Tanzania Ilipofikia Sasa Hata 'Banana Republic' Ina Nafuu

Zinatokana na aina ya katiba tuliyonayo kwa sasa maana imeweka mamlaka yote mikononi mwake rais. Anaweza kuteua, kutengua, kufukuza na asihojiwe na yoyote. Rais anateua hadi mwenyekiti wa bodi ya bonde la mto pangani
 
Acha tu...
 
Zinatokana na aina ya katiba tuliyonayo kwa sasa maana imeweka mamlaka yote mikononi mwake rais. Anaweza kuteua, kutengua, kufukuza na asihojiwe na yoyote. Rais anateua hadi mwenyekiti wa bodi ya bonde la mto pangani
Hili swala la katiba ni kisingizio tu. Sababu nyepesi tunayoitumia tunapokosa majibu sahihi kuhalalisha maovu yanayofanyika.

Ubinaadam/utu hauhitaji katiba.
 
Raisi aseme namtaka huyu, halafu wewe upinge, wakati ubunge wenyewe ni yeye kakupa, hapo utakua unataka kuokotwa koko
Eti ,eeh Bhwanah!
Ni fursa hiyo sasa anayoitumia Samia kutimiza ajenda ambayo sote tunaogopa kuizungumzia, si humu tu JF na hata huko kwingineko.
Una maana hata humu JF Samia (unayemwita Rais) kaingia na kufunga vichwa vya watu wasijue tatizo la nchi yetu linatokana na nini, na wala hatutaki kujuwa wahusika wa tatizo ni akina nani?
 
Zinatokana na aina ya katiba tuliyonayo kwa sasa maana imeweka mamlaka yote mikononi mwake rais. Anaweza kuteua, kutengua, kufukuza na asihojiwe na yoyote. Rais anateua hadi mwenyekiti wa bodi ya bonde la mto pangani
Utanisamehe mkuu wangu 'Kinyungu', ninaelewa unachosema, na ni sababu ambayo tumezoea kila mara kuiweka mbele, hii habari ya Katiba.
Binafsi sasa hili sihangaiki nalo tena, kwa sababu najuwa tatizo letu ni kubwa zaidi ya hicho kisingizio cha kila jambo kuwa katiba.

Katiba nayo ina ukomo wake maswala ya 'decency'/utu/ubinaadam unapopuuzwa.
Baada ya kutafakari vya kutosha, sasa nimejiridhisha kuwa hili siyo swala la Samia peke yake kutaka urais kwa mabavu yote awezayo. Hili sasa limekuwa ni swala linalosukumwa na nguvu nyingine nje ya kutaka madaraka pekee..
 
Kwa tz raisi ni Mungu mtu, anaumba na kutoa roho, ni hatari
 
Usisahau kuna cartel ya watu walio nje ya serikali lakini wenye maslahi na hii serikali ya ccm. Hao ni wafanya biashara wakubwa wa the like of RA ambao wanasukuma mambo tokea pembeni.

Kimsingi hapa tulipofikia ni kama kile kilichotokea South Africa enzi za Zuma. Wenyewe waliita "state capture" kuna kila ukweli kuwa na sisi tumetumbukia kwenye huo mduara. Uzuri wao South Africa walikuwa na wazalendo waliokataa na kuamua kumtoa Zuma na hatimaye kuwa pursue kina Gupta japo sijui kama waliwapata.

Tanzania hatuna state apparatus za kuweza kulitoa taifa katika hali lilipo maana vyote vipo chini ya milki ya hao walio capture nchi yetu.
 
Kimsingi hapa tulipofikia ni kama kile kilichotokea South Africa enzi za Zuma. Wenyewe waliita "state capture" kuna kila ukweli kuwa na sisi tumetumbukia kwenye huo mduara
Now you are talking. Lakini bado.
"State Capture" is real sasa hivi kwa Tanzania; lakini hao unaowazungumzia, hao wafanya biashara baadhi yao ni wawezeshaji tu wa dude kubwa wasilojuwa ndilo linaloset pace ya uchangiaji wao.

Akina RA wanafaidika pande zote mbili, if you know what I mean! Yaani wanatumia jiwe moja kuua ndegewawili kwa mpigo.

Ninakubaliana na wewe kuhusu bahati waliyokuwa nayo Afrika Kusini . Inavyoelekea sisi hapa hiyo bahati hatuna, kwa hiyo tukishajuwa tatizo letu hasa ni nini, njia pekee tuliyo nayo ni mapambano tu, sisi kwa sisi; au tuikubali hali tunayotakiwa kuifuata na hawa wanaotuongoza kwenda huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…