Tanzania idadi ya watu imeongezeka lakini hali sio nzuri mkoa wa Kilimanjaro

Tanzania idadi ya watu imeongezeka lakini hali sio nzuri mkoa wa Kilimanjaro

Kutokana na utaratibu wa wachagga kutokuuza viwanja kama makabila mengine, maendeleo yamezorota maeneo mengi.

Ukibaki kijijini utaishia kuwa mlevi wa mbege
Mkoa wa Kilimanjaro ndio wenye vijiji vilivyo endelea zaidi, nyumba bora, umeme, maji hata kipato, sio maneno yangu bali ni takwimu za serikali
 
Hii ni cjangamoto kubwa sana. Wengi tunatembelea kwa siku chache na kurejea mjini. Vijana wa makabila menhine ndio wanalinda majengo mengi uchagani. Kuna haja ya kutafakari. Mimi nakusudia kubadilisha matumizi ya mji wetu uwe sehemu ya mapumziko kwa wanaohitaji kubadilisha mazingira kwa vipindi.
Mimi nina moango wa kufyeka migomba na kahawa zote kule nilime maparachichi kwa large scale
 
Kwaiyo mkuu kule Kilimanjaro hakuna fursa za ujasiriamali zaidi ya kupika pombe za kienyeji , kuwa boda boda ni ngumu kwasababu wateja wanaonde kazin asubuhi hawapo na watu ni wachache na hawa tembei

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Hawapiki sana siku hizi, kuna viwanda bubu ambavyo vinatengeneza zile pombe kama jamii ya banana ndio vinazalisha pombe nyingi inayotumika sasa
Mbege hata haipikwi sana siku hizi
 
Tanzania nzima ndio inatakiwa iwe hivyo, huu ujinga wa ukabila haisaidii chochote zaidi ya kuleta ubaguzi
Tamduni muhimu kijana, Tz nzima sio kabila moja lazima ujue na uielewe asili yako.
Ubaguzi hautakuja kuisha duniani ni kuupunguza na kuishi nao tu.
 
Kusema ukweli mleta mada yupo sahihi kabisa, natoka wilaya ya rombo nadhani huko ndio hali mbaya kabisa hata biashara ndogondogo ni vigumu kufanya kwa sababu hakuna watu, serikali hapa lazima ifanye kitu huu ujinga wa kuzaa kwa mpango hamna tutajikuta siku moja mkoa flan unapoteza origin yake.
Tatizo linaletwa na watu kuhama, wala sio kuzaa kwa mpango
 
Kilimanjaro hakuna maisha mpaka watoke kwenda kutafuta sehemu zingine??
 
Mkoa wa Kilimanjaro ndio wenye vijiji vilivyo endelea zaidi, nyumba bora, umeme, maji hata kipato, sio maneno yangu bali ni takwimu za serikali
Kilimanjaro ukiitoa Moshi, sehemu nyingine MJINI ni wapi?
 
Kwahiyo Kilimanjaro hakuna Maisha?
Kilimanjaro maisha ni magumu mnoooo. Ukitaka idadi kamili ya watu Kilimanjaro labda uwahesabu December au uhesabu NYUMBA. Maana NYUMBA zinajengwa halafu Hakuna watu.
 
Hii mambo inaniwazisha sana mkuu
Sjajua haya mabaliko yataishia wap
Maana hata wale vijana wachache waliobakia pale hawana malengo ya pale wanawaza mjini tu
 
Arusha sehemu gani? Labda huko Longido, Maeneo ya Meru Ardhi ni ngumu
Sasa Meru ni sehemu ndogo haifikii hata marangu kwa ukubwa, hapo hujaongelea kibosho, old Moshi, machame, rombo Kilimanjaro hadi kule upareni kwenye milima watu wanagombania ardhi
 
Huduma kama hizo kwa hali ya Tanzania unazikuta tu mjini
Kwasababu mikoa mingi Kuna MIJINI
Pia, Kilimanjaro ni ndogo sana, na udhaifu wa serikali ulivyo wanaofanya maamuzi hawana akili.

Mfano, Kilimanjaro Kuna shule nyingi na zahanati, lakini unashangaa pesa za mgawo wa UVIKO na TOZO wakalazimishwa wajenge Tena madarasa wakati yaliyopo tu hayatumiki yote.

Lakini wangewaacha huru, wangetumia hizo pesa kufanya ukarabati wa majengo mabovu.

Kwa Kilimanjaro, Wilaya moja tu mfano Rombo inalingana na Tarafa mkoa mwingine, kwahiyo usitarajie wakashindwa kuweka umeme mkoa mzima.

Rombo unaweza kuzunguka na pikipiki masaa 6 ukaimaliza yote.

Lakini Wilaya Kama Geita au Mlimba Morogoro huo uwezo haupo leave muda mfupi.
 
Back
Top Bottom