Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

....simpaka hiyo nafasi iwepo yeye anaaamini ktk Fyombo fyadola kumbakisha hapo alipo
Kama next year kutakuwa na uwanja huru japo wa kusemea kisiasa jiwe atapanguliwa mapema sana
Zaidi ya vituo vya afya hakuna kipya amefanya maana ndege haziwahusu watu wa kawaida
 
Kiongozi ungesoma post yangu in line with the context za arguments ya mleta mada ungeona kwanini nimeleta historical data za bei ya dhahabu.

Kwa mujibu wa Zitto
Nchi imepoteza $200 za mauzo ya dhahabu na tsh 450B in tax revenue. In other words kwa lugha ya finance kama wewe ndio bookkeeper wa serikari whatever assets zilizokuwa zinabashiria hiyo income in this instance makanikia you need to wipe that value also from the books aipo tena. Ndio misingi ya hoja ya Zitto in accounting terms.

Mwisho akamalizia in return tutapata $25m tu after all baada ya kupiga hesabu zake zingine which could also be contested. Na kudai matendo ya serikari hayakuwa na maslahi kwa taifa yameleta hasara.

Nilichoandika mimi si kweli anachosema makanikia kwa sababu yapo na thamani yake uwezi kuitoa (kwenye kitabu) ni hela ambayo aijafika ukiamua unaeza iweka kama accrual lakini iko pale pale na kwakuwa bei ya dhahabu imeongezeka thamani tokea hili sakata lianze as inventory makanikia leo yatakuwa na thamani kubwa na ivyo more income kwa serikari sakata likiisha.

Sasa kwa muktadha uo uwezi kusema serikari imepoteza mapato wakati invetory bado ipo, uo ni upotoshaji either kwa makusudi au bahati mbaya.
 
Kipi hujaelewa, wameweka wazi kabisa kutakuwa na mazugumzo kuhusu hizo terms. Acha wazungumze wakubaliane makubaliano yakianza kuwa effected tutakuja hapa tuone kama Kuna kitu tumepata kama Nchi au tumerudi nyuma. Lakini mtu yeyote at this point anayekuja na ramli zake wakati hata makubaliono bado tumueleweje!?
 
Serikali haiko kwenye business ama ku trade trade kwamba kila action inahesabu imagain kiasi gani. Basi isingepiga marufuku wauza bangi maana nao wanaingiza mipato kwenye uchumi wetu. Kila hatua lazima ina costs zake. Wawekezaji wapya niblazima wajipange na kuheshimu rasilimali zetu kutokana na message wanayoipata kama nchi tumeshapeleka message dunia nzima kwamba si shamba la bibi anymore . Kwa hiyo mh zitto hizo ndo gharama zenyewe za kuchukua hatua
 
Wafunge virago. Kama ni kweli mkombozi wa Afrika amekuwa CCM(halibishwi hili) basi sasa wafanye huu Ukombozi, tuonyeshe mfano.

Lazima tuwe wajeuri ama tutakuwa tunapiga ramli ya mlevi anayetapika!

Wakati ni sasa wakati vuguvugu hili likiwa limetanda AFRIKA ...jamani mtu kwao. RASILIMALI ni zetu ati watuchimbie wauze halafu tupate kaduchu tena kwa masharti...shaabash!


Tukachimbe wenyewe, watu wapo tayari.

Mh. Zitto,
Pole na dhoruba.
Kumekuwa na tuhuma haswa kwa vyama vya siasa visivyo madarakani kuwa hamna mbadala? Tuache sayansi zote hizo za sijui riba GDP, mkato, marejesho, mapato, sekta, bajeti na mlolongo mrefu.Rasilimali watu ipo! Vichwa vipo, sululu zipo, polisi wapo, jeshi wapo.
Mbadala upo wapi?
 
Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.

Faida na hasara ni tofauti kati ya investment costs na returns zake. Hasara ni pale ambapo returns zinakuwa ni ndogo kuliko investment costs. Siwezi kusema tumepata hasara au faida bila kujua tuli-invest nini. Opportunity loss au opportunity cost siyo hasara; haiingii kwenye income statement au balance sheet yoyote ya accounting.
 
Ilibudi tuwaache acacia waendelee kutulalia . Apo Zito sijakuelewa mi nafikiri hii hatua ni nzuri kutusaidia ili tusije ingia mkenge miaka ijayo. Fikiria yaani wanasafirisha mchanga pamoja na makenikia. Sisi wanatuachia mashimo ambayo ni janga kubwa.
 
Unatafuta 30 to 40 bullets? Only TL can survive
 
Yaelekea hujaelewa.

Unachotakiwa kujua makinikia hayazalishwi tena. Hayo yaliyopo Dar thamani ni ndogo sana. Na wala siyo thamani ile iliyooneshwa kwenye zile report za kipuuzi za maprofesa wapuuzi.

Sahizi kwenye makubaliano, tena tunawaruhusu waendelee kuzalisha kama zamani kwa utaratibu wa zamani. Sasa kwa nini tuliyazuia?

Kama yale makubaliano yale yakitekelezwa, ukweli hakuna chochote ambacho tutakipata kuzidi mwanzo. Makubaliano yale yatakuwa ya manufaa sana kwa Barrick.
 
Mabadiliko yaliyokuwa yanatakiwa ni yenye kuleta faida.

Ni sawa na mtu ulimkodisha nyumba kwa sh 2m. Ukaamua kutaka kupata kodi zaidi kwa madai kuwa mpangaji wako ingawa mtaji wa biashara yake ni sh 10m lakini kwa miaka 10 aliyofanyia biashara yake kwenye jengo lake anepata faida ya sh 400m. Ukaenda kumtoa, vitu vyake ukapeleka stoo yako ukidai alikuwa anakupunja kwenye malipo ya kodi.

Ukaanza kujadiliana naye kwa miaka minne, baadaye ukaonekana wewe ni mpuuzi maana biashara ya mtaji wa milioni 10 haiwezi kutengeneza faida ya sh milioni 400 ndani ya miaka 10.

Kipindi cha miaka 4, ukakosa 8m. Baadaye ukakubaliana akufanye kuwa sehemu ya mradi kwa kupewa umiliki wa upendeleo, pia awe anakulipa 2m kama kodi kwa mwaka ila wakati wa kufunga mahesabu ya nwezi, akuhusishe na wewe lakini wewe hutaruhusiwa kufanya maamuzi kwa sababu hisa zako ni za upendeleo tu.

Lakini mkakubaliana pia, japo madai yako ya kusema nilikuwa napata faida ya milioni 200 yalikuwa ni ya uwongo, kwaajili ya kuwa na uhusiano mzuri, nitakupa sh laki 3 ila nitatoa gharama za matengenezo ya mlango ambayo ni sh 240,000. Iliyobakia sh elfu 60 nitakuwa nakupa kidogo kidogo kila mwaka sh elfu 8.

Pia mkakubaliana kuwa kwa kuwa wewe ni mpuuzi na mwonevu ili usinifanyie tena aliyoyafanya, kuanzia sasa, kama tutashindwa kuelewana, itabidi twende mji wa jirani unaitwa Sinapore, kule kuna mtu mmoja anaaminika sana, akitoa uamuzi wake ndiyo utakuwa wa mwisho, wote mkaridhia.

Hivi hapo umepata hasara au faida? Kama ni faida, ni ipi hasa?
 
Hivi wewe umeishia la ngapi, unadhani hayo mabadiliko yangeweza kufanyika bila kuleta athari yoyote!?

Mkuu dunia ya sasa hatuendi hivyo, ndio maana haya maneno ya kiingereza, smooth engagment, smooth handover, smooth transition... Kabla hujafanya jambo lolote unatakiwa kwanza ulisome ulione namna ya kuliendea ili utakapolianza lisilete madhara.. Ndio maana kukawepo mabadiriko chanya na mabadiriko hasi..

Miaka ya zamani ili ulete maendeleo ilikuwa lazima uumize/uue/utese watu ndio maendeleo yatokee mfano China, German nk lakini kwa dunia ilipofikia sasa huhitaji kuua au kutesa watu kufikia maendeleo bali ni akili tu mfano South Korea, Malysia, Brazil, Indonesia,India nk..

Hili makinikia halikuhitaji nguvu nyingi bali lilihitaji hesabu na akili kuliendea ili liwe na faida kubwa za miaka mingi kuliko hasara, kabla ya kuliendea lilihitaji maandalizi ya kimyakimya na uchunguzi wa kina wa watalaam hata kwa miaka 2-3 then baada ya hapo ungetengenezwa utaratibu wa kulifanya bila kuingilia operations mpaka liishe..
 
Kama hayazalishwi si yanabaki chini, mi nadhani wwe hujui hata maana ya makinikia ni nni na hujui yanatokana na nni, nenda kwa wachimbaji au kwenye migodi ndo urudi kuchangia, siku wakijenga smelter utayaona mengi tu kwa kuwa hayaondoki kwenda nje, na hiyo pesa iliyosimama itatoka nyingi tu, kuliko hawa waliokuwa wanasafirisha huku wakiweka na dhahabu pure. kwa hiyo unataka kusema na nyerere alipata hasara kutoruhusu wazungu kuchimba hiyo dhahabu?

 
Hebu acha upuuzi aisee.

Upuuzi? Ukikumbushwa njia ya kisayansi ya kujenga hoja na kujadili issues kwa manufaa ya nchi yetu unaita upuuzi! Wewe ni mtu mzima sasa hivyo ni vizuri ukaepukana na kauli za kitoto. Kumbuka kuna siku ulijipambanua hapa hapa JF kwamba una umri mkubwa kwa kutaja mahali uliposoma sekondari na miaka. You are about my age my dear!.
 
details of Tanzania-Barrick deal emerge, gazeti la citizen limeandika tumepigwa na Wanaume huko kiukweli.
 
nyie wataalamu wa jamiiforums ndio mnampoteza zitto
 
Wewe umeshindwa kujibu hizo data alizotoa na baada ya kuona hauna hoja za kumpinga ndio ukaishia kumshambulia.!

Watu kama wewe ambao ni "The Praise Singers/Boot lickers" kamwe hiyo hulka yenu haiwezi kuwaruhusu muwe na rational reasoning kwani huwezi kutetea kosa linaloleta madhara kwa nchi kwa kisingizio cha kuwa ulikuwa na nia nzuri. That's a feeble defence even in law.
 
Hii ilikuwa ni vita ya vikundi viwili ndani ya chama Tawala. Sasa hivi ndio yajionyesha wazi, kwani kwa msaada wa Musiba bila hata yeye mwenyewe kujua hajawavua nguo wastaafu bali hata walioko madarakani.

Mmoja mmoja watajitokeza na kutubu. Tafakari yafuatayo:
  • Onyo la Benki ya dunia kuhusu madeni kupanda kwa ghafla
  • Korosho, kunde, Mahindi (Tumepoteza zaidi sana hapa mwaka jana kuliko hiyo ya Dhahabu)
  • Makinikia
  • N.K
Watajipambanua wenyewe. Sisi tutulie tu kwani kuunga mkono kikundi hiki au kile ni kujipalia mkaa tu wote ni wachafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…