Tanzania hatuna shule inayovaa sare ya aina hii. Acheni kuichafua na kuipaka matope Serikali yetu iliyojenga madarasa bora mpaka vijijini huko

Sio kweli.Hata wewe na mwingine mnajukumu la kuchangia.
 
Kwa hiyo wewe hujiamini kuwa ni Mwanaume? Au ni mpaka ujitangaze kuwa wewe ni mwanaume kama matangazo ya waganga wa kienyeji mitaani? Kwani watu hawafahamu kuwa wewe ni mwanaume? Au huwa wanakwambia wewe ni mwanamke?
Ding angepizi out tuuu hii shida isingekuwepo.
 
Sio kweli.Hata wewe na mwingine mnajukumu la kuchangia.
Jukumu la kulipa kodi.
Jukumu la kuchangia sungusungu.
Jukumu la kuchangia takataka.
Jukumu la kuchangia ujenzi wa barabara.
Jukumu la kuchangia ujenzi wa zahanati.
Jukumu la kuchangia madawati.

Ninapolipa kodi,tozo na makato mbalimbali kwenye mauzo,manunuzi na shughuli zangu, hiyo hela inaenda fanya nini mpaka nipewe majukumu mengine hayo niliyoyaorodhesha!!?

Kila sehemu penye shughuli yangu ya kiuchumi, huwa natoa CSR, pamoja na kulipa kodi na tozo mbalimbali kulingana na shughuli husika.
 
Unaposema wajibu unamaanisha nini? Kwani Nchi ngapi zimeshindwa kutimiza wajibu wao? Kwanini usipongeze kwa kazi nzuri iliyofanywa na serikali yetu?
Kodi, kodi, kodi, kodi, tax payers,tax payers,tax payers, ndio wenye kustahili pongezi
 
Kukosoa na kupongeza vyote viende sambamba

Shida ni wewe, kazi yako wewe ni kupongeza tu na hukosowi

Kwa nini unawakasirikia wanaokosoa?

Wewe sitiki kwenye eneo lako la kupongeza, waache wanaookosoa nao waendelee
Mjinga huyo analazimisha wote tuwe machawa
 
Kwani Nchi ambazo wanafunzi wao wanakaa chini na kukosa madarasa na huduma zingine.Je wao hawakusanyi kodi? Tujifunze kupongeza pale serikali inapofanya vizuri.
Kwani serikali ni nini? Na kuna aina ngapi za serikali?
Pia usisahau biashara inayofanya serikali hata kupata ili ajifunze kuisifia.
 
Mjinga mmoja wewe Kuna Mhadhiri msaidizi wa chuo x alitembelea shule x Kwa ajili ya asesment ya wanafunzi wa field akapiga picha mazingira kikichomkuta ni historia. Na waliomganyia hayo ni watu wa aina Yako bumunda wewe Karne ya 21 unajisifia matundu ya choo yalojengwa Kwa msaada
Wewe ndiye useme ni ya Nchi gani,mkoa gani,wilaya gani,kata gani,kijiji au mtaa upi na jina la shule ni lipi . Na siyo kuweka vipicha vya mitandaoni
 
Jibu swali hili kama una akili Timamu. Ni shule ipi ya msingi ya serikali wanaovaa sare aina hiyo hapa Nchini Tanzania?
 
Swala la shule inaitwaje , wilaya gani na mkoa gani haliendani na kichwa Cha habari Cha Uzi wako bwana Lukas.
Sasa je kwa hizi picha nilizoleta hapa kwa rangi za sare zilizopo kwenye picha ke, hizo shule ziko Tanzania au ni nchi za nje?!
 

Attachments

  • wanafunzi darasani.JPG
    25.9 KB · Views: 2
  • images(198).jpg
    12 KB · Views: 1
  • images(195).jpg
    58.3 KB · Views: 2
  • images(190).jpg
    32.8 KB · Views: 2
  • images(187).jpg
    8.9 KB · Views: 1
  • images(191).jpg
    40.5 KB · Views: 1
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…