Tetesi: Tanzania hatarini kuondolewa AFCON 2025 baada ya kukiuka kanuni za Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)

Bila intelligence taifa huwangamia nakuwa kituko Rais kashatoa 700 mnafanyeje kufuta hili kituko uchawa unauwa Taifa
 
Ile million Mia saba iende kwa waliopata maafa na wananchi wanao hitaji misaada..

Haswaa kabisa basi ikalipie waliojifungua mahospitali ya serikali na kuzuiliwa kutoka hadi walipe bili.
 
yaani aliyefanya hii mistake ni mjinga sana
sasa huyu ni kit manager au?
 
hapo caf labda watumie ubinadamu tu wakienda kwenye sheria tunaliwa kichwa
 
Mtoa mada anavuja..., nikajua tumechezesha raia wa Ghana, au tumechezesha mcheza mieleka ambaye hakusajiliwa katika soka.. kumbe ni mchezaji wetu kabisa jezi namba tu ndo shida?
 
Hao wanataka kulalamika kwa vile Ghana imetolewa. Kanuni hiyo inakataza kutumia acheazji ambao ni "ineligible" yaani hawana sifa kwa maana ya kuwa siyo raia wa nchi husika au walizuiwa kucheza au wale ambao majina yao hayakupelekwa. Haisemi kuwa namba ya jezi atakayovaa itakuwa ni ipi. Wachezaji wote wanaoingia kama subs hukaguliwa uhalali wao na refa wa mezani ndipo anaruhusiwa kuingia uwanjani.
 
Taarifa hii ya TFF haijitoshelezi na haijibu hoja husika

Taarifa hiyo ilitakiwa ifafanunue huyo mchezaji aliyeingia sub alivaa jezi namba ngapi na ndiyo hiyo iliyowasilishwa kwa mamlaka husika kabla ya mechi?
Hawa TFF wajinga sana wanawaona wTZ hamnazo. Shida hapo ni jezi badala ya 24 aliyotakiwa kuvaa Ibrahim Ame amevalishwa jezi namba 26 ambayo haipo kabisa kwenye orodha siku hiyo.

Hii ina maana walichukua mtu toka jukwaani wakamwingiza kucheza uwanjani kwa jina la Ibra Ame.

Wasitufanye wajinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…