Tanzania huenda ikatuchukua karne nzima kumpata Rais Samia mwingine

Mkuu watumishi tumepandishwa madaraja. Ila aturudishie Mchengerwa wizarani.
 
Mmeanza tena 🤣🤣🤣!!! Yaan uchawa bas tu!

 
Angekuwa mzuri zaidi angepunguza uwoga, angejiamini mwenyewe na angehakikisha anapenda haki,na kujiridhisha kuwa anachokosema amekifanyia utafiti. Angalia kesi ya Mbowe kadanganywa na kadanganyika, eti wenzie Mbowe walishafungwa akina Nani hai! Mkuu wa nchi mwenye vyombo vyote chini yako unafanganywa? Amesema Kuna 2025 fever inawasumbua wasaidizi wake mawaziri nitawatoa waende wakaendelee na 2025 election,angalia waliotolewa sijui Nani kati yao amewahi hata kuchukua fomu ya kugombea urais,unafanya mabadiliko mwenyewe halafu unashangaa mwenyewe,eti hawa sijawatoa watakuwa wasaidizi wangu Ikulu japo kazi zao hazipo kwenye utaratibu eeh!! Mbona wenzake wakimuhitaji mtu walimwita waziri asiye na wizara maalum basi! Hivyo,Kama kweli anataka legacy nzuri Ni kurekebisha hizo kasoro, Mzee Mwinyi,mchakato wa vyama vingi ulianzia kwake, kabla hata ya marekebisho ya katiba kuruhusu huo mchakato lakini watu walikuwa na vikao vya mchakato huo na Hakuna kupigwa mabomu,au kuwekwa ndani kwani Nini kilitokea? Mbona nchi ilitulia tu! Wamepita kina Mtikila na kudai Tanganyika, walisema mpaka kuuza Kanda za hotuba zao kwani kina madhara yaliyotokea zaidi ya kasoro ndogo ndogo tu. Lakini wenzake pamoja na kasoro zao waliheshimu Sana nafasi ya mihimili mingine. Nyerere na ubabe wake aliheshimu Sana uhuru wa mahakama,hata marehemu Francis Nyalali aliwahi shuhudia kuwa aliwahi kumhukumu kifungo mtu akiwa Hakimu wa Wilaya ya Musoma ambaye ni jamaa wa Nyerere, matokeo yake Nyerere alimheshimu mno. Mh. Jaji Warioba uchaguzi wa ubunge Mwaka 1990,ushindi wake ulitenguliwa na Jaji Mfalila pamoja na sifa ya kuwa alikuwa waziri mkuu na makamu wa kwanza wa Rais. Niishie Happ nampenda Sana japo natamani afanye vizuri kwa maoni yangu akirekebisha. Labda pengine wengi humu mlikuwa wadogo,Ni uhuru wa vyombo vya Habari. Kesi ya uhaini ya 1982 au 1983 hakukuwa na luninga wakati huo,lakini tulipata kila kitu kilichoendelea mahakamani utadhani tulikuwepo, kumbuka Ni utawala wa Nyerere wakati lakini hakuingilia uhuru wa waandishi wa habari japo karibu wote walikuwa ni watumishi wa serikali. Pamoja na udhaifu wa katiba yetu, Utashi wa mtu ni muhimu Sana.
 
Makamba bwana
 
Natamani Rais mwenyewe angesoma hili andiko,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…