Tanzania huenda ikatuchukua karne nzima kumpata Rais Samia mwingine

Kazi ni nzuri sana ya mama
 
Nchi inayoendeshwa bila kufuata miongozo ya katiba unaweza kutana na tafakuri kama hizi ! Tatizo si kumpata Raisi kama huyu tatizo ni dira ya taifa ya namna ya kuendesha nchi kwa muda mrefu wakati Tanzania inakuwa inaanza upya kila kitu kila baada ya miaka mitano ya uchaguzi nchi zilizoendelea zinafanyia kazi mipango iliyowekwa miaka 100 nyuma ambayo hata wanaoongoza nchi hizo hawakuwepo!

chama cha Mapinduzi kimeongoza nchi hii tangu uhuru lakini kimeshindwa kabisa kumaliza matatizo ya kawaida tu kama maji ,umeme ,matundu ya vyoo shuleni na madarasa kwa miaka yote kuna sehemu hazina hata madaraja ya kuunganisha vijiji

Kila mwaka fedha inayotajwa kupotea kwa mujibu wa ripoti za CAG zingeweza kumaliza matatizo hayo mojamoja kwa nyakati lakini ni ndoto !

Huenda huyu akawa asipatikane tena kwa sababu ameweza kuitumbukiza nchi kwenye matatizo makubwa ya kimikataba kuliko watangulizi wake kinachotumika na kuonekana kwa macho huenda ni robo tu ya kile kinachoibwa na kufujwa hakuna jipya pombe mpya kikombe cha zamani
 
Inategemea unamfananisha nani but yoote hayo nimambo yakawaidaa saana nikama ujisifu kwawatu kuwa
1.) Huwa unatawaza
2.) Unapigaga mswaki
3.) Unakulaga misosi
4.) Unalalaga kitanda NK. NK.
Sasa Acha ujinga na uchawa rais mbunifu na anayeasisi mambo yasiyo ya kawaida ndiyo tunamhitaji siyo anayechkua Kodi Yako akanunua CT scan unasifu...jinga wewe...
Maeneo nyeti yakusifu
1.) ELIMU - Aifumue na kuiunda upyaa Toka primary mpaka chuo iendane na Dunia yaleo.
2.) NISHATI - Sio kutupiga siasa umeme mwingi wauhakika kushawishi uwekezaji...tunaimba tuu Nyerere dam miaka inasonga
3.) DEMOKRASIA - Tume huru,katiba Bora na haki na usawa katika vyama vya siasa.
4.) AFYA - Huruma Bora na nafuu,dawa beinzuri,upatikanaji wa madaktari wengi na mabingwa sio nchi nzima mabingwa hawafiki aftatu.
5.) AJIRA - Viwanda vidogo vidogo vyamaana kupitia veta,Sido na teknolojia yamaana kufundishwa huko
6.) KILIMO - Chakisasa kisitegemee mvua Bali umwagiliaji,ufugaji wakisasa ngazi za wilaya sio vijikundi vyabashe vyakisiasa.
7.) USAFIRI - Mwambie bado kunavijiji wanaozewa namazao huku kunamasoko mazao hayo hayanunuliki humuhumu ndani ya nchi kisa hakuna USAFIRI.
8.) TAASISI IMARA - TAASISI nyingi ni hovyo na Zina underperform kuanzia BUNGE,mahakama,mabenki,TANESCO,MAJI,TAKUKURU,tanapa,Tcra,Nida taaaja mpaka uchoke maana nikaribu zooote...nchi ni mifumo na TAASISI zake ziwe imara.
Mwambieni aanze nahivyo vichache muache kumsifu kipumbafu Kila anapogusa pitty issues malofa ninyi
 
Chawa hizi akili hawawezi kua nazo.hongera sana kwakuweka mambo ya msingi kwa njia rahisi inayoeleweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…