Tanzania idadi ya watu imeongezeka lakini hali sio nzuri mkoa wa Kilimanjaro

Watu wamehama ardhi nyingi ipo tupu, sema mambo yale yale ya ukale yanawarudisha nyuma, mimi kijijini kwetu majirani karibu 4 kati ya 6 wamehama na mashamba hayatumiki ila kuuza hawauzi wala kukodisha
Na akikodisha anatazama aliyekodi anafanyia nini akiona kinalipa mkataba ujao anapandisha dau la kodi ukikataa anakubalasa anasema hapangishi tena, rudi baada ya miezi kazaa unakuta anafanya shughuli ile ile ambayo alikuwa anafanya mtu aliyekodi shamba.
 
Ishu inayozungumziwa hapa ni wakazi, kama wenyeji mkiwa wengi ila hamkai huo mkoa ni shida
 
Mkuu mbona Zanzibar ina watu 1.8 na uchumi upo vizuri mzunguko wa pesa ni mkubwa tu

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Ishu ni watu kupungua, ujue hata wangekuwa laki 5 ila wakawa hawapungui na nyumba kubaki tupu hapo haina shida, ila population inayopungua ina athari kiuchumi na kijamii
Mkoa mzima overall unaonyesha watu kuongezeka kwa laki 2 (hii imebebwa na Moshi mjini) ila ukichunguza wilaya moja moja watu wanapungua
 
Kila kitu kizuri kinawekezwa Dar Es Salaam.
Kazi, biashara, huduma za afya, elimu n.k.
Matokeo yake ndio hayo, mtu mwenye elimu yake kama haishi Dar, basi ni ughaibuni, na huko ndiko familia yake ilipo.
Wachaga walijenga shule nyingi, na walielimika wengi hata huko migombani, tatizo huko hakuna pa kuzitumia elimu yao, hivyo we go kama sio wote waliondoka. Sijui kama watarudi watakapostaafu au la.
 
Ishu inayozungumziwa hapa ni wakazi, kama wenyeji mkiwa wengi ila hamkai huo mkoa ni shida

Ishu inayozungumziwa hapa ni wakazi, kama wenyeji mkiwa wengi ila hamkai huo mkoa ni shida
Na ndicho nilichojibu lakini kwa mapana:

Wakazi - Kwa mujibu wa sensa 2022 bado wanaongezeka ingawa kwa kasi inayopungua tofauti na mtoa mada anayesema wakazi wamepungua sana kama si kwisha kabisa.

Ukijumlisha na sisi tunaoenda holiday season tu idadi inakuwa kubwa zaidi kuendelea ku sustain lively hood.
 
Nitazungumzia Wachaga tu.
Ukweli utabaki palepale sisi Wachaga ni miongoni mwa makabila machache yaliyo starabika na kujali asili yetu, mila zetu, wazee wetu vilevile ardhi ya nyumbani ni mali na urithi wa kizazi kilichopo na kijacho.

Ni kweli kabisa kuna nyumba hamna watu zaidi ya wazee na mashambaboy tu mfano mzuri ni nyumbani kwetu na hii ni kutokana na kila mtu kuajiriwa/kujiajiri sasa abaki nyumbani kufanya nini..?

Hizo nyumba ulizoona zimefungwa hazikai watu hebu rudi tena kuanzia tarehe 10 December ukakutane na wamiliki wake.
Maana kila mtoto wa kiume aliyeoa atapambana ajenge hata room mbili kwenye shamba lake ili akienda nyumbani kusalimia au kwenye shughuli ya ukoo/familia afikizie kwake na sio kwenye nyumba ya mzee.
 
Huu utaratibu inabid uachwe hakuna haja ya kujenga nyumba nyingi huku ambazo zipo watu hawakai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…