Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Na huyu msanii wao wa sasa amewafanya nini hao waliotuingiza mikataba mibovu,au hao waliotetea wizi for 15 years au amefanya nini hiyo mikataba zaidi ya kusababisha hasara zaidi

Better late than never. Ni ngumu sana kuwarudi maana wengi wao ndio wanashikilia some of the strings important for the continuity of the place.
Ila wawekezaji lazima watakuwa waangalifu katika wanayoyafanya. Maana hawajui kama hili lililotokea sasa litajirudia kama wakiichezea mikataba ya umma.
Na mikataba ya umma iwekwe wazi sasa. Tujue mbivu na mbichi. Kuna siku itawaletea shida sana
 
Wewe unadhani Magufuli anapowaita wapumbavu,do you think anawatukana au anawaonea?kishawaona ni Wapumbavu kweli.
 
Kwahiyo ile ilikuwa show iliyoligharimu taifa billioni kadhaa, na wazungu walikuwa right all the time!

Yani bwana mkubwa anapata political gain huku simultaneously akiliingiza hasara taifa.

Alafu tulijitoa kwenye mfumo wa open governance so what else don't we know....
 

..hawawezi kukoma.

..sisi ndiyo tunatakiwa tubadilike.

..kwani aliyekubali "kishika uchumba" cha 300 million badala ya 190 billion ni mtu mzuri kuliko hao waliokuwa wakibadili mikataba enzi za kina Kigoda?

..kuna watu tuna ushahidi kabisa kuwa wameiba lakini tunawaunga mkono.

..wakati huohuo tunawachafua na kuunga mkono dhuluma na ukatili dhidi ya waTz kama Zitto, na Tundu Lissu, ambao wamepinga wizi wa rasilimali zetu muda wote ambao wamekuwa ktk siasa.
 
Mkuu kwa mfano mkataba wa sasa wa Barick na Tanzania, unadhani kati ya Barrick na serikali yetu nani ana pata tabu sana?Ungejua kuwa kwenye yake mazungumzo barick ndo wameshika mpini ungejihurumia
 
Jipya kwa zitto hakipo tofauti na porojo na ndiyo maana watu hawastuki wanamjua vema ,hata kwenye hoja ya buzwagi aliitosa chadema nao wakamtosa siyo wa kumuamini hata kidogo.
Mpumbavu kumuelewa Zito anaanzaje kwa mfano
 

It needs a strategy to win a war. In the book of art of war, the author says you will be a successful general, if you win a battle without firing any bullet.
Kimkakati sidhani kama kuna mambo yalikuwa sawa kwa baadhi ya wanaopinga. Na tutakuwa waongo kutegemea 100% shift of approach over night. That is not practically in the way we work and operate.
Siamini kabisa katika wana siasa wetu. Uzoefu unaonyesha lao ni moja. Ni muda tu ndio unawavuruga na kuwatofautisha.
 
Ni kweli maana kwenye taarifa ya juzi alisema Tanzania tayari imesaini makubaliano na nyie Misukule yake mkaja hapa kumshangilia, hadi pale alipoelezwa kwa fact kuwa amepotosha hakuna mkataba wowote uliosainiwa. Hakuna sehemu mimi nimepinga data zake and I don't want to know Kama ni za kweli au laa. Concern yangu ni kama mpampanaji na wa muda mrefu juu ya uhovyo wa sekita ya Madini na ambaye siku zote alitaka intervention ya serikali kwenye uhovyo huo na akiwa Mchumi alipsawa kujua kuwa intervention hiyo ingekuja na athari hasi kwa sekita ya Madini.Hivyo hakupaswa kuja tena hapa kuleta povu wakati alichokipigania kwa muda mrefu kimefanyika.
A little bit about Kabwe, huyu ni tapeli wa kisiasa ambaye wakati wa Kikwete alitumia muda mwingi kutafuta taarifa dhidi ya viongozi wa Serikali na wawekezaji hasa pale palipokuwa na upigaji na alitumia taarifa hizo kuwa blackmail watu hao ili wamuhonge ili asiwashambulie. So that is the way alivyokuwa anapiga mtonyo during Kikwete administaration. This time hizo information hana, anabaki anaokoteza okoteza, na kwakuwa kwake siasa ni biashara, na kwakuwa sasa hana hizo apportunitiea ndio maana ameamua kuwa Kuwadi.So long Accacia wamemuweka kwenye payroll he doesn't care kama huko nyuma alikuwa Against them.
 
Huwezi kusema tumepoteza wakati, makinikia yamejazana kusubiri mgogoro umalizike ili yauzwe. Pili dhahabu haiozi. Ukipunguza uzalishaji leo, maana yake umevuna dhahabu kidogo ambayo kesho na kesho kutwa bado utaendelea kuvuna.
 

Sahau kuhusu hili Mkuu ,unapoona mikwamo na hizi fujo kati ya Mabeberu na wenzetu (wenye dhamana) basi tambua pana namna ilifanyika.Ikiwekwa wazi basi Asilimia kadhaa hazitokuwepo kwa washika Dau.
 
