Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Haya ni maoni yangu mimi kama mimi kuiomba Serikali yetu kuiandikia barua VOA kupitia Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania kuiomba Msamaha nchi yetu, kwa habari yake ya kizushi, uongo, fitina, uchonganishi na yenye kuichafua serikali pamoja na Rais wetu.
Hii ni kwa kuwa kila mmoja anatambua kuwa habari iliyotolewa na VOA yaani Sauti ya Marekani ni ya uongo mkubwa sana, kwa kuwa mkataba uliosainiwa na Nchi yetu inahusisha mkopo wa masharti nafuu kabisa wa Dolla Billion 2.5. ambao utalipwa kwa muda wa miaka 40 na ambao riba yake ni 0.01% tu. Mkopo ambao utasaidia sana katika kuchochea kasi ya maendeleo na kuinua uchumi wetu kupitia miradi ambako pesa hizo zitawekezwa pamoja na kuzalisha fursa za maelfu ya ajira kwa vijana.
Ni Muhimu chombo hiki kiombe msamaha kwa propaganda zake chafu na zenye nia ovu ya kutaka kujenga taswira mbaya kwa serikali na Rais wetu. Ikumbukwe habari hii haijatolewa kwa bahati mbaya au kukosea, bali ni habari ambayo inalenga kuichonganisha serikali na wananchi pamoja na kutaka kumshushia heshima Rais wetu kwa watanzania ,hasa kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu na kutambua nguvu na Ushawishi mkubwa alionao Rais wetu kwa watanzania.
Hii ni baada ya kuona kuwa Marekani kwa sasa Inaendelea kupoteza nguvu na ushawishi wake iliokuwa nayo pamoja na kuendelea kubomoka kwa ule ufalme wake na U Mungu mtu wa kuabudiwa na mataifa mbalimbali.
Sasa mataifa mengi yanaikimbia Marekani ambayo mikopo yake wakati mwingine imekuwa na masharti Magumu ambayo yanakwenda kinyume na mila na utamaduni wetu. kwa wao kusema ni sehemu ya haki za binadamu na kwamba tuziheshimu haki hizo na kuzilinda na kuwalinda watu hao.
Napenda kuwakumbusheni tu watanzania wenzangu kuwa hakuna mkataba ambao serikali yetu imesaini unaoitoa sehemu au kipande chochote kile cha bahari yetu, wala hakuna mahali popote pale ambapo mkataba umesainiwa ambao Unayatoa madini yetu au Mgodi wetu na kuwakabidhi Korea kusini, hakuna mkataba huo na hakuna sehemu yoyote ile penye masharti ya aina hiyo wala makubaliano ya namna hiyo.
Hii ndio sababu hata hao wazushi na wachonganishi na wafitini wameshindwa kabisa kabisa kuweka na kuonyesha sehemu au mahali au kipengele chochote kile cha mkataba kinachozungumza habari hizo za Uzushi na ufitini wa kutoa bahari na madini yetu kama sehemu ya masharti ya kupata pesa hizo takribani Trilioni 6.5.
Tuendelee kuwa na Imani na serikali yetu pamoja na Rais wetu kipenzi. Tukumbuke ya kuwa mahasimu wetu pamoja na washirika wao wameumia sana kwa sisi kupata mkopo huo wa masharti nafuu kabisa na wenye tija kubwa sana kwa ustawi wa Taifa letu na maendeleo ya watanzania.
Kazi iendelee, Mama ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Soma:
- VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini