Tanzania iliwaza vyema, umeme mkubwa uliopita sokoni umeua watu 26 Kongo

Tanzania iliwaza vyema, umeme mkubwa uliopita sokoni umeua watu 26 Kongo

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Nchini Tanzania hairuhusiwi kujenga au kufanya shughuli chini ya miundombinu ya umeme inayobeba umeme mkubwa(High voltage). Wachache wanaelewa lengo, wengine wakijaribu kuishi chini ya njia hizo na mara kadhaa tumeshuhudia bomoa bomoa. Pia TANESCO wakijenga njia mpya wako radhi kulipa fidia wahusika waondoke.

Nchini Kongo, hali imekuwa tofauti kwenye soko lililopo mjini Kishasa ambapo waya unaobeba umeme mkubwa umedondoka na kugusua baadhi ya nyumba na soko hilo, watu 26 wakifariki.

Chama cha wahandisi nchini Kongo kwenye taarifa yake, wamesema ajali hiyo ambayo iliweza kuepukika ni matokeo ya kutoheshimu mipango miji chini ya njia kubwa za umeme.

Shirika la umeme nchini Kongo limesema ajali hiyo ilitokea radi ilipopiga wakati wa mvua na upepo mkali Jumatano asubuhi na kutoa pole kwa familia zilizoathirika.

Video iliyosambaa inawaonyesha marehemu miili yao ikiwa imelala sehemu ikiwa kwenye maji yatokanayo na mvua. Waziri mkuu amesema soko hilo lilishapangwa kuhamishwa kwenye baraza la mawaziri kilichofanyika Jan 7, sababu ya wakati huo ikiwa ni soko kutengeneza foleni barabara inayounganisha Kinshasa na mji wa Matadi.
 
Nchini Tanzania hairuhusiwi kujenga au kufanya shughuli chini ya miundombinu ya umeme inayobeba umeme mkubwa(High voltage). Wachache wanaelewa lengo, wengine wakijaribu kuishi chini ya njia hizo na mara kadhaa tumeshuhudia bomoa bomoa. Pia TANESCO wakijenga njia mpya wako radhi kulipa fidia wahusika waondoke.
Wewe unauhakika hakuna masoko chini ya nyaya za umeme au unajipa uzalendo wa kijinga!
 
Wewe unauhakika hakuna masoko chini ya nyaya za umeme au unajipa uzalendo wa kijinga!

Masoko sijawahi kuyaona, mfano wa nguzo iliyodondosha waya Kongo ni huu.. Umeona zimepita katika soko gani Tanzania?

High voltage.jpg
 
Mleta mada NENDA HAPO TABATA SANENE kuna TUSIIME SCHOOLS PARKING YA MABASI YA KUPAKIA NA KUSHUSHA watoto iko chini ya NGUZO za Umeme wa MSONGO MKUBWA zinazoelekea KIPAWA. Wakaguzi wa Uthibiti Ubora wa Shule Wanasubiri lakutokea ndipo waje waseme ni Mipango ya Mungu!
Over
 
Asalaaleeeh! Danger
 
Back
Top Bottom