Tanzania hatujawahi kulala njaa kwa kukosa mkopo dhidi ya COVID-19, woga na tamaa ndiyo itakayotumaliza

Tanzania hatujawahi kulala njaa kwa kukosa mkopo dhidi ya COVID-19, woga na tamaa ndiyo itakayotumaliza

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
IMF imeitega Tz Kwa kutaka kuipa mkopo wa kupambana na C - 19 na kuielekeza jinsi inapaswa ifanye ili ipewe huo mkopo

Ok, pale mwenye nacho anapotaka kumyang'anya zaidi mwenye kidogo, na Masikini

Mtu jasiri akitaka kurogwa na Mchawi huanza kwa kutishiwa tishiwa, mara sijui kesho hutaiona, mara sijui nitakufanya hiki na kile ili tu amwondolee ujasiri wake, amtie hofu na iwe vyepesi kwake kurogeka.

Maneno meeengi, na kikawaida, mtu hurogeka pindi anapokuwa amejawa na hofu ya kurogwa, hofu ya maisha ya itakuwaje sasa, mtu huyo ni rahisi saana kurogeka.

Kukubali mkopo wa IMF na masharti yake, kisa tu tukabiriane na ugonjwa hewa wa Corona nchini, ni kumruhusu shetani mla watu kwamba, tuko tayari afanye atakavyo kufanya, kwani tnaona huko Kwa wenzetu mambo yalivyo, baada tu ya kutiwa hofu na wakakubali kupewa mikopo hii.

Jambo la kujiuliza, Je, mpaka sasa, ni Kweli Tanzania tumeathirika mno kiasi cha kuhitaji msaada wa kifedha za masharti ambayo ndiyo yanayoambatana na maambukizi ya Corona kwa kasi kubwa?

Tanzania hatujawahi kufa njaa kwa sababu ya kutokukopa fedha za IMF ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Ila nina uhakika, endapo tukikubali kuingia huu mtego wa fedha hizo, Corona itasambaa kwa kasi ya ajabu!

Kwanza, tutakuwa tumefanya uongo Mbele za Mungu kusema, tumeathirika mno na tunahitaji msaada huo na wakati kila kitu Kinafanyika bila zingatio lolote!

Tanzania, Tumepewa nafasi nzuri Sana na Mwenyezi Mungu wa kujifunza kutoka mataifa mengine yaliyopokea misaada hiyo pamoja na kufuata masharti yake jinsi ambavyo watu wake walivyotabika, na bado tumeendelea kujifunza tena Kwa mataifa ambayo yaliyoanza kupokea chanjo.

Kwa hiyo sisi kama nchi, tusiishie tu kupata somo kutoka kwa mataifa mengine na somo Hilo lisitusaidie na kufanya tena kama walivyofanya wao. Itakuwa ni ujinga.

Tunahitaji kufanya tofauti na wao.

Mungu ibariki na kuilinda nchi yetu Tanzania.
 
Huu mkopo hauna tija, dola zaidi ya milioni 500 kupambana na Corona!

Hilo deni linaweza kuwa na athari kubwa kwa nchi kuliko Corona yenyewe. Tusichukue hizo fedha.

Uganda, Kenya wamechukua na 80% imeishia kwa ofisi ya Rais, posho za wabunge nk.

Bora tukope pesa kama hizo tuzipeleke kwenye Kilimo cha kisasa ( umwagiaji, mbegu bora, tractors, mbolea, barabara zinazopitika misimu yote)
 
Mkuu, umesema Jambo la mhimu saana hapa
 
Serikali ya Tanzania kama imeomba huo mkopo tunahitaji kuhabarishwa imeomba za nini? Kama ni za kununua jabs au ndio mwendelezo wa kukinga bakuli wananchi tunahitaji kuambiwa.