Siasa hazijawahi kuishiwa ya kuzungumza.

Mleta mada huyu huyu walikua wanapiga sana kelele bungeni kwamba serikali imezuia kuuza mazao nje ya nchi wakulima wanataabika na mazao yao, wanayahudumia kwa gharama kubwa na wanauza bei ndogo sana.

Sasa serikali imeruhusu kuuza mazao nje tena wakenya watakuja kununua kwa fujo, hapo ndipo bei za mazao zitakavopanda bei, na unga utauzwa bei kubwa madukani, na ukiangalia mwaka huu mikoa mingi haiko vizuri kwa chakula kutokana na hali ya hewa ya mwaka huu haikua vizuri.

Sasa basi hapo ndipo utakapowaona wanafiki watakapo kuja mbio kuleta nyuzi zao humu zenye maudhui ya kisiasa za kuilaumu serikali kua haiko makini chakula kimepanda bei.

Ndipo utakapojua kua watanzania tupoje, tunapenda sana porojo, blahblah hata kazi wavivu kufanya, uaminifu sifuri tutachelewa sana sisi.
 
Hasara tuliyopata Zito anasema inatokana na nini? au hukusoma,au hizo kodi anazozungumzia zimeanza kutozwa baada ya mkurupuko?Magufuli atawandanganya na kuburuza sana,na kwa akili hizi mtaitwa wapumbavu sana
Tunamtaka zito ajibu, sio wewe mwenye akili ndogo.
 

..hawakuwa wakipinga bali walitoa tahadhari.

..kwa mfano suala la kushtakiwa, accacia walikwenda mahakamani na waliondoa kesi baada ya kuridhika na offer ya barrick.

..pia kuna maoni ya hao wanaoitwa wapingaji yamo kwenye sheria mpya kwa mfano kipengele kwamba migogoro baina yetu na wawekezaji itatuliwe ktk mahakama za Tz.

..tungekuwa na mjadala wa wazi, wenye nia njema, usiokuwa na chembe za ulaghai, tusingefika hapa tulipofika.

..kuna ulaghai umefanyika kuwaaminisha waTz Barrick wako kwa maslahi yetu. Ukweli ni kwamba Barrick ndiyo waanzilishi wa Accacia na kwa muda wote walikuwa wakimiliki shares nyingi zaidi.

..Baada ya kutulaghai kwamba Barrick hawahusiki na wizi uliokuwa ukiendelea wanaojiita wazalendo wakaingia ktk makubaliano ya kuachana na madai ya 190 billion na kukubali "kishika uchumba" cha 300 million.

..Sasa hapo unajiuliza kama huo siyo usaliti ni kitu gani? Je, hawako compromised?
 
Sahau kuhusu hili Mkuu ,unapoona mikwamo na hizi fujo kati ya Mabeberu na wenzetu (wenye dhamana) basi tambua pana namna ilifanyika.Ikiwekwa wazi basi Asilimia kadhaa hazitokuwepo kwa washika Dau.

Bila uwazi rushwa haiakaa kuja kumalizika. Lazima ifike mahala kuwe na namna ya kuwa accountable kwenye interest za public
 
Huwezi kusema tumepoteza wakati, makinikia yamejazana kusubiri mgogoro umalizike ili yauzwe. Pili dhahabu haiozi. Ukipunguza uzalishaji leo, maana yake umevuna dhahabu kidogo ambayo kesho na kesho kutwa bado utaendelea kuvuna.

Hebu soma hichi kipengele na ukielewe Mkuu :👇


*Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ).
 
Aliyeleta madai ya hizo bilioni 970 anastahili kuangaliwa kama yuko sawa sawa. Alitumia reference gani? Anajua nini kuhusu kodi? Maana anadai kuliko hata mali za uwekezaji wenyewe. How does it work?
 
Shida iko wapi? Kama dhahabu haikuchimbwa na kuuzwa kuna hasara gani ilimradi haiozi wala kipotea? Hawa waliomjengea zahanati na kumpa pesa ili aendelee kuwatetea wamekoma. Makanikia hayatoki na inaonyesha hawamheshimu tena kwa kushindwa kufanikisha malengo yake. Pole nyingi kwako
 
Aliyeleta madai ya hizo bilioni 970 anastahili kuangaliwa kama yuko sawa sawa. Alitumia reference gani? Anajua nini kuhusu kodi? Maana anadai kuliko hata mali za uwekezaji wenyewe. How does it work?

..aliyeleta hayo madai ni serekali.

..na wale waliosema madai hayo yana walakini waliitwa vibaraka na wahaini.

..na waliounga mkono madai hayo wakaitwa wazalendo.

..waTz tunapaswa kubadilika na kukataa kudanganywa kirahisirahisi.
 
Zitto haya mambo huwezi kuelewa na si kila jambo ni propaganda. Wewe Chama umekitelekeza bila kuzingatia maslahi ya wengine huwezi kuengelea ''transactions'' kubwa.

Sasa kama Zitto hawezi kuelewa sijui nani ataelewa; nisaidie kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…