Tanzania ichukue maamuzi magumu ijenge kinu cha kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe

Tanzania ichukue maamuzi magumu ijenge kinu cha kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe

Tanzania ni nchi yenye potential kubwa ya deposit ya makaa ya mawe kwenye mikoa ua Mbeya, Ruvuma, njombe na Mtwara na maeneo ya kanda ya ziwa.

Makaa ya mawe ni chanzo cha kuaminika cha uzalishaji umeme, umeme usioyumba yumba kama wa maji ama upepo ama jua.

Tanzania inaweza kuzalisha umeme zaidi ya megawati 2000 kwa makaa ya mawe iliyonayo kwa miaka mingi sana na kuhakikisha upatikanaji wa nishati kwa maendeleo ya kiuchumi.

Tanzania inatakiwa ichukue maamuzi magumu ianze kujenga kinu cha kuzalisha umeme kwa makaa ya mawe. Tanzania inabidi ifanye maamuzi magumu kama yaliyofanyika kwenye kujenga bwawa la mwalimu Nyerere.

IMF na World bank ndio wanaikataza Tanzania isijenge umeme wa makaa ya mawe kwa kigezo cha uchafuzi wa mazingira. Kumbuka WB na IMF hawataki Tanzania inenge mradi mwingine wa umeme kwa kutumia maji, wanasema ni uchafuzi wa mazingira. WB na IMF wameitaka Tanzania iondoe mpango wa kujenga umeme wa makaa ya mawe kwenye mipango yake na wanalazimisha Tanzania ijikite kwenye umeme wa sola na jua(Renewable Energy).

Jamaa hao pamoja na unafiki wao wa kwamba makaa ya mawe yanachafua mazingira lakini wao kwenye nchi zao wanazalisha umeme kwa makaa ya mawe na ndio wanaonunua makaa ya mawe kutoka Tanzania (bandari ya mtwara iko busy kila siku kusafirisha makaa ya mawe kwenda ulaya kuzalisha umeme)

Wakati WB na IMF wanaikataza Tanzania, South Africa iinajenga kinu cha makaa ya mawe cha kuzalisha megawati 4800, Kusile Power Plant Mpumalanga.

Tanzania ifanye maamuzi magumu, ijenge kinu cha makaa ya mawe kuzalisha umeme, iachane na mikara ya wb na imf.

Mtu wa kufanya maamuzi magumu bila kupepesa macho alitangulia mbele ya haki. Na alifanya kwa manufaa ya nchi.

Ukiona mnyukano wa kutafuta madaraka na dola, unajiuliza ni kwa maslahi ya nani. Ukishajua ni kwa maslahi ya nani, then utajua hakuna kitu kama hicho.

Ili kupata maendeleo, lazima kuwe na watu wabishi, ambao wako tayari kukataa the existing status quo. Nani kama hao? Kweli wapo? Wako wapi?

Otherwise tuendelee kufanya siasa zetu ambazo mpaka tukaroge ndio tunaona tuko sawa
 
Tanzania ifanye maamuzi magumu, ijenge kinu cha makaa ya mawe kuzalisha umeme, iachane na mikara ya wb na imf
Ni Magufuli tu, angeweza kufanya hivyo. Siyo hawa walio baki.

Pamoja na kuungana nawe katika hilo, pia usisahau tunayo uraniaum nyingi tu.
Ingefaa tuanze mikakati ya kujenga kinu cha kuzalisha umeme wa 'nuclear'. Sioni kwa nini tuwe na raslimali, halafu tusiweze kuzitumia kwa manufaa yetu.

Gesi yenyewe tunalilia tu kuiuza nje, kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea imeshindikana?
 
Jamaa hao pamoja na unafiki wao wa kwamba makaa ya mawe yanachafua mazingira lakini wao kwenye nchi zao wanazalisha umeme kwa makaa ya mawe na ndio wanaonunua makaa ya mawe kutoka Tanzania (bandari ya mtwara iko busy kila siku kusafirisha makaa ya mawe kwenda ulaya kuzalisha umeme)
Unajua kitakacho fuata ni nini?

