Kinyungu
Platinum Member
- Apr 6, 2008
- 22,912
- 46,240
Zinatokana na aina ya katiba tuliyonayo kwa sasa maana imeweka mamlaka yote mikononi mwake rais. Anaweza kuteua, kutengua, kufukuza na asihojiwe na yoyote. Rais anateua hadi mwenyekiti wa bodi ya bonde la mto panganiSasa jiulize, nguvu au uwezo wa kushawishi hawa wote, hivyo vyombo vya dola, BAKWATA, na CCM yote yeye kazitoa wapi?
Binafsi naamini tukijuwa nguvu zake zinatokana na nini, huo utakuwa ni mwanzo wa kujuwa njia za kumkomesha
Samia anapata wapi nguvu za kuwanyanyasa waTanzania wote kiasi hiki.
Nikisoma andiko lako hapa, naona jibu limo humo katika hao uliowaorodhesha.
Lakini vyombo vya ulinzi siyo washiriki wa moja kwa moja. Hawa wabnapewa amri tu kutimiza kilichoamriwa.