Tanzania hatuna wachekeshaji bali tuna waropokaji, wengi ni kinyaa kuwatazama

Tanzania hatuna wachekeshaji bali tuna waropokaji, wengi ni kinyaa kuwatazama

Wachekeshaji wapo ila hii sanaa imevamiwa na watu wenye njaa kali lengo lao wapate vijitangazo vya kwenye Instagram wapate pesa ila hawana vichekesho vinavyo weza dumu miaka kadhaa mbele

Sent using Jamii Forums mobile app
 
List yangu ya wachekeshaji (1)Msukuma akiwa bungeni(2)Muroto akiwahoji watuhumiwa na kuwahukumu live mbele ya wahandishi wa habari(3)Bashite akiangua kilio kanisani.
 
Ndio uwezo walio nao na hapo ndipo walipofikia, sasa wafanyeje?
 
Kamtafute mtu anaitwa Deogratius wa cheka tu ndo utajua wapo au hawapo jamaa talented sana.
Huyo pipipili hamna kitu.

Mr Romantic

Pilipili ninachoona kazi yake ni kutusi watu na kujisifia kuwa ana PRADO basi. Deogratius namkubali sana. Wenzetu wa Kenya wapo mbali sana. Uganda yupo mmoja anaitwa Salvador huyo ni mkali sana.
 
Wabongo stand up comedy bado sana, bora hata Cheka tu kidogo wanajitahidi ambako Deogratious na Nalimi nawaelewa sana, ila pilipili yule jamaa chenga sana kuchekesha ni ziro kabisa, ndo maana wajanja tunaangalia Churchill ya kenya kule Kuna jamaa anaitwa YY ni shidaa
Kuna Pastor kuria "Man Kushi", Mammito, profesa Hammo, Tricky Sana.... nawakubali sana jamaa wa churchil show
 
Kweli kabisa Kiongozi Jamaa wale ni talented sana halafu ni wabunifu sana..wametuletea ladha mpya ya komedi tofauti na ile tuliyozoea (mf. Bambo, Kingwendu, kiwewe n.k).Comedians wengi bongo ni wapiga zumari tu hamna kitu.
Hao jamaa wa Jambo na Vijambo wapo Chennel gani asee? Muda gani? Zamani nilikuwa nawaangalia EATV, Sasa siku hizi siwaoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unafiki pembeni, wale jamaa wa "JAMBO NA VIJAMBO" Wanajua sana. Kibongobongo nawakubali sana wale raia.....Kwa malegendari, Joti yupo juu.

Kinachowabeba jamaa ni ubunifu pamoja na kipaji cha hali ya juu kila mtu akiuvaa uhusika fulani anaweza kuutendea kazi mfano jamaa wa maneno kumi akiwekwa avae uhusika wa utoto aisee utacheka utake usitake, bado cha uroho na jamaa mwenye misemo na misamiati anayeigiza mithiri ya Yesu. Hawakulazimishi kucheka ila utacheka tu. Na pia wamebeba maudhui ya kuelimisha jamii pia. Kwa Tanzania hawa jamaa wapo vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom