozi uliokuwepo DARUSO. Na sasa watanzania hawawezi kushangazwa na uamuzi wa kuifuta DARUSO iwapo huu ndio upeo wa viongozi wake.

Maneno yanayokaribiana na hayo yaliwahi kutamkwa na Nelson Mandela na kweli alienda jela lakini baadaye ubaguzi wa rangi uliweza kutokomezwa kwa kiwango fulani na huyo huyo Mandela kaja kuwa Raisi wa Afrika Kusini.

Maneno kama hayo yaliwahi kutamkwa na Martin Luther King lakini pamoja na kupigwa, kuteswa na baadaye kuuwaawa, hivi leo matunda ya maneno yake tumeyashuhudia kwa Barack Hussein Obama kuutwaa Uraisi Maerekani.

Maneno kama hayo yaliwahi kutamkwa Na msururu wa wapigania haki na ingawa walipatwa na misukosuko yasiyoweza kuelezeka kirahisi, lakini matunda yake hata kama hawakuyafaidi wenyewe yalikuja kuwanusuru vizazi vilivyofuatia.

Tanzania tuna ugonjwa na ni ugonjwa mbaya kuliko ukimwi - woga wa kutetea kile tunachokiamini kuwa ni haki yetu ya msingi kwa nguvu na ujasiri kama wanavyofanya wanamapinduzi duniani kote eti Tz ni kisiwa cha amani hata kama hiyo amani inalindwa kwa mtutu wa bunduki.

Tumeweka rehani maisha ya baadaye ya watoto wetu kwa mamluki eti kwa kisingizio cha kuvuruga amani lakini ukweli ni kuwa tunachofanya hakina tofauti na kumwaga petroli kwenye moto ambao unaanza kutuzunguka kila pembe.

ZeMarcopolo, nani alimpa Nelson Mandela kiburi, nani alimpa Indira Gandhi jeuri, nani alimpa Martin Luther King kiburi na hapa nyumbani nani alimpa Mwl Julius Nyerere jeuri ya kupambana na Mkoloni aliyekuwa na himaya ya nchi zaidi ya hamsini duniani.

Jeuri ya mtu moja, Field Marshal Okelo iliweza kuzaa mapinduzi ya Zanzibar - bahati mbaya ilichukua ujeuri wa mtu wa nje kuwezesha hili. Tumeshuhudia jeuri na kiburi kutoka kwa watu kama Raila Odinga (nusu ya maisha yake ya siasa akiwa jela), je sisi ?

Tumezoea vya kunyonga na anapotokea shujaa kati yetu tunajiuliza huyu jeuri katoa wapi. Tumezoea kula tusivovifanyia kazi na akitokea mzalendo akahoji, tunakimbilia kumhukumu kuwa anataka kuvunja amani na mshikamano.

Wazee wa EAC tuliwanyooshea kidole kwa jeuri ya kulala barabarani kudai haki yao, wanafunzi wa UDSM unawanyooshea kidole kwa kiburi cha kudai haki, Dr. Slaa ananyooshewa kidole kwa kupandikiza siasa za chuki kwa kuwapa kibano mafisadi - Watanzania ndivyo tulivyo.

Jeuri ya serikali dhidi ya wamanchi wala hatuinyoshee vidole, jeuri ya CCM kukumbatia mafisadi hatuulizi inatokana na nini, jeuri ya Mkapa kukwapua mali ya wananchi wala haitunyimi usingizi. Heko Machibya kwa kujitolea mhanga hata kama wakina ZeMarcopolo watajificha mvunguni mwa vitanda vyao. A luta continua !!
 
Sikutegemea maneno kama haya yatamkwe na mtu aliyepewa dhamana ya kuongoza wanafunzi, tena ktk chuo kikuu cha Dar es salaam. Anataka nini? Hivi angesema kuwa Uamuzi uliofanywa na Serikali haukuwa mzuri na kuwaomba wananchi kuishinikiza kwa hoja za maana Serikali iufute uamuzi wake angepungukiwa na nini? Ni nani anakata vita Tanzania? Kuna makundi mengine yapo kwa ajili ya kuwaingiza ujinga wenzao. Wana-Daruso muwe makini sana na viongozi wa namna hii.
 
Wapigania uhuru hao waliyatamka maneno hayo kupitia vyama vya harakati za ukombozi, je, munataka kututhibitishia kuwa naye ni mwana-siasa? Ni wa chama gani vile? Kwanini asiende kuyazungumzia maneno hayo ktk jukwaa la kisiasa?
 
Jemedari mzuri hupeleka majeshi yake kwenye vita anayojua kuwa atashinda. Tusijazane ujinga hapa. Unataka tumsaidie halafu kipatikane kitu gani? Kwani hatua za Serikali kuifuta DARUSO zimefanya wanafunzi wakose walimu wa kuwafundisha? Mbona tunashabikia vitu bila kuvipima jamani? Kwani Chuo hakiwezi kutoa masomo bila DARUSO? Kuna nini hasa ktk chombo hiki? Daruso sio mwisho wa Elimu Tanzania hata kidogo.
 
Hawa vijana wasilete masihara na serikali hawataishinda. Wao wameshika shoka wakati serikali imeshika mpini. Kwa taarifa yenu pana mkono wa Zito, Mnyika na wengineo kupitia mtandao wa Students Network Programme. Ukienda BRELA and ukisearch utagundua akina Zito Kabwe ndiyo guarantors. Mpaka leo wamezeeka bado wanutumia mtandao huo kuihujumu serikali. Haikubaliki lazima washughulikiwe. Kwa sababu hawa wanafunzi ni UV CHADEMA
 
Daruso ilishafutwa sijui alikuwa anaongea kwa niaba ya nani kauli kama hizo hazitakiwi haswa kwa nchi yetu ya tanzania tuliozoea amani , uhuru na upendo maisha yetu yote hatuko tayari kuacha vijana hao watishie maisha wengine

Hiyo Amani unayoiongelea ni amani ya namna gani?
Hiyo amani uhuru na upendo mmezoea wewe na nani?
Kuna uppendo Tanzania?
MH Mkapa anampenda nani?

Je huu ni ule Uhuru wa kujichomoa na kujikomboa kutoka katika makucha ya Waingereza, kisha wenzetu wachache wa kundi la CCM kwa makusudi kuamua kutuchomeka makucha yao kwa niaba yao nawake zao palepale alipochomeka Muingereza na kututia katika utumwa ndani ya dola yetu wenyewe???

Afadhari hata Muingereza alinyonya akajenga London, ninyi wakoloni weusi mnajenga nini na mnajenga wapi?

Uhuru wa Viongozi wa serikali ya CCM kufungua milango ya BOT na kuchota Tani 50 za Dola ili kudumisha tabala lao chafu la viongozi wenye choyo na kila aina ya hila?

Uhuru wa viongozi wa serikali ya CCM kuuza ardhi ya Wahadzabe kwa Matycoon wa kiarabu ili wajenge jiwanja la kuchezea polo, bila kubughudhiwa na wananchi?
Ni Uhuru gani huo usio na nidhamu wala kiasi?

Ni Uhuru ni Uhuni?

Mimi binafsi kamwe sijawahi kuimba wimbo huu wa amani na utulivu ukaniingia akilini.
Sikatai kwamba sijawahi kuimba, ila nakataa katakata kwamba umewahi au utakuja niingia akilini.
Hata Yesu yule nabii Mgalilaya aliwahi kusema " Amani nawapa lakini si kama ile itokayo duniani bali ile itokayo kwa Mungu" Yeye pia alikuwa na maana yake ambayo ni wale tu wanaotaka kuelewa ndiyo huelewa maana yake.

Mimi si msomaji mzuri wa alama za nyakati, pia uatafiti wangu unaonyesha kwamba wengi hawajui au hawana mpango wa kusoma alama za nyakati.

Kama alivyosema MH Obama kwamba "Wengi wanabisha na kubeza juhudi mpya kwa kudhani kwamba bado wanasimama pale pale walipo simama jana, kumbe ardhi chini ya miguu yao imehama, kwa hiyo pale wasimamapo si pale waliposimama jana."
Watu wa namna hii wako wengi na wapo kwenye makundi makubwa mawili wengine wamechelewa na kamwe hawatakuwa kwenye msafara na wengine wamewahi tatizo lao wameweka kikao pasipo na makao.

Wote tunatakiwa kujifunza kusoma alama za nyakati kuliko kubeza kila jambo kwa visingizo vya juzi.
 
Hawa vijana wasilete masihara na serikali hawataishinda. Wao wameshika shoka wakati serikali imeshika mpini. Kwa taarifa yenu pana mkono wa Zito, Mnyika na wengineo kupitia mtandao wa Students Network Programme. Ukienda BRELA and ukisearch utagundua akina Zito Kabwe ndiyo guarantors. Mpaka leo wamezeeka bado wanutumia mtandao huo kuihujumu serikali. Haikubaliki lazima washughulikiwe. Kwa sababu hawa wanafunzi ni UV CHADEMA

Haya ni maneno ya kizushi na sidhani kama yanatusaidia.
 
Maneno yanayokaribiana na hayo yaliwahi kutamkwa na Nelson Mandela na kweli alienda jela lakini baadaye ubaguzi wa rangi uliweza kutokomezwa kwa kiwango fulani na huyo huyo Mandela kaja kuwa Raisi wa Afrika Kusini.

Maneno kama hayo yaliwahi kutamkwa na Martin Luther King lakini pamoja na kupigwa, kuteswa na baadaye kuuwaawa, hivi leo matunda ya maneno yake tumeyashuhudia kwa Barack Hussein Obama kuutwaa Uraisi Maerekani.

Maneno kama hayo yaliwahi kutamkwa Na msururu wa wapigania haki na ingawa walipatwa na misukosuko yasiyoweza kuelezeka kirahisi, lakini matunda yake hata kama hawakuyafaidi wenyewe yalikuja kuwanusuru vizazi vilivyofuatia.

Tanzania tuna ugonjwa na ni ugonjwa mbaya kuliko ukimwi - woga wa kutetea kile tunachokiamini kuwa ni haki yetu ya msingi kwa nguvu na ujasiri kama wanavyofanya wanamapinduzi duniani kote eti Tz ni kisiwa cha amani hata kama hiyo amani inalindwa kwa mtutu wa bunduki.

Tumeweka rehani maisha ya baadaye ya watoto wetu kwa mamluki eti kwa kisingizio cha kuvuruga amani lakini ukweli ni kuwa tunachofanya hakina tofauti na kumwaga petroli kwenye moto ambao unaanza kutuzunguka kila pembe.

ZeMarcopolo, nani alimpa Nelson Mandela kiburi, nani alimpa Indira Gandhi jeuri, nani alimpa Martin Luther King kiburi na hapa nyumbani nani alimpa Mwl Julius Nyerere jeuri ya kupambana na Mkoloni aliyekuwa na himaya ya nchi zaidi ya hamsini duniani.

Jeuri ya mtu moja, Field Marshal Okelo iliweza kuzaa mapinduzi ya Zanzibar - bahati mbaya ilichukua ujeuri wa mtu wa nje kuwezesha hili. Tumeshuhudia jeuri na kiburi kutoka kwa watu kama Raila Odinga (nusu ya maisha yake ya siasa akiwa jela), je sisi ?

Tumezoea vya kunyonga na anapotokea shujaa kati yetu tunajiuliza huyu jeuri katoa wapi. Tumezoea kula tusivovifanyia kazi na akitokea mzalendo akahoji, tunakimbilia kumhukumu kuwa anataka kuvunja amani na mshikamano.

Wazee wa EAC tuliwanyooshea kidole kwa jeuri ya kulala barabarani kudai haki yao, wanafunzi wa UDSM unawanyooshea kidole kwa kiburi cha kudai haki, Dr. Slaa ananyooshewa kidole kwa kupandikiza siasa za chuki kwa kuwapa kibano mafisadi - Watanzania ndivyo tulivyo.

Jeuri ya serikali dhidi ya wamanchi wala hatuinyoshee vidole, jeuri ya CCM kukumbatia mafisadi hatuulizi inatokana na nini, jeuri ya Mkapa kukwapua mali ya wananchi wala haitunyimi usingizi. Heko Machibya kwa kujitolea mhanga hata kama wakina ZeMarcopolo watajificha mvunguni mwa vitanda vyao. A luta continua !!

Hivi kweli tunaweza kufananisha madai ya Mandela na madai ya hawa vijana wanaotaka pesa nyingi zaidi ya pesa za wizara ya Elimu???

Hivi kweli tunaweza kumfananisha Martin Luther King Jr. na viongozi wanaotegemea vita kuwa suluhisho la mambo? Hivi kweli tumefika mahali tunaona vita ni bora kuliko kuweka utaratibu wa kuwalipisha ada wale wenye uwezo na kuwakopisha wale wasio na pesa???

Hivi kweli tunaweza kutegemea kupata ''akina Obama'' toka kwenye kizazi cha wanafunzi wanaobuni sababu ya mgomo kila kipindi cha mitihani kinapokaribia.

Hivi tunategemea kupata great people among watu ambao wanaona ni bora kununua TV kuuuubwa kuliko kujilipia ada? Hivi kuna haja gani kila mwanafunzi awe na TV yake pale mlimani. Je, TV Moja haitoshi kwa block nzima ya wanafunzi ambao wanaclaim kuwa ni masikini???

Mifano yako haiko relevant kwenye situation iliyo mbele yetu. Viongozi wa DARUSO ni watu dhaifu sana kiroho na kimwili na hawapaswi kufananishwa na Mandele, MLK Jr wala Barack Obama.
 
Mkuu, asante kwa mawazxo yako unayoyaonyesha humu ndani!

Mkuu, nimekuwa nikidodosa mwasali mengi na kufuatilia nione unafika wapi kumbe hapa!

1. Sikupenda kusema hivi, lakini acha niseme mimi ni assitant lecturer hapo mlimani, niko chuo cha uhandisi, masomo ya ujenzi. Nikiwa katika harakati za kuwasajili wanafunzi mwaka uliopita, tulipewa order , kuwa wanafunzui wasiolipa asilimia wanazodaiwa wasiingie madarasani.

Katika kitivo cha ujenzi chenye wanafunzi zaidi ya mia moja, ni asilimia 25, waliweza kulipa fedha za ada husika, asilimia 30 walipata mikopo asilimia 100, na asilimia 45 hawakuweza kusajiliwa, japo walipata mikopo kwa asimia zao!

Nilipewa dhaman ya kuwasajili hawa tukiwa na junior wenzangu kama 4. deadline ilipofika, hapo ndipo mwanzo wa picha nzima nilivyoipata.

Binti akiwa amevaa ushungi, mtoto mdogo amefaulu kutoka shule moja maarufi ya special school, akija ukweli akiwa anatoa machozi! alisema anasubiri wapewe mikopo na serikali, katika ule mkopo (posho ya chakula)atakaopewa ndio atakayokata alipe asilimia 40 anayodaiwa! mimi ni mtu mzima, na ndoa yangu changa, nilimwacha yule binti pale na kwenda chooni kutoa machozi kidogo. nikamuuliza sasa utakula nini? akasema sijui, kwao morogoro, dar hana ndugu, ila kuna watu anatoka nao kijiji kimoja, labda atakuwa akienda kwa katika nyakati za shida.

Nilimsikiliza wa pili,wa tatu, wa nne, mpaka wote 20. Moyo wangu ulijaa simanzi. hadithi kama hizi zipo nyingi na wengi wanazifahamu kama umekuwa karibu japo kujua wanafunzi hawa wanatoka wapi. uzuri ni kuwa waliwaruhusu waingie madarasani! kwenye uongozi huu, huu!!!

Well chuo kikuu, wanakuja watu wametoka makazini, wengine kweli kwao wanafedha, hivyo swala la TV, halitakosekana, kugeneralise kuwa wanafunzi wataka TV kuuuuubwa, ni kufanya makosa makuuuuuuuuuubwa ambayo hata kama siioni sura yako lakini value yako haina tofauti na watu wa kijiweni.

nimesoma malimani, nimekaa hotseli za mabibo, nimekaa main campus , I hereby saying si wanafunzi wote wana TV!!!!!!!, Hayo ni mawazo ya wasiofika vyuo vya juu!! wasiojua kuwa kuna level mbalimbali za watu na haziepukiki.