Ni hivi: hao jamaa sasa wataanza kuweka masharti. Kama unatengeneza bidhaa zako kutokana na vyanzo ya nishati vya uchafuzi wa mazingira, wanakuwekea ngumu kwenye soko lao na kwingineko.

Tayari wamea anza kuhoji hata mazao ya kilimo; kama kahawa, iwapo imezalishwa katika maeneo ambako misitu ilifyekwa.

Maendeleo ya hizi nchi zetu maskini yatapatikana kwa kazi ngumu sana.

Wewe angalia kama wanavyo tuhimiza sasa na hizi 'private sector', ambazo wanajuwa huku kwetu hazipo; kwa hiyo wanawajengea wigo wafanya biashara wao kuja kuchuma huku. Sasa PPP haiondoki kwenye ndimi zao na zetu. Kila mradi sasa wanataka ushiriki wa PPP (Public Private Partnership); mikataba ya miaka 30 au zaidi, jamaa wakivuna huku sisi wenyewe tumelala usingizi wa pono!
 
Tatizo viongozi tulionao ni wajinga na wapumbavu.akili zao nimeishia kuyauza makaa ya mawe Kwa shilingi elfsinini Kwa Tani Moja na kusafirishwa ulaya.Ni sawa tu na makinikia kudai kwamba hayana chochote na kupelekwa ulaya.kama kweli hayana chochote Kwa Nini wazungu wapeleke makinikia Kwa gharama kubwa ya usafirishaji kiasi hicho?
 
Kwa nini tusijenge tu kinu cha Nyuklia kama Kenya?
I thought the same.

Nuclear energy is more reliable than any source regardless of high cost in initiation and handling.

We have nuclear raw materials in Bahi and elsewhere in Tanzania but we can't consume to produce energy.
 
Jamaa ndiyo vinara wa kutoa hewa ya ukaa duniani, tukiendelea kuwasikiliza itakula kwetu.
Ni sahihi kabisa. Lakini haiondoi ukweli. Hawa wenzetu siku wakiwweza kuachana na hizi na sisi tukawa kama wao kwa sasa nadhani unaelewa vitisho na vikwazi tutakavyokutanana navyo.
 
Tabia nchi iko Tanzania peke yake? Sisi tusipotumia coal wengine wameacha pia? Kwa hiyo bora watumie wengine halafu sisi tugharimike na madhara..si bora tutumie wote sababu madhara ni kwetu sote, Botswana wanaotegemea coal 100% ulishasikia wanalalamika madhara ya kutumia coal? Hata miti si mingi sababu sehemu kubwa ni jangwa, Uchumi je na maendeleo kwa ujumla Tanzania tunawazidi au wako mbele yetu..
Msimamo wako ni sawa na msimamo wa mtu asiye na maadili na utu!
Usifanye mambo yenye madhara kisa wengine nao wanafanya!
You need to embrace intergenerational moral audacity and chart your way forward towards a greener future!
Washauri wenzako wawekeze kwenye teknolojia ya kuibadili coal kuwa cleaner energy. Mkiweza muendelee nayo kama mataifa mengineyo yanayojitahidi kuifanya coal kuwa nishati safi!

Someni shule na ziwasaidie kufikiri kwa usahihi!
 
Tatizo viongozi tulionao ni wajinga na wapumbavu.akili zao nimeishia kuyauza makaa ya mawe Kwa shilingi elfsinini Kwa Tani Moja na kusafirishwa ulaya.Ni sawa tu na makinikia kudai kwamba hayana chochote na kupelekwa ulaya.kama kweli hayana chochote Kwa Nini wazungu wapeleke makinikia Kwa gharama kubwa ya usafirishaji kiasi hicho?
Unachosema kweli kabisa
Kuna wakati nlikuwa nataka nifanye mchakato wa kuwaingiza
Na kuwafanya watu wawe wanatumia makaa ya mawe/domestic use/matumizi ya nyumbani ila kuna sehemu ndg nlikwama....ila mchakato wangu uko pale pale
Ila makaa ya mawe yanasafirishwa zaidi kuliko matumizi ya humu ndani...
Ila kama serikali ikiwa makini hyo noshati tunaweza kuitumia wenyewe na ikatusaidia

Ova
 

Attachments

  • VID-20240917-WA0002.mp4
    10.7 MB
Back
Top Bottom