Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kuna kijana kwenye mtandao wa kijami ameibua mjadala ambao nimeusikia na Clouds kwamba Tanzania kuna tabia iliyoota mizizi ya ya raia kujichukia sana(self-hate mentallity). Mifano yake aliyotoa sasa kwamba tuko vizuri ndio imenichekesha anazungumzia SGR, movie ya Idriss Sultan huko Netflix, miziki ya Diamond na mambo ya startups!
Hivi kweli sisi Tanzania ndio wa kujivunia hizi peanuts, yani Tanzania yenye rasilimali na jiografia tuliyo nayo leo baada ya miaka 60 ya uhuru ndio tujivunie hivi tuvitu?!
Tuache upotoshaji na uchawa usiotusaidia bali wenye kuzidi kutudumaza, bado tuko nyuma sana ukilinganisha na ukwasi wa rasilimali tulizo nazo, hali ya hewa na jiografia ya kikanda, tusifarijiane kwamba eti angalau tuna kidogo na wengine hawana, hiyo mitazamo ya Kiswahili itazidi kutudumaza.