Ni kweli Ulaya na Merikani kunatisha - hivi sasa inaelekea mataifa hayo yanakabiliwa na second phase ya maambukuzi ya COVID-19.
Kilicho nitisha zaidi ni pale nilipo msikia Waziri mkuu wa Uingereza jana akionya kwamba hivi sasa Uingereza inakabiliwa na strain mpya ya COVID-19 ambayo inaweza kuwa ni more virulent kuliko strain ya kwanza, nikawa najiuliza maswali mengi kwamba inawezakana kuna wanasayansi wanavifanyia virus ukarabati ili viwe hatari zaidi.
Waziri mkuu wa Uingereza alionekana ana wasi wasi sana anawashauri raia wake kwamba hata XMAS washerekee wakiwa majumbani kwao wasitoke nje na kuranda randa ovyo kutokana na kuwepo STRAIN mpya ya COVID-19 - sasa hii inaleta picha gani kimataif?
Ni wazi tukiendelea kuruhusu ndege na watalii pamoja na wageni kutoka kwenye Mataifa hayo athirika bila ya kuchukua hatua kali za kudhibiti miingiliano holela na wageni, Taifa letu linaweza kukumbwa na second phase ya corona ambayo Waziri mkuu wa Uingereza amethibitisha kwamba ni STRAIN mpya -
no one knows how to deal with it labda tukisaidiwa na wataalamu wa Kichina kwa kuwa Taifa la China ndilo limeonekana lina mbinu za hali ya juu jinsi ya ku-deal na COVID-19 pandemic effectively - pendekezo langu ni kwamba Wizara ya afya pamoja na Wizara ya Utalii ziwe makini sana kudhibiti wageni, zisiogope lawama.