Kama kuna linaloumiza usilolijua ni kuwa kuna wanafunzi wamendikwa wanapata asilimia 60, lakini ukweli wanapata asilimia 90 au 100. fedha za juu zinaenda kwa wajanja wachache waliobodi ya mikopo. Kuna watu nawafahamu ambao ni mayatima with death certificates of thei parents, lakini wanapata asilimia 60, 80.

Labda kwa kukusaidia kidogo mkuu, wazo la asilimia lina work tu kama aina ya mfumo tulio nao unaruhusu mtu yeyote kufanya kazi katika level yeyote ilimradi adeliver, pili kama mfumo wetu wa elimu unaruhusu mtu kujiajiri akimaliza form six. ukienda vodacom customer care unakuta graduates! na pia unawakuta form six, waliotoka international school! kwani wanajua kiingereza!

Hilo PIA LINA WORK KAMA CHUO HAKINA MFUMO WA DISCO,KUWA WEWE SOMA, PIGA KAZI SOMA, ILI MRADI MALIZA CHUO KWA WAKATI WAKO NA TUPE MKOPO WETU. NOT NOW! NOT TANZANIA! NOT WITH THIS KIND OF SYSTEM!!

ebu futa hilo la TV kwanza nione kuwa ngau umesoma vyuo vyetu, kama IFM, MZUMBE, MLIMANI, TUMAINI N.K! kusema wanataka fedha kwa ajili ya TV, ni kukosa la kusema
 
Sasa swali ulilopaswa kujiuliza wewe kama mwalimu ulioona wanafunzi wenye hali ngumu mpaka ukalia ni je, kwa nini wanafunzi wenye hali ngumu wanakubali kugoma kudai kila mwanafunzi apewe asilimia 100 wakati wanajua kuna wenzao wenye uwezo wa kujisomesha. Na kwanini hujiulizi wanafunzi wenyewe kwa wenyewe kwanini wasiripoti hao wanafunzi walioandikwa kuwa wana asilimia 60 na kupewa asilimia 100??? Je kwanini wanafunzi wanaamini in the solidarity ambayo haipo? Kama kuna solidarity basi wale wenye uwezo wasingeenda hata kuomba huo mkopo, Kama kuna solidarity wale waliopewa mkopo mkubwa kuliko mahitaji yao wangeripoti, kama kuna solidarity basi wanaosaliti solidarity wangeshughulikiwa. Ukweli ni kwamba mtu mwenye hali ngumu kama uliyoelezea hapa hawezi kuwa kiongozi wa mgomo hata siku moja. Viongozi wa mgomo huwa ni watu wenye alternatives.

Kuna kijana ninamfahamu alikuwa ana fujo sana shuleni. Alikuwa anaorganise migomo na fujo nyingi tu. Huyu jamaa ni mtoto wa kiongozi wa juu serikalini. Baba yake alikuwa hataki akasome nje ya nchi, sasa jamaa alikuwa anatafuta mbinu za kufukuzwa mlimani ili apate sababu ya kupelekwa kusoma nje!!! Sasa vitu kama hivi ndio hawa wanafunzi wanapaswa kuvitambua. Mtoto wa masikini anapata wapi nguvu ya kukataa kujaza form ya kurudi chuo?? Kwanza ndugu zake watamuelewa?

Kuna jamaa mwingine alikuwa nachukua mkopo bodi na hataki baba yake ajue kama ameomba mkopo, kwa sababu baba yake pia anampa mahitaji yake yote ya chuo. Sasa ni akili gani mnayoitumia kutaka kila mtu apewe asilimia 100?? Wewe kama ni mtetezi wa wanyonge unapaswa kutetea wanyonge wapewe asilimia 100 na ili hilo litokee ni lazima idadi ya wanaopewa mkopo iendane na uwezo uliopo, the best way to cut the number ni kuwatoa wenye uwezo wa kujilipia kwenye mahesabu ya mkopo.

Swala la TV nimetumia kama mfano tu, samahani kama limekuoffend fellow.
 
Last edited:
Back
Top Bottom