Tanzania iko katika matishio ya amani na usalama chanzo wivu wa rasilimali zetu

Tanzania iko katika matishio ya amani na usalama chanzo wivu wa rasilimali zetu

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
268
Katambi ajitetea na agizo lake la kuzuia mikutano :'Sijakiuka Katiba', awashukia vikali CHADEMA

Akizungumza leo Juni 27, 2026,wakati wa maadhimisho ya siku ya wazee duniani huko mkoani Shinyanga, Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobasi Katambi amekanusha juu ya kuvunja Katiba na kueleza matishio ya amani ndio sababu ya kuzuia mikutano ya kisiasa.

“Wapo wanasiasa ambao wanasema,mmewasikia.Nimezuia vyama vyote vya siasa katika kipindi hiki chenye matishio. Hata CCM chama changu nimezuia, sasa ubaguzi unatoka wapi? Katiba hii nimeisoma kwa miaka yote shuleni, sasa leo eti kuna mtu hapo amekiuka katiba? Nani amesema tunavunja Katiba?,”amehoji Katambi.

“Hali na matishio ya amani na usalama yapo pale, taifa letu leo mmesikia kila mahali inaelezwa vijana wachache,kundi la watu wachache wadogo, ambao wanatamani madaraka kwa kutumia nguvu. Wanatamani madaraka kwa kuhongwa vifedha ili waumize Watanzania, wapeleke clip za video. Hawajafa watoto wao, Watanzania wamekufa, wao waje kupewa madaraka kwa mabavu,”aliendelea kufafanua.
 
upinzani wanataka kuichafua nchi dawa washushwe bega kaba hawajakomaa

hii tabia ya wanachokiita mandamano naona inamea kwa kasi sasa
 
Njaa mbaya mno
Buku 7 kwa cku.
Joined
Kazi ni kipimo cha utu
 

Attachments

  • Screenshot_20260628_150539.jpg
    Screenshot_20260628_150539.jpg
    45.1 KB · Views: 12
Back
Top Bottom