Watanzania inahitajika tujitambue tunahitaji nini? Mikopo ambayo wanakula walafi wachache na tija haionekani sio ya kuiendekeza. Tujifunze kutoka kwa awamu iliyopita kuishi bila kukinga bakuli kwa kila kitu. Wenyewe wakiwa na shida wanajikopesha tu na kufikiria kutukamua sisi kama ng'ombe.
 
Tunafungua Duka wakat wenzetu wanakaribia kufunga maduka

Nilisema hapa kuwa hayo barakoa wanayovaa kuna kitu nyuma yake tuendelee kula mtori nyama zipo chini leo wavuja jasho watakuja kulipa deni la mikopo ya Corona ambao hauexit ktk maisha yetu, Tanzania yapo magonjwa ambayo yanasumbua kama Maralia,Kansa na mengine si Corona

Inasikitisha sana kufanya kazi na mtu ambae yupo pale kwa mshahara na cheo lakini Ideology yako haiamini naona umuhimu wa katiba mpya na baadhi ya vyeo vitolewe tu coz baadae vinaweza kuleta hatari ikitokea mtu ambae si mwaminifu na mroho wa madaraka
 
Mtu jasiri akitaka kurogwa na Mchawi huanza kwa kutishiwa tishiwa, mara sijui kesho hutaiona, mara sijui nitakufanya hiki na kile ili tu amwondolee ujasiri wake, amtie hofu na iwe vyepesi kwake kurogeka.

Maneno meeengi, na kikawaida, mtu hurogeka pindi anapokuwa amejawa na hofu ya kurogwa, hofu ya maisha ya itakuwaje sasa, mtu huyo ni rahisi saana kurogeka

Kukubali mkopo wa IMF na masharti yake, kisa tu tukabiriane na ugonjwa wa Corona, ni kumruhusu shetani mla watu kwamba, tuko tayari afanye atakavyo

Jambo la kujiuliza, Je, mpaka sasa, ni Kweli Tanzania tumeathirika mno kiasi cha kuhitaji msaada wa kifedha za masharti ambayo ndiyo yanayoambatana na maambukizi ya Corona kwa kasi kubwa?

Tanzania hatujawahi kufa njaa kwa sababu ya kutokukopa fedha za IMF ili kukabiliana na ugonjwa wa Corona.

Ila nina uhakika, endapo tukikubali kuingia huu mtego wa fedha hizo, Corona itasambaa kwa kasi ya ajabu!

Kwanza, tutakuwa tumefanya uongo Mbele za Mungu kusema, tumeathirika mno na tunahitaji msaada huo na wakati kila kitu Kinafanyika bila zingatio lolote!

Tanzania, Tumepewa nafasi nzuri Sana na Mwenyezi Mungu wa kujifunza kutoka mataifa mengine yaliyopokea misaada hiyo pamoja na kufuata masharti yako jinsi ambavyo watu wake walivyotabika, na bado tumeendelea kujifunza tena Kwa mataifa ambayo yaliyoanza kupokea chano, Kwa hiyo Sisi kama nchi, tusiishie tu kupata somo na lisitusaidie na badala yake tufanye kama walivyofanya wengine.

Tunahitaji kufanya tofauti na wao

Mungu ibariki na kuilinda nchi yetu Tanzania
Huu mkopo hauna tija, dola zaidi ya milioni 500 kupambana na Corona!

Hilo deni linaweza kuwa na athari kubwa kwa nchi kuliko Corona yenyewe. Tusichukue hizo fedha.

Uganda, Kenya wamechukua na 80% imeishia kwa ofisi ya Rais, posho za wabunge nk.

Bora tukope pesa kama hizo tuzipeleke kwenye Kilimo cha kisasa ( umwagiaji, mbegu bora, tractors, mbolea, barabara zinazopitika misimu yote)
Wabongo kwa kupiga domo hatujambo. Midomo kama tarumbeta.

Kwanza tangu lini Tanzania imewahi kuchukua mkopo na kufanyia kile ilichoombea?

Hata kwenye maisha binafsi huwa tunadanganya bank zitukopeshe kwaajili ya matibabu lakini tunaenda kuhonga.

Magufuli alichukua pesa za athari za COVID-19 kutoka UMOJA wa ULAYA. Alichukua pesa za nini wakati alisema hatuna CORONA ?

Na hizo pesa alifanyia nini !

Vile vile, Magu alipiga marufuku wanafunzi watakaopata ujauzito kuendelea na masomo lakini pesa za elimu yao kutoka WORLD BANK alizitaka kwa nguvu zote mpaka kufikia kina Zitto kutishiwa maisha.

Sasa hizo pesa alipeleka wapi ???
 
Umasikini ni kitu cha kupiga vita saana, Kilichofanywa na IMF ni kutupaka utamu mdomoni ili kuona kama tutaweza kuishinda tamaa ya chakula hicho

Lakini, ukweli wake ni kwamba, mikopo yote iliyotolewa Kwa kusudi la kupambana na Corona, ni kama ilikuja kusambaza Corona Kwa Kasi katika nchi husika
 
Kwanza, tutakuwa tumefanya uongo Mbele za Mungu kusema, tumeathirika mno na tunahitaji msaada huo na wakati kila kitu Kinafanyika bila zingatio lolote
Kwani tuseme mala ngapi uongo ndiyo uwe uongo tumedanganya vya kutosha kua hatuna tatizo huku watu wakiathilika na gonjwa wengine wakipoteza bahati ya kuishi turuhusu na akili zetu alizotujalia mola zifanye kazi ya kutushauri Nini Cha kufanya hakuna atakaye tupigia ramli ya maisha yetu yako mkononi mwetu uongo hua ni mfupi
 
Mkuu, unadhani endapo tutakopa hizi dollar milioni 500+ hazitakuwa Mali ya wachache kweli, lakini Je, ni kweli Tanzania tunatishio kuubwa Sana la Corona?
 
Mkuu, unadhani endapo tutakopa hizi dollar milioni 500+ hazitakuwa Mali ya wachache kweli, lakini Je, ni kweli Tanzania tunatishio kuubwa Sana la Corona?
Hukumsikia waziri wa maliasili na utalii jinsi utalii ilivyo shuka hiyo Sio athari jiulize he mapungufu ya makusanyi hayo yatazibikaje leo tunamashaka hujiulizi t 70 zimefikaje?
 
Zile njia za juu pale Ubungo zimejengwa na kwa pesa ya benki ya dunia. Na miradi mingine mingi tu inajengwa kwa pesa za wazungu.

Tusitake kumuonea Rais Samia kwa kumjazia nongwa kisa kikiwa COVID 19 wakati aliyemwachia ofisi alikuwa ni fundi wa kuchukua pesa hizi hizi za wazungu.

Kuongoza nchi ni kazi kubwa sana tofauti na wengi tunavyodhani.
 
Kuongoza nchi ni kazi ndoogo Sana mkuu, ni kuiruhusu pua yako iwe inanusa tu na masikio yako usiyawekee pamba basi!!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Kwa hiyo maisha yetu siku zote ni feki,

Tunaishi Kwa uwongouwongo tu, siyo, basi nchi yetu ni Taifa la Aina yake!
Hata leo inasomwa bungeni budget feki.

Upatikanaji wa pesa utategemea makusanyo, siasa, mikopo na misaada.

Pesa zinaweza kupelekwa sehemu ambayo hata haikupangiwa budget.
 
Magufuli alichukua pesa za athari za COVID-19 kutoka UMOJA wa ULAYA. Alichukua pesa za nini wakati alisema hatuna CORONA ?

Na hizo pesa alifanyia nini !
Athari za covid-19 zimewafikia hata wale ambao hawakuathirika sana na huo ugonjwa.
 
Back
Top Bottom