The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Tanzania ni nchi yenye potential kubwa ya deposit ya makaa ya mawe kwenye mikoa ua Mbeya, Ruvuma, njombe na Mtwara na maeneo ya kanda ya ziwa.
Makaa ya mawe ni chanzo cha kuaminika cha uzalishaji umeme, umeme usioyumba yumba kama wa maji ama upepo ama jua.
Tanzania inaweza kuzalisha umeme zaidi ya megawati 2000 kwa makaa ya mawe iliyonayo kwa miaka mingi sana na kuhakikisha upatikanaji wa nishati kwa maendeleo ya kiuchumi.
Tanzania inatakiwa ichukue maamuzi magumu ianze kujenga kinu cha kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe. Tanzania inabidi ifanye maamuzi magumu kama yaliyofanyika kwenye kujenga bwawa la mwalimu Nyerere.
IMF na World bank ndio wanaikataza Tanzania isijenge umeme wa makaa ya mawe kwa kigezo cha uchafuzi wa mazingira. Kumbuka WB na IMF hawataki Tanzania inenge mradi mwingine wa umeme kwa kutumia maji, wanasema ni uchafuzi wa mazingira. WB na IMF wameitaka Tanzania iondoe mpango wa kujenga umeme wa makaa ya mawe kwenye mipango yake na wanalazimisha Tanzania ijikite kwenye umeme wa sola na jua(Renewable Energy).
Jamaa hao pamoja na unafiki wao wa kwamba makaa ya mawe yanachafua mazingira lakini wao kwenye nchi zao wanazalisha umeme kwa makaa ya mawe na ndio wanaonunua makaa ya mawe kutoka Tanzania (bandari ya mtwara iko busy kila siku kusafirisha makaa ya mawe kwenda ulaya kuzalisha umeme)
Wakati WB na IMF wanaikataza Tanzania, South Africa iinajenga kinu cha makaa ya mawe cha kuzalisha megawati 4800, Kusile Power Plant Mpumalanga.
Tanzania ifanye maamuzi magumu, ijenge kinu cha makaa ya mawe kuzalisha umeme, iachane na mikara ya wb na imf.