Tanzania hatuna Comedians bali tuna waropokaji tu. Comedians wa Kitanzania humwelewi kama hujui lugha anayotumia jukwaani

Tanzania hatuna Comedians bali tuna waropokaji tu. Comedians wa Kitanzania humwelewi kama hujui lugha anayotumia jukwaani

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Kwa hakika siwezi kupoteza muda wangu au data kumtazama mchekeshaji wa Kibongo. Hawa wachekeshaji wetu mimi ninawaita waropokaji.

Comedy ya wenzetu wengi utacheka na kufurahi hata usipoielewa lugha wanayoitumia jukwaani.

1. Comedy ya Kibongo imekosa ubunifu.

2. Wanadhani mpaka leo mavazi yanaweza kumchekesha mtu.

3. Komedi ya Bongo ni kwa Watanzania tu kwani inabeba mazingira ya Kibongo tu.

4. Imejaa kelele(uropokaji) tu haijulikani inahusu nini.

Hebu cheki hii clip chini ujionee comedy ya wenzetu.
 
Mimi sikuwepo na sijatazama kwenye runinga ile shughuli.
Tangu kitambo nilijua kuwa Masanja hajui comedy sema tu anaishi kwa ngekewa. Si unajua Bongo kujuana na ngekewa ndio kila kitu.
Original komedi ilikuwa overated sana enzi zile
Achana na hiyo clip kwanza, hebu tuwekee na ya Masanja ile juzi akiwa anaongea mashudu mbele ya halaiki kubwa kama ile...
 
Kwa hakika siwezi kupoteza muda wangu au data langu kumtazama mchekeshaji wa Kibongo .
Hawa wachekeshaji wetu mimi ninawaita waropokaji.
Comedy ya wenzetu wengi utacheka na kufurahi hata usipoielewa lugha wanayoitumia jukwaani.
1. Comedy ya Kibongo imekosa ubunifu.
2. Wanadhani mpaka leo mavazi yanaweza kumchekesha mtu.
3. Komedi ya Bongo ni kwa Watanzania tu kwani inabeba mazingira ya Kibongo tu.
4. Imejaa kelele(uropokaji) tu haijulikani inahusu nini.
Hebu cheki hii clip chini ujionee comedy ya wenzetu.
View attachment 2040040
Hapo kwenye uvaaji matambara na manguo makubwa umepigilia msumari! Comedy ya kitanzania lazima wanaume wenye ndevu zao wavae kama wanawake na waweke matambara makalioni!!!
 
Lakini Joti anajitahidi sana ukweli usemwe,
Hao wengine sijaona ila kwa Joti angalau anaweza kukufanya ucheke, napenda anavyoweza kubadilika badilika kuanzia Mtoto, kijana mtukutu, kijana wa makamo, dada wa mjini hadi mzee kikongwe,

I love that.
 
Bongo mtu akiongea upuuzi kuanza kuitwa comedian ni swala la muda tu.

Na akiwa ana sura mbaya au hana meno au disability usishangae kuona anakua comedian.

Kuna video ya jamaa anasema asiposhika milioni kumi atachukua mjegeja na kuanza kutembeza za kichwa.

A month later a nigga hasi his own IG page and he introduces himself as a comedian. Na watu wamempokea.

Mama wa 'Ukorofi' netizens waliforce apokelewe kama comedian ila naona yeye hajachagua route hiyo.

Ambacho watu hawajui ni kwamba ni ngumu mno kucreate content, so mtu akibahatisha aina fulani ya content hapa ndo kama yule jamaa aliyekua anachukua video anakimbia, na kama mkojani, na ikakubali anajikuta anastuck hapo na anai-over exploit mwisho inakua miyeyusho.
 
Mimi kwenye standup comedy namkubali Deogratius.
Yule nakubali anavyojua kuunga matukio halafu yaka make sense. Standup comedy lazima ujue lugha inayozungumzwa ndo utaelewa. Hata akina Kelvin Hart au Basket Mouth kama hujui lugha huwezi kucheka kwakuwa hutoelewa.
Mimi naenjoy zaidi standup comedy.
 
Mimi sikuwepo na sijatazama kwenye runinga ile shughuli.
Tangu kitambo nilijua kuwa Masanja hajui comedy sema tu anaishi kwa ngekewa. Si unajua Bongo kujuana na ngekewa ndio kila kitu.
Original komedi ilikuwa overated sana enzi zile

Nilitazama hiyo scene Youtube, na imewekewa title kubwa, "Masanjamkandamizani amvunja mbavu Rais Samia"...

So i was attracted...utopolo nilioukuta huko aibu tupu...

Lakini Joti anajitahidi sana ukweli usemwe,
Hao wengine sijaona ila kwa Joti angalau anaweza kukufanya ucheke, napenda anavyoweza kubadilika badilika kuanzia Mtoto, kijana mtukutu, kijana wa makamo, dada wa mjini hadi mzee kikongwe,

I love that.

Hata mama ima yupo vizur kias anachekesha
 
Starter pack ya comedian wa kibongo;

Kuvaa nguo za kike.
Kubadilisha sauti, kuongelea puani.
Kujifanya hamnazo.
Kuropoka ovyo.

Wakishapata umaarufu kidogo kama Mpoki ni kuanza kutukana watu kwa kisingizio cha kuchekesha.

Waliopata exposure kidogo, kama Idris Sultan wao hujichekesha wenyewe kwa kuongea upumbavu usiochekesha.

In short ma comedian wa kibongo wana mwendo mrefu mno mpaka kujua maana halisi ya comedy.
 
Back
Top Bottom