Tanzania hatuna wachekeshaji bali tuna waropokaji, wengi ni kinyaa kuwatazama

Tanzania hatuna wachekeshaji bali tuna waropokaji, wengi ni kinyaa kuwatazama

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,943
Mimi ni mpenda comedy sana hasa za nje. Awali nilikuwa nikizitazama hizi za Bongo za kina Kingwendu, Majuto n.k lakini sasa natazama za nje za kina Charlie Chaplin, Buster Keaton na wengine walio hai.

Ukitazama comedy ya MC Pilipili utagundua kuwa uropokaji ndio aliojaaliwa. Akina Kingwendu pia ndo walewale maneno mengi.

Comedy za bongo hovyo sana, wengi hawana vipaji na kazi zao hazina hata uwezo wa kushindana na soko la miaka hata 25 tu ya mbele.

Akina Tiny white, Erick, Kitale, Ringo hamna kitu.
Maufundi unakuja vizuri.
 
Mc Pilipili kwanza yeye mwenyewe ni kichekesho tu yaani ukifikiria nachofanya unacheka. HAKUNA KITU.

MPOKI: Hakuna kitu huyu ni kuongea tu kama mvuvi haramu.

JOTI: Huyu kabaki kujigeuza tu jinsia.

MAJUTO: Ulale salama ila yeye alikuwa ni kucheka badala ya kuchekesha.

MR BEAN: Huyu kazi kukodoa tu.

Chalie Champlin: Pumzika kwa amani mfalme wa VICHEKESHO.
 
mlevi piere anachekesha natural tu bila kufosi.. joti nae anachekesha sana .. japo kama hayupo serius sana now days

mc pilipili anatumia nguvu sana ila bado hucheki...

kuna watu wengi sana walazimisha kuchekesha watu...

now days nikitaka kucheka namwangalia piere tu...
 
Back
Top Bottom