Tanzania idadi ya watu imeongezeka lakini hali sio nzuri mkoa wa Kilimanjaro

Tanzania idadi ya watu imeongezeka lakini hali sio nzuri mkoa wa Kilimanjaro

Hayo maswali yako ni rahisi sana kuyajibu, Jamii ya wachagga ni jamii inayo jishughulisha sana kwenye masuala ya maendeleo hususani biashara n.k

Cha msingi kuwa na maisha bora kuweza kumudu kusaidia familia kuwa katika hali nzuri n.k sasa basi kutokana na hali hiyo mchagga lazima atoke kwao ili atoboe ni lazima akajichanganye popote panapo wezekana ili apate chochote kitu.

Hili ni jambo la kawaida sana kwa jamii hii tofauti sana na jamii zingine hapa nchini ambazo huwa hawa sanuki mapema kuanza harakati za kimaendeleo ikiwemo ku make mkwanja ndio maana kwa asilimia kubwa sana nchi hii wachaga wana miliki pesa ndefu sana ukilinganisha na jamii zingine.

Lakini pamoja na hayo yote jamii zingine hapa nchini kwa sasa zimeamka sii haba wana jichanganya na kufanya harakati zao za kusaka noti sehemu mbali mbali nchini na kwingineko duniani.
Mim sijaongelea maisha Bora na sijafanya comparison na jamii nyingine nimeongelea mkoa wa Kilimanjaro
 
ukiona hivyo ujue nimkoa ambao hauna fursa ukibaki huko utabaki maskini. halafu shida nyingine wanaoa kamke kamoja kamoja kamavile nimahanithi unamkuta mtu anavitoto viwilitu vya dawa.
 
Ukienda mkoa wa Kilimanjaro utashangaa mambo yafuatayo haya matatizo hayako tu uchagani bali hata upareni yapo

Idadi ndogo ya wanafunzi wanaoandikishwa darasa la kwanza, huku mikoa mingine wanafunzi wakiwa wengi na wengine wanakaa chini Hali ni tofauti mkoa wa Kilimanjaro idadi ya wanafunzi inazidi kushuka kila miaka inavyozidi kwenda Kuna shule inaandikisha darasa la kwanza wanafunzi 10, Kuna nyingine iliandikisha wa-nne

Nyumba nyingi kuwa empty hili ni tatizo lingine kubwa Kuna idadi kubwa sana ya nyumba hazina watu na ukienda vijijini Hali ndo mbaya Zaid nyumba nzuri nyingine gorofa Ila hazina watu sanasana utamkuta kijana mmoja tu ambaye Yuko kwa ajili ya kuziangalia

Vijiji mkoa wa Kilimanjaro havina watu kama umepanga kwenda kukaa week kwa Ile Hali ya vile vijiji vyao utajikuta umehairisha hakuna watu kabisa yaani in-short mkoa wa Kilimanjaro una ukiwa sio sawa na kipindi tunakua

Changamoto nyingine hakuna vijana Kuna kijiji nilienda kijiji kizima kijana ni mmoja ambaye ni bodaboda wengine waliobaki ni watu wa miaka 40 na kuendelea ni nadra sana kumuona kijana wa miaka 20's
Kwani Kilimanjaro nzima ni wachagga tu? Kwani watoto wanaoandikishwa darasa la kwanza mikoa mingine hakuna kichagga? Kwani sensa inaonesha idadi ya watu mkoani kilimanjaro imeshuka, ingawaje si wote ni wachagga?
 
Huko Kilimanjaro watu hawaendi kutafuta maisha
Ukihamia Kilimanjaro na ukatoboa basi jua ungekuwa kwenye majiji ungetoboa zaidi.

Mfano sisi kwenye group la whatsApp tuliokuwa na kusoma pamoja waliopo Moshi kwa sasa hawazidi hata 5, wengine wote tupo mikoa ya watu huku
 
ukiona hivyo ujue nimkoa ambao hauna fursa ukibaki huko utabaki maskini. halafu shida nyingine wanaoa kamke kamoja kamoja kamavile nimahanithi unamkuta mtu anavitoto viwilitu vya dawa.
Ule mkoa sio maskin hata ukiangalia kwa kipato wako vizuri
 
hatuongelei kuhusu panya mkuu.
Nimejibu kutokana na alichokiandika, huwezi kusema wachagga ni mahanithi kwakuwa wanaoa mkeo mmoja na kupata watoto 2.

Unaoa na kutafuta watoto kutokana na nguvu zako katika majukumu ya kuilea familia. Kuna watu wana wake na watoto wengi lakini hawawezi kutimiza majukumu yao katika ulezi.
 
Ukimkuta kijana anaishi Kilimanjaro miezi 12 ya mwaka chunguza akili yake.

Ule mkoa haufai kuishi kabisa. Hakuna changamoto, hela ngumu, watu wachoyo, wabahili.

Ila ni pazuri kwenda kutalii. Pale Moshi hali ya hewa yenyewe ni utalii tosha
 
Sis tulizaliwa 15 ila sasa wako baba na mama peke yao
Duuu ina maana kilamanjaro ni pangumu kufanya maisha na kuo au kuolewa? vijana wanaishi Kilimanjaro kufanikiwa kimaisha wakiwa Kilimanjaro inaoneka ni jambo ambalo haliwezekani?

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom