Tanzania imegeuka kuwa Taifa linaloshauriwa na watumiaji wa Mitandao?

Tanzania imegeuka kuwa Taifa linaloshauriwa na watumiaji wa Mitandao?

Ili mradi katiba haijavunjwa, kwani ndivyo inavyotaka.
 
Ni kweli kwamba kuna mambo yanafanyika mpaka yanashangaza kwamba ni kweli kuna wataalam kwenye serikali au vipi.

Lakini chanzo ni roho za kimaskini na chuki ndiyo zinawasumbua watu.

Kuwa rais ni kitu kigumu sana.

Imagine kwamba unahusika na kila kitu kwenye nchi na wewe sio mtaalamu wa kila kitu kuna mambo huna ufahamu nayo hata kidogo kwa hiyo unawategemea wataalam wako ili wafanye kazi zao vizuri na wakupe taarifa kadiri inavyofaa.

Lakini katika haohao kuna wasio kupenda hawajapenda ulivyokuwa rais kwa hiyo hawapendi ukifanya vizuri lakini inawezekana ndiyo watu unaowaamini kwa sababu hawaishi kuonyesha uhalisia wao ni changamoto sana ndiyo maana wakati mwingine unakuta mtu anamteua ndugu yake.

Kushughulika na hoja za mitandaoni na kuzifanyia kazi ni jambo jema unapata mambo halisi kuliko wale unaowategemea wakati mwingine huwenda wakakupa taarifa zisizo sahihi kwa maslahi yao binafsi.

Ningekuwa rais ningekuwa na application kabisa ya wananchi kungekuwa na setion ya kila mkoa kuongea kero zao humo ambacho ningefanya ni kuchunguza na kufanyia kazi bado pia ningedili na wananchi feki na kupost kero feki ikibainika ingekuwa ni jinai kuidanganya serikali.

Maisha yamebadilika maisha kidigital.
 
Unaelewa maana ya mitandao ya kijamii? Huon ni platform muhimu ya kisasa ya kukutanisha wananchi na serikal yao. Kuna tatzo gani kwa wananchi kutoa maoni...aliekwambia watu wa ikulu ndio wenye weledi zaid kuliko wananchi ni nani?

Zaman mlikua mnalalamika saut za wananchi hazipai..leo kuna access hyo mnapiga kelele.

Ujue sis wa Tz tuna pepo fulan hiv la ujinga na umaskin...siku tutakapo badilika ndipo tuta tutaibadili taswira ya nchi yetu.
 
Mkuu hujui chochote ndio mana unakuja na nadharia zako hapa.
 
Hauko sawa kiakili unakurupuka kama unaharisha mavi.
Ndugu, mbona unatukana tena. Kwa nini usionyeshe udhaifu wa hoja yangu badala ya kutukana? Tuko hapa kujadiliana, kuelimishana na kutoa mawazo na mitazamo yetu.
 
Madhara ya ajira za undugulization,ukanila,baba kanituma,vimemo ndo haya.

Mtaani wameacha cream wamewaeka ndugu zao utategemea nn Zaid ya madudu Kama hayo.

Ni doa kubwa Sana hili,mama Kama anaona bp ajipe muda Zaid then atakao ridhika nao awachendue tu.

Wengine Wana maCV makubwa lakini uwezo mdogo.

Watafute watu Wana elimu na wanauwezo wa asili ktk vision ya Mambo mbalimbali.

Wasirudie Tena hii kitu,imeleta taharuki na wengi kuhoji Ni Nani wanajua nyuma ya hili la teuzi?Wako wapi usalama wa Taifa wachukue majina wakafanye upembuzi warudi na majibu kabla ya teuzi
 
Sasa huko ndani watashauri nini ikiwa wote akili zilikua zime focus kumwongezea mtu fulani miaka ya kuongoza?
 
Digital age haiepukiki , social media ni jamii halisi katika mfumo wa digital. usipokubaliana na mitandao ya jamii utakuwa direct hukubaliani na jamii yenyewe.

Kuna mabaya pia ila mazuri ya social media ni mengi.
 
Tunaamini Raisi wetu Mama Samia ni muungwana mwenye mila na desturi na silka ya Kizanzibari na muungwana akilivuliwa nguo huchutama imani yangu ni kuwa dhulma zote zilizofanywa na mwenda zake atazitatua na kuzipatia ufumbuzi.

JF we should be very proud kama sauti zinakwenda mbali na kusikika na serikali ,kusikiliza sauti za raia yake ndivyo inavyotakiwa na hiyo ndio serikali ya wananchi .Tunamwambia Mama Samia Raisi wetu Hala hala Ujiti na macho ncha ina hoho, vyako vyako na wenzako vikikupata vyako peke yako na kikulacho kimo katika nguo yako, tenda wema wende zako usingoje shukurani .Mama Samia miaka 4 ni sawa na siku nne tu katika kipindi chako cha uongozi kumbuka Allah kakupa mtihani katika maisha yako kuwa MUADILIFU Usidhulumu na weye usikubali Kudhulimiwa.

Allah akulinde na kila sui akufanyie wepesi ktk uongozi wako akulinde na mahasidi wako kila ajae na shari waijua yake siri ivunje yake dhamiri asiweze kusimama.Allahumma Amin Thumma amiiiiiin.
 
Ni kweli tupo kwenye ulimwengu wa kidigital, hivyo huwezi kuwakwepa watumiaji wa mitandao. Maana mitandao kama JF huku watu wanatiririka ukweli tofauti na kwenye magazeti.

Lakini hii sio sababu ya kusema kuwa serikali iwe na watumishi amabo inawalipa mishahara alafu hawajui masuala ya kitaalamu na kiutawala. Matokeo yake eti likitokea kosa wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii ndio wapost juu ya hilo kosa na kisha serikali kujirekebisha.

Mfano alipofariki hayati rais JPM, rais wa sasa alitangaza maobolezo kinyume na sheria ya mazishi ya viongozi, na alisema maombolezo ni siku kumi na nne. Ni aibu ofisi nyeti ya ikulu ambayo inawatalaamu wa kila namna wakiwemo wanasheria kumuingiza chaka aliyekuwa mtoa taarifa. Lakini kosa hili lilibainishwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa JF na baadae wakajirekebusha.

Hii ya kuteua kada wa Ccm awe mkurugenzi wa TPDC ni doa baya sana kwa ofisi ya rais hasa ukizingatia sifa za huyo kada ukilinganisha na unyeti wa shirika alilokuwa anapaswa kuliongoza. Nalo ni watumiaji wa mitandao ndio waliliibua na baada ya masaa 12 ndio akatenguliwa.

Hii inatupa picha mbaya sana juu ya watu ambao wanalipwa mishahara mikubwa kwa kutumia kodi za wananchi huku wakionyesha wazi kuwa hawana uwezo wa kutimiza wajibu wao.

Je, kama kungekuwa hakuna mitandoa ya kijamii ingekuwaje?

Na kwa Kukusaidia tu hakuna Mtandao ambao Mama ( Mheshimiwa ) Rais anaupenda na anauamini tena 99% japo hata Yeye pia tunae humu humu kama huu wa JamiiForums.

Na kama kuna Awamu ambayo Maudhui ya JamiiForums ( hasa yaletwayo ) na Members hapa yatakuwa yanatumiwa nae ( Mheshimiwa Rais ) basi ni Awamu yake hii ( Uongozi wake ) huu Mama.

Nilishawahi kusema huko nyuma kama Rais yoyote wa Tanzania Alitalia kujua mengi au kupata Ushauri wa Kuongoza vyema na hata Kupima uelekeo wake ili ajirekebishe Basi autumie sana huu Mtandao wa JamiiForums utamsaidia vingi.

Ni bahati mbaya mno wengine ama kwa Ushamba wao au kuwa na exposure ndogo ya kujua Nguvu ya Mitandao katika dunia ya sasa waliichukia Mitandao wakidhani ipo tu kwa ajili ya Kuwakosoa ( Kuwasema ) wakati kuna nyakati ilikuwa ikimsaidia kuyajua yale asiyoyajua huko huko Serikalini na Ikuluni Kwake.

Mimi JF Members wote huwa nawaita Whistleblowers ( na ndiyo maana tunatumia anonymous ID's ) hivyo ukiona Mtu ( Member ) kaja na Critical Observation yake hasa ihusuyo Jambo Nyeti la Serikali au Idara zake au anatoa a very Classified Information hapa jua yupo sahihi na huenda akawa yuko Jikoni pia vile vile.

Nadhani kama kuna Awamu ambayo inatakiwa si tu iutambue huu Mtandao wa JamiiForums bali pia ikibidi Founder wake Maxence Melo ( Genius and IT Guru ) apewe Tuzo ya Kipekee kwa kuja na hii Platform nzuri inayoleta Mawazo Kinzani, Mawazo Tija na Mawazo Shauri basi ni hii aliyoshika sasa Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan na kwa nimjuavyo najua hili atalitekeleza vizuri tu.

Usipoyaanini Mawazo na Fikra za JamiiForums Great Thinkers waliojazana hapa utayaamini ya Wapuuzi gani wengine huko nje? Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan tumia huu huu Mtandao wa JamiiForums utakusaidia vingi tu kuliko hao Wanafiki wengi wanaokuzunguka hapo ambao muda mwingine wanaweza wasikuambie Ukweli.
 
Ni kweli tupo kwenye ulimwengu wa kidigital, hivyo huwezi kuwakwepa watumiaji wa mitandao. Maana mitandao kama JF huku watu wanatiririka ukweli tofauti na kwenye magazeti.

Lakini hii sio sababu ya kusema kuwa serikali iwe na watumishi amabo inawalipa mishahara alafu hawajui masuala ya kitaalamu na kiutawala. Matokeo yake eti likitokea kosa wananchi wanaotumia mitandao ya kijamii ndio wapost juu ya hilo kosa na kisha serikali kujirekebisha.

Mfano alipofariki hayati rais JPM, rais wa sasa alitangaza maobolezo kinyume na sheria ya mazishi ya viongozi, na alisema maombolezo ni siku kumi na nne. Ni aibu ofisi nyeti ya ikulu ambayo inawatalaamu wa kila namna wakiwemo wanasheria kumuingiza chaka aliyekuwa mtoa taarifa. Lakini kosa hili lilibainishwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa JF na baadae wakajirekebusha.

Hii ya kuteua kada wa Ccm awe mkurugenzi wa TPDC ni doa baya sana kwa ofisi ya rais hasa ukizingatia sifa za huyo kada ukilinganisha na unyeti wa shirika alilokuwa anapaswa kuliongoza. Nalo ni watumiaji wa mitandao ndio waliliibua na baada ya masaa 12 ndio akatenguliwa.

Hii inatupa picha mbaya sana juu ya watu ambao wanalipwa mishahara mikubwa kwa kutumia kodi za wananchi huku wakionyesha wazi kuwa hawana uwezo wa kutimiza wajibu wao.

Je, kama kungekuwa hakuna mitandoa ya kijamii ingekuwaje?
1617683635750.png

Ukisoma kitabu hiki utaona mapungufu ya Katibu Mkuu Kiongozi aliyekuwepo wakati wa tukio la kufariki kwa JPM. LABDA NDIYO MAANA KAONDOLEWA
 
Mkuu mbona ni walewale ameongezeka ummy mwalimu tuu,na pangua pangua ya hapa na pale.
Ameongezeka wapi kwani wew hujui ummy mwalimu alikua waziri katika ofisi ya makamu wa Rais muungano na mazingira, Ummy na jafo wamebadilishana wizara.
 
Makonda alisemwa sana huku mitandaoni ila Jiwe hakutaka kupangiwa.
 
Social media ni moja ya muhimili muhimu ktk kuendesha Serikali mangi ktk nyakati hizi za maendeleo ya Sayansi na Teknolojia acha zako au shule bado kidogo, soma kitu inaitwa E-Governance utaelewa nguvu ya Media na Social media kwa ujumla wake.
 
Social media ni moja ya muhimili muhimu ktk kuendesha Serikali mangi ktk nyakati hizi za maendeleo ya Sayansi na Teknolojia acha zako au shule bado kidogo, soma kitu inaitwa E-Governance utaelewa nguvu ya Media na Social media kwa ujumla wake
We pimbi unatafuta kuolewa humu JF?
 
Tunaamini Raisi wetu Mama Samia ni muungwana mwenye mila na desturi na silka ya Kizanzibari na muungwana akilivuliwa nguo huchutama imani yangu ni kuwa dhulma zote zilizofanywa na mwenda zake atazitatua na kuzipatia ufumbuzi .JF we should be very proud kama sauti zinakwenda mbali na kusikika na serikali ,kusikiliza sauti za raia yake ndivyo inavyotakiwa na hiyo ndio serikali ya wananchi .Tunamwambia Mama Samia Raisi wetu Hala hala Ujiti na macho ncha ina hoho, vyako vyako na wenzako vikikupata vyako peke yako na kikulacho kimo katika nguo yako ,tenda wema wende zako usingoje shukurani .Mama Samia miaka 4 ni sawa na siku nne tu katika kipindi chako cha uongozi kumbuka Allah kakupa mtihani katika maisha yako kuwa MUADILIFU Usidhulumu na weye usikubali Kudhulimiwa.Allah akulinde na kila sui akufanyie wepesi ktk uongozi wako akulinde na mahasidi wako kila ajae na shari waijua yake siri ivunje yake dhamiri asiweze kusimama.Allahumma Amin Thumma amiiiiiin.
Umeandika nini sasa hapa duu kweli uhuru wa mitandao utatuonyesha mengi
 
Back
Top Bottom