Tanzania huwa kuna shida gani katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri?

Mteuaja anaa galia zaidi manufaa yake binafsi
 
Naunga mkono hoja, ni kama ulikuwa kwenye akili yangu,niliwaza sana kuhusu hilo. Katika Africa hasa hasa ni hizi ahadi kabla ya uchaguzi "nikienda ofisini nakuahidi uwaziri hata kama ni boya".
 
Mtendaji mkuu wa wizara ni Katibu mkuu wa wizara sio waziri. Uwaziri ni cheo cha kisiasa. Waziri hawezi hata kuandika barua ya kuajiri watu
 
sio lazima waziri awe mjuzi wa sekta hiyo,kwani wapo waajiriwa wa serikali kwenye wizara hiyo ndio watendaji na ni mabingwa wa sekta hiyo,waziri ni political figure
 
Urafiki na nasaba, badala ya uwezo
 
uwaziri ni cheo cha kisiasa, sasa wapewe nani mwengine?
Hapo hapo kwenye cheo cha kisiasa kwani hakuna wanasiasa wenye taaluma zinazoendana na nafasi wanayoteuliwa?

Kwamba hakuna mbunge ambaye ana fani ya udaktari akapewa nafasi ya waziri wa afya?
 
Hapo hapo kwenye cheo cha kisiasa kwani hakuna wanasiasa wenye taaluma zinazoendana na nafasi wanayoteuliwa?

Kwamba hakuna mbunge ambaye ana fani ya udaktari akapewa nafasi ya waziri wa afya?

Lakini bado anabaki kuwa mwanasiasa, malalmiko yenu ni kuwa hamtaki wanasiasa kwenye uwaziri, wakati vyeo vya uwaziri ni vya kisiasa.
 
Tuiombe Mamlaka ya uteuzi ifanye mabadiliko katika Wizara ya Fedha.
 
Lakini bado anabaki kuwa mwanasiasa, malalmiko yenu ni kuwa hamtaki wanasiasa kwenye uwaziri, wakati vyeo vya uwaziri ni vya kisiasa.
At least atakuwa na uelewa wa mambo yanayohusiana na wizara yake hata ufuatiliaji hautakuwa mgumu kama asingekuwa na taaluma husika.

Mtu asiye na taaluma ya wizara husika kudanganywa ni rahisi zaidi kuliko mwenye ubobevu wa taaluma husika.
 
Dr Jenister Mhagama(Diploma in Education)!
Hii kitaalamu tunasema,"ungaunga mwana tusonge"!
 
Mie nauliza kwann ile sheria ilipelekwa jeshi lisikaguliwe na CAG manake we pay taxes and they get paid to save our country pesa wanazolipwa zinatokana na kodi zetu why wasikaguliwe??????
 
Mtendaji mkuu wa wizara ni Katibu mkuu wa wizara sio waziri. Uwaziri ni cheo cha kisiasa. Waziri hawezi hata kuandika barua ya kuajiri watu
Waziri ni msimamizi Mkuu wa sera katika sekta husika na Katibu Mkuu ni Mtendaji na msimamizi wa utumishi Wizarani.
 
Ndiyo maana mambo mengi hupindishwa kwa kivuli cha alishauriwa vibaya... Umenena vyema na wenye akili wataelewa, huwezi simamia sector/wizara kwa ufasaha ambayo ww mwenyewe huijui vyema structure na mianya yake
 
Makatibu wakuu wasimamie Wizara. Wabunge wabaki bungeni wasimamie serikali
 
Kwanza wawe makada wa chama ndo kipaumbele cha kwanza. Na makada wengi elimu sufuli au ya kuugauga, kazi wanazo weza ni uchawa
Wewe jenista ana masters Cambridge 😁😄 nimecheka